Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini leo (Jumanne, Septemba 2, 2008) mchana kwenda Lusaka, Zambia, kushiriki katika mazishi ya kiongozi wa nchi hiyo, Rais Levy Patrick Mwanawasa. Rais Mwanawasa anatarajiwa kuzikwa kesho.

Rais Kikwete ameambatana na mkewe, Mama Salma Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Rais Mwanawasa alianguka ghafla na kupata kiharusi Juni 29, mjini Sharm El Sheikh, Misri, siku moja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika mjini humo.

Alikimbizwa hospitali Paris, Ufaransa, lakini alifariki dunia Agosti 19. Rais Mwanawasa alitarajiwa kufikisha umri wa miaka 60 kesho.

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, baada ya kuwa amewasili Lusaka, Rais Kikwete leo atatia saini kitabu cha maombolezo na baadaye kwenda Ikulu ya Zambia kumpa pole mjane wa Rais Mwanawasa, Maureen Mwanawasa.

Kesho wakati wa mazishi, Rais Kikwete atahutubia waombolezaji kwa niaba ya wakuu wenzake wa serikali na nchi za AU katika nafasi yake ya Uenyekiti wa umoja huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wana Jamii naomba kuuliza Vasco Da Gama ni nani katika hitoria?!?

    ReplyDelete
  2. Hilo swali hapa si mahali pake angalau ungeluliza alipokuwa ziarani marekani, sio hapa akienda msibani au kuhani jirani, huo ni ujirani mwema na kila binaadamu anatakiwa ampende jirani yake kama nafsi yake, wanasema fumbo mfumbie mjinga werevu tumeng'amua.

    ReplyDelete
  3. Wewe una wasiwasi gani ndugu yangu?Rais wetu anaweza kwenda hata Post Graduate Marekani Mwaka Mzima na Nchi hii isitetereke!Yupo Makamu wa Rais wa Muungano Dr.Shein;yupo Waziri Mkuu Pinda;yupo Rais wa Zanzibar Dr.Karume;yupo Waziri Kiongozi Nahodha;bado hujagusa Maspika wetu!Huu ndiyo Muundo wa Serikali yetu kwa mujibu wa Katiba!Shida yako nini ndugu yangu?Usukani Mmoja lakini una Madereva Kibao!Kasi Mpya Nguvu Mpya Ari Mpya!Maisha Bora kwa Wote!Na Baaaadooooo.......................watu watakaanga ubuyu hapa nakwambia!

    ReplyDelete
  4. Wewe una wasiwasi gani ndugu yangu?Rais wetu anaweza kwenda hata Post Graduate Marekani Mwaka Mzima na Nchi hii isitetereke!Yupo Makamu wa Rais wa Muungano Dr.Shein;yupo Waziri Mkuu Pinda;yupo Rais wa Zanzibar Dr.Karume;yupo Waziri Kiongozi Nahodha;bado hujagusa Maspika wetu!Huu ndiyo Muundo wa Serikali yetu kwa mujibu wa Katiba!Shida yako nini ndugu yangu?Usukani Mmoja lakini una Madereva Kibao!Kasi Mpya Nguvu Mpya Ari Mpya!Maisha Bora kwa Wote!Na Baaaadooooo.......................watu watakaanga ubuyu hapa nakwambia!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...