Ndugu yangu Michuzi,
Hongera kwa kuukwa ubalozi wa Zaina na naoa uko Ujerumani sasa. Unarudi lini bongo. Mbona huku Italy haujigi?

Aisee nashukuru safari yangu ya kurudi huku Cesena, Italy, ilimalizika salama na jamaa wote nilikuta wazima. Wanawasalimia sana wadau wote na kutoa pole ya mfungo kwa wote wasio makobe.

Nakutumia picha hii ya mzinga niliolishwa na daladala pale magomeni siku ya pili tu toka nilipofika Dar. Unaweza kuita karibu mgeni maana jamaa alikuwa amechomekewa na daladala ingine, sasa wakati anarudi rivasi, mie ndio nakatiza na hilo gari dogo. Nikasikia kochooo!


Bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila gari iliumia vibaya mlango wa nyuma kama unavyoona. Majeraha yangu makubwa ni hasara niliyoipapa kwani huyo dereva wa daladala alinikomalia na kusema yeye hana kosa ati mie ndiye niliyemgonga.

Zogo liliendelea hadi kituo cha polisi magomeni ambako jamaa alikazania kuwa mimi ndiye mwenye makosa, akisema sheria inatamka wazi kwamba aliyegonga kwa nyuma ndiye mwenye makosa. Nilijitahidi kujieleza, wapi. Ah, nikaachana nao na kurudi nyumbani. Kesho yake nikapeleka gari kwa fundi wa mabodi akaninyooshea na kupiga rangi. Nilitumia visenti kibao.


Namalizia kwa kutoa wito kwa wenzangu wanaorudi nyumbani wawe wangalifu sana na madaladala. madereva wake wengi hawana adabu na sheria za barabarani wao hawazingatii kabisa, tena hata mbele ya askari w trafiki.

Ni mimi yuleyule
B. Chibiriti



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Wewe Chibiriti ebu uwe una post vitu vya maana hapa. Inabidi uwe mjanja kuendesha gari bongo, kama ndio mara ya kwanza unaendesha bongo then you need a trainer first. Tuachie Michuzi atuwekee news za maana kwenye blog hii ya jamii sio unaweka insha zako hapa kila siku zisizo na maana.

    ReplyDelete
  2. Chibiriti bwana una makosa,
    hebu angalia upana wa barabara, na hata kama ungekua muangalifu ungeshamuona tayari huyo anayerudi nyuma, kama ungemuona anakuja kwenye upande wako ungempigia honi ili ajue kinachoendelea.
    hapo unaonyesha kabisa wewe ndio mwenye makosa

    ReplyDelete
  3. BONGO HAMNA SHERIA ZA BARABARANI. SHERIA IKO MIKONONI MWAKO, BEBA BASTOLA KWA GARI. KUNGEKUWA NA WATU WENGI KAMA AKINA DITOPILE MADEREVA WA DALADALA WANGENYOOKA!

    ReplyDelete
  4. Pole sana Chibiriti ila kwa taarifa yako bongo sheria za barabarani wengi hawazijui si madereva tu mpaka maaskari wa trafiki kwani wote hamna kitu. Wewe uliona wapi dereva ndiye anayesema eti hana kosa wakati askari wapo ambao wangepima na kuona kama kweli wewe una kosa au la. Nakumbuka hata mimi wakati niko nyumbani bongo nilikuwa najiona najua sana kuendsha gari kumbe ilikuwa ni ujuha tu.

    ReplyDelete
  5. Chibiliti siku hatunyooshi nunua panel na mlango mwingine

    ReplyDelete
  6. anon wa sept 27 8:58 hivi uko nchi gani, uliposema "uliona wapi dereva ndie anayesema eti hana kosa wakati askari wapo" jawabu ni kuwa hapa uk ndivyo ilivyo. mkigongana mnamalizana wenyewe, mnabadilishana details za insurance zenu, details za gari na majina yenu, kama palikuwepo mashahidi mnachukuwa details zao kwisha kila mmoja anaondoka zake, kama ni kuita recovery people mnaita. Polisi anaitwa na kuja kwenye ajali pale {kwa maneno yao} ajali inapokuwa ni 1.very serious (watu wameumia), 2.fatal (mtu au watu wamepoteza roho) au 3. ajali imezuia flow ya traffic. Pia wanakuja haraka kama ukisema dereva wa gari la pili anaonekana kuwa amelewa. vyenginevyo mnamalizana wenyewe. kama hakuna alokubali lawama basi ni heri uchukuwe picha na uchora kwenye karatasi roughly sehemu ilipotokea na details zozote zile muhimu na uwapelekee insurance wako ambao wao watawasiliana na insurance wa gari la pili na wana deal na kila kitu kwa niaba yako. ukitaka unaweza kuwaita polisi lakini watachukuwa muda kuja, yaani operator anakwambia kabisa ni heri mkamalizana wenyewe.

    anyway point yangu ni kuwa hapa uk ukigongana, dereva mmoja hukataa na mmoja hukubali lawama na wanamalizana wenyewew bila ya kuita polisi

    ReplyDelete
  7. Sheria zingine ni vigumu kufanya interpretation, wanaposema kama mtu ukimgonga kwa nyuma ni wewe ndiye mwenye makosa, ni kwamba kama gari zote mbili zilizohusika katika ajali hiyo zilikuwa zinaenda mbele/upande mmoja na wewe wa nyuma ukamkonga wa mbele, hii ikiwa inamaanisha kuwa mtu akiwa mbele yako hawezi kuona nyuma au hana haja ya kuangalia nyuma mahala ambapo ameshapita salama, lakini hii ya CHIBIRITI ni kwamba Daladala ilikuwa ina rudi nyuma/reverse baada ya kuzuwiwa mbele na nyingine na kumgonga CHIBIRITI wakati aki-reverse, kwa maana hiyo mwenye Daladala ana makosa ya kugonga, kwani kabla hujarudi nyuma ilimbidi kuangali nyuma kama hamna kipingamizi chochote cha kumzuwia yeye kufanya hivyo, na hata hivyo hakukuwa na haja ya yeye kurudi nyuma alichotakiwa kufanya ni kusubiri mpaka ile iliyomzuwia kwa mbele kuondoka naye aondoke. Pia ukiangalia hiyo picha ya CHIBIRITI there is no way angegonga mpaka akapitiliza hadi mlango wa nyuma, how on earth that could happen before the car stop, it is utterly and absolutely immpossible, na kwa ushauri wangu bado hapo kuna kesi ya kujibu na anaweza kwenda mahakamani back na kushnda na kulipwa fidia ya matengenezo ya gari yake, and this will happen only if the courts of law are free and democratic free from corruption. JUST APATE MASUMBUKO LAMWAI MZURI WA KUMTETEA, yo know what I mean innit?.

    ReplyDelete
  8. Pole sana bwana mkubwa,kama mlitoka salama shukuru mungu.

    ReplyDelete
  9. Insurance companies siku zote huambia wateja wake wasikubali makosa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...