Katika kuunga mkono mawazo ya wengi lile onyesho la msanii Ali Kiba lilokuwa lifanyike tarehe 20 mwezi huu yani jumamosi ijayo jijini Atlanta sasa limesogezwa mbele hadi tarehe 25 mwezi wa kumi (25/10/2008).
Hii ni katika kuadhimisha mwezi huu mtukufu wa Ramadhani pia ratiba hiyo imebadilika kutokana na Tufani kubwa iliyoukumba mji wa Houston Texas ambao kutokana na ratiba walikuwa wamuhost Kiba wikeend hii.
Kwa kukubaliana na ombi lao basi Ali Kiba atakuwa Houston tarehe 20 na atakuwa Atlanta tarehe 25 mwezi ujao.
Tunawaomba radhi kwa usumbufu wowote uliotokea!
helpers10 Ent. Inc.,
Shakaentertainment,
JFC Ent.
Akhsanteni!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Ali Kiba umejitangaza na umepata pesa pia tunakuomba ukirudi Bongo endeleza mziki sio matanuzi wakati ndo huu.

    ReplyDelete
  2. sababu kuu ya kubadili tarehe ni huo mtanange wa Hurricane na sio mwezi mtukufu.usione wadau humu kama watoto wadogo kwa kutoa sababu za kudanganyia pipi.

    i hope ndugu zetu wote huko Houston wako salama salimini.

    ReplyDelete
  3. Na kweli hata mimi nilimuona huyo aliyeandika hilo tangazo kama mswahili vile. mmmmm
    mara ni kuunga mawazo ya wengi mara ni Ike. Mashow yote ya nyuma kwa nini msiunge mkono mawazo ya watu toka mwanzo......

    Acha kudanganya watu and be honesty to yourself na acheni unafiki

    ReplyDelete
  4. Naomba kukusitiza kuwa onyesho litafanyika October 25th na sio September 25th kama mkuu wa wilaya alivyoweka. Tunazidi kuomba radhi kwa usumbufu.

    ReplyDelete
  5. nadhani kijana Ali ameona kuwa atafanya makosa mbele ya mungu wake kwa kudharau mwezi huu mtukufu kuliko miezi mingine na ameamua kusubiri mwezi mtukufu upite ndio aendelee na kazi yake.

    ReplyDelete
  6. Ali kiba yuko kazini, acheni kumsakama, watu wengi wanafanya kazi maeneo ambayo madili ya dini zao yanawafunga, LAKINI HUWA HAWACHUKUI LIKIZO katika vipindi hivyo.Muacheni Ali K.

    ReplyDelete
  7. I think H-town wanahitaji kujirusha baada ya Balaa la mzee IKE. Ali Kiba usiwangushe.Poleni jamaa yoooooooooooooote huko mlioathirika kwa namna moja ama nyingine.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...