



Alikiba anapenda kuwashukuru wale wote waliojitokeza kwa mamia kumsupport Washington d.c na Minnesota, Anawahaidi wakazi wote wa kansas kujitokeza kwa wingi kwa sababu amepania kuwasuuza roho zao na show kabambe.
Usingoje kuhadithiwa hakikisha unajionea mwenyewe kipaji cha mwanamuziki wetu kutoka nyumbani.
Wengi wamekuwa wakijiuliza kwa nini kijana huyu anapendwa hivi kila pembe ya dunia. Jibu ni rahisi sana. Ukiwachilia mbali kipaji na uwezo wake mkubwa wa kutawala jukwaa, nje ya jukwaa hana nyodo, halewi wala havuti na pia hufika kazini katika muda aliopangiwa na akianza amenza, tofauti na wasanii wengi wengine wa kibongo ambao hujisahau kwa kujiona wao ni wao.
Madhali Ali keshaambiwa kuhusu adabu za mwezi mtukufu. Ni vizuri tujue kuwa watu huwa wanapata laana kwa mambo ambayo wangeweza epuka kirahisi. Mjumbe hauwawi!
ReplyDeleteNdugu Ali
ReplyDeleteHongera ndugu maana kama ni wasanii wenye exposure kwa sasa nafikiri wewe unaongoza kwa sasa maana hiyo tour yako imekuwa ndefu. Ni world tour.
Ni matumaini yangu kwamba itakuwa imekufunua macho na ukirudi utakuwa mfano kwa wasanii wenzio.
Nakutakia kila la kheri
DM
Mwezi mtukufu unakataza mtu kutafuta ridhiki yake?Mbona Jk anafanya TOUR zake ndani ya mwezi huu mtukufu na hakuna anayesema?
ReplyDeleteHivi huko nyumbani hakuna waislam wanaendesha biashara za migahawa,BAR na zile tusizoweza kuzitamka hadharani ktk mwezi huu mtukufu?Hii ni karne ya 21 sio karne ya 8 badilikeni kimawazo.Kwanza mimi ni wasiwasi kama huyu dogo atarudi bongo tena,ameshakimbia mavumbi ya bongo huyu.
Kweli ndo maana umeitwa Mbigiri. Wadau usipofaham jambo si lazima uchangie, ukizungumzia karne ya 21 utaniambia watu wanaenda na wakati, ya usasa umezidi, napenda kukukumbusha Ndg Mbigiri, uislam hauna usasa, waislam wa karne ile ibada yao haijatofautishwa na wasasa...riziki anapanga Allah, kwahiyo Ali angestahamili kwa kusheshimu mwezi mtufuku naamini angepangia riziki nyingine na ziara za jk huwezi linganisha na Ali Kiba, kuna upataji wa riziki kwa njia haramu na halali umenipata...this is islam predictions, punguza munkari!!
ReplyDeleteKATIKA PICHA YA TATU NAWAONA WANANGU WANYEWE WA D.C THA SWAHILI WAKIWA NA ALI KIBA, NICE TO SEE YOU GUYS TOGETHER. I LIKE THEIR MUSIC
ReplyDeleteooooh! my God!!!! the show wow.. fun fun fun....ama kweli we ni msanii na nashukuru kwa burudani.. karibu tena wichita
ReplyDeleteWanaom-sponsor Ali Kiba:Hamuwezi kumfanyia maharifa huyu kijana akakutana na wanamuziki wa uko waliopiga hatua kubwa sana kimuziki wakampiga 'fafu'kidogo ya kumsaidia kimuziki ili naye aweze kufanikiwa kama wao?.I am talking about watu kama akina R.Kelly,P.Diddy,Akon,Usher R n.k, au ni ngumu sana na gharama kuwapata?Sijawahi kufika USA,samahani kama nitakuwa nimekosea.
ReplyDelete