barabara ya sam nujoma rodi inavyoonekana. juu ni upande wa kwenda mwenge, chini ni upande wa ubungo. barabara inakaribia kumalizika ujenzi na foleni zimepungua kwa sasa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nashukuru mkuu wa Wilaya ya nani hii kutupa news lakini wasiwasi wangu ni pale Darajani kama napo wamerekebisha vizuri ni wazi foleni itapungua hapo maombi watengeneze na bara baba za mitaani hapo watakuwa wamepunguza foleni hata mjini mimi sie elewi hwa watu wanafikiri nini.

    Mdau

    ReplyDelete
  2. Hapo ndio mnaisififa barabara karibu inaisha na hivyo vifusi pembeni!!? barabara haijamalilizika haina sehemu ya waendao kwa miguu au waendesha baskeli kwa ujumla ni uchafu mtupu.barabara itaharibika kirahisi sana pindi mvua zitakapoleta balaa yake...jamani hamuoni barabara za wenzenu?

    ReplyDelete
  3. Kweli Roma haikujengwa kwa siku moja. Halikadhalika Dar nayo haitajengwa kwa siku moja.

    Mji unazidi kupendeza. Miaka 50 ijayo itakuwa kama New York

    ReplyDelete
  4. ...waweke na drainage system, siyo mvua ikinyesha maji yote yanazagaa barabarani

    ReplyDelete
  5. naona ma-engineers wengi humu ndani...hehehe
    Pia naona mafisadi wameamua kusamehe chache zitumike kuleta maendeleo kidogo

    ReplyDelete
  6. WEWE 6:47 UNAUHAKIKA KUWA NEW YORK HAIZIDI KUJENGEKA? HIVYO SISI TUTAWEZA KUIFIKIA? HILO SAHAU KABISA, KWANZA TUANZE KIFIKIA BAADHI YA MIJI ILIYOPO AFRICA KITU AMBACHO PIA NI NDTOTO KWANI NAYO INAZIDI KUENDELEA. WAZO LAKO NI SAWA NA LILE LA WATANZANIA WALOTAKA TUSIJIUNGE KATIKA SOKO LA EA MPAKA MIAKA ISHIRINI IJAYO TUTAKAPOWEZA KUIFIKIA KENYA, LAKINI KENYA NA UGANDA ILYOKUWA SI LOLOTE WALA SI CHOCHOTE ZINAENDELEA KWA KASI, ILA KITU KIMOJA TULICHONACHO NI UBISHI WA KUTOKUBALI UKWELI, HUO NAO UNAENDELEA KWA KASI HAPA NCHINI.

    ReplyDelete
  7. Wabongo hawana shukurani, hawabebeki, hawaambiliki, hawaeleweki, hawaoni!! Angalia kama huyo mtoa maoni wa 2! Kwa taarifa yako barabara hii Tanzania hakuna nyingine!

    ReplyDelete
  8. Kweli wabongo hatuna shukrani.Mimi nadhani serikali ikifanya kitu kizuri tuisifie.Barabara za Kilwa,mandela,na hiyo ya Sam ni hatua nzuri.Majengo ya kisasa yanajengwa.Forget about America,Europe,Mimi binafsi nimetembelea miji mingi ya Africa.Dar inazidi majiji mengi ya Africa!Majiji mengi ya Africa yalijengwa na wazungu wakati wa ukoloni,sisi tunajenga wenyewe(Hatujihamini ndiyo tatizo).Tumeshakuwa na dhana mbaya eti Dar haitaweza kuifikia New York(Pourquoi?).Mdau kasema ukweli.Kidumu chama cha mapinduzi.

    ReplyDelete
  9. Nadhani hao wanaodhani ulaya na marekani barabara zao zilikuwa safi mara moja nadhani wanachemsha. Pia hao jamaa hawakujenga barabara siku hizi mbali wanakarabati tu kwani barabara zao nyingi zilijengwa zamani. hawana ujenzi mpya kama sisi so huwezi kulinganisha mtoto aliyezaliwa akarithi kila kitu toka kwa babake na yule ambaye kalelewa na wazazi wakambo kisha wakamuibia kila kitu, including wamewafanya watoto wake wasiwaze mapya mbali ya kusifia familia ya baba wa kambo.

    Nasikitika sana nikisikia watu wanaoisifia kenya kimaendeleo utadhani kama kuna kitu kikubwa sana. Nawaambieni tembeleeni kenya na mujaribu maisha kenya kama mutaweza. Serikali yao inapesa lakini watu wake afadhali bongo watu wanabangaiza wakatoka.

    wakenya wengi walio huku walikuja kama wakimbizi baada ya maisha kubana kule, just ongea nao and uende ukaone. sasa uganda inakipi chakusifiwa!!!

    Please bongo inaprospect safi sana tukitulia tukafanya mambo badala ya majungu!!

    G7
    !!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...