
JK jioni hii alikuwa miongoni mwa ndugu, jamaa na marafiki waliofika hospitali ya muhimbili kitengo cha mifupa kumfariji mpiganaji athumani hamisi aliyelazwa hapo kufuatia ajali ya gari aliyopata wiki iliyopita huko kibiti, wilayani rufiji, mkoa wa pwani alikoenda kikazi

JK akiongea na athumani hamisi huku mchumba wake aliyewasili jana toka marekani akiwa karibu

baada ya kumjulia hali athumani hamisi, JK alipita kwa wagonjwa wengine na kuwafariji. hapa anamfarji david kasembe wa mamlaka ya bandari ambaye pia alipata ajali siku moja na athumani, na wote wako wodi moja hapo MOI

supa modo happiness magesse na mkuu wa itifaki wa kamati ya miss tanzania albert makoye nao walikuwepo kumpa pole mpiganaji athumani hamisi

mzee hamisi msengi, baba mzazi wa mpiganaji athumani hamisi akimfariji mwanae leo.
hali ya mgonjwa inaendelea vizuri ingawa anahitaji matibabu zaidi nje ya nchi. habari zimeingia sasa hivi zinasema serikali imeamua kumpeleka akatibiwe nje na taratibu zote zimetimia. huenda akasarirshwa kesho ama keshokutwa, ila nchi atayokwenda itajulikana kesho. athumani amejeruhiwa mfupa wa mgongo na shingoni
tunamuombea mpiganaji mwenzetu nafuu ya haraka
Pole kaka Achu, mmh ila hii ya mchumba kuja kuuguza kaazi kwelikweli, hemu nyie kina dada sasa mtulie kaka apone kwanza, mana hapo wanaweza tokea kina dada 2 -3 wakajiita wachumba, kasheshe hapo,,tena unakaa USA, mmh lazima kuna wake wenza hapo, jamani Achu upone uoe sasa,hii BADO NIPO NIPO, italeta magomvi mbele ya rais hapo,,watu watakuja mwagiana chai ya mgonjwa BUREEEEE
ReplyDeletehilo ndo PENZI, katika SHIDA NA RAHA, sio umesikia mwenzio kapata ajali unaishia pole ya simu mana unajua ukija hata nguvu hanazo, kwa hiyo hamtaenjoy..sasa mdada katoa nauli, kapanda ndege, safari ndefu kumuwahi mchumba, hili ndilo PENZI...i hope uko peke yako, mana kaka zetu mmh, NDOO NA VIDUMUUUZ
ReplyDeleteSio kuwa watamwagiana chai tu, hata uji wa mgonjwa inapobidi, we siku zote uko marekani, sisi tunaye hapa, ati wewe ni msomi sana wataka kumfariji, shauri yako.
ReplyDeleteanon wa 10:27 umeniacha hoi, mana mi ndo nimeandikwa hiyo ya kumwagiana chai, sasa we umenipa ya uji, duu nimecheka sana mana uji wa moto balaaa..
ReplyDeleteWe wapanda KLM, wenzio wamepanda daladala zao washafika Muhimbili, wamletea mgonjwa chocolate, wenzio wammbebea mahanjumati na wamekuja wamejivukiza udi, shurti wanukia kinyumbani,,,khe kheeee, nicheke mie..LOL!!!ngoja niimbe mie TUTABANANA HAPAHAPA, NAKULA NAWE SAMBAMBA....TUTABANANA HAPAHAPA NIKO NA WEWE BENET,TUTABANANA HAPAHAPA NIKO NA WEWE SIKWACHI, NA UKIZUBAA NAKUTOA KAPA, UKILEGEA......
mmh, mmenichekesha, kweli uke wenza mbaya, lakini acheni jamani uke wenza una utamu wake,ni CHALLENGE... yule bi wa pembeni anakuwaga ana utundu mwingi sana, anamzidi mwenzie vitu vidogovidogo,shurti kwa kumuongelesha Mr.kwa sauti nyororo, "Pole bwana angu" basi tayari bwana akamatwa, ukizingatia kwake anaitwaga " we baba Sikudhani wewe"..he heeee, LOL!!!
ReplyDeleteTeh teh taarabu hizi zina mengi, real life:
ReplyDeleteAmekushit huna maana, kila siku kiguru na njia nimemchukua mchana, mchana eeh mchana, mchana jua la utosi mchana..
haya jamani mungu amsaidie kaka yetu apate matibabu yote ya lazima na apone.
Pia wifi amalize shule, aje akae na mwenzie wawe mwili mmoja (labda!!!!!???)mana bongo sikuhizi kuna totoz, ni balaaa.
Huyo aloingia na mipasho huko juu shogaa hilooo hamna lolote! Kijiwe kimeingiliwa leo, makubwaa madogo yana nafuu!
ReplyDeleteMPIGANAJI, Mungu atakusaidia upone haraka. amina.
Ndugu Athumani, Mwenyeezi Mungu atakuafu, INSHAALLAH. Dua zetu ziko pamoja na wewe na ramadhani hii. Amin.
ReplyDeleteroho zinakuumeni tu nyie wasabasi! mara daladala mara chokoleti mara ndege mara mahanjumati.ana mwenyewe huyo na ushahidi ndo huo, acheni kujibamiza mtatoka na manundu pus nyiee!
ReplyDeleteHABARI NDO HIYO!
Litakaye mkuna limemchoma!
Naomba kuuliza wadau? Huyu jamaa alikuwa anafanya kazi serikalini? Au inakuwaje hadi serikali inatumia PUBLIC FUNDS kumpeleka kwa matibabu nje ya nchi? Kama ni muajiriwa wa serikali...ni kwa kigezo gani yeye anapewa umuhimu zaidi ya waajiriwa wengine wa serikali waliopo na walioshakuwepo matibabuni katika kupelekwa nje kwa matibabu?
ReplyDeleteKama serikali ingekuwa inapeleka watumishi wake wote kwa matibabu nje basi isingekuwa ishu...lakini mimi ninavyoona hii ni mara ya kwanza...au ni moja ya mara chache hili linafanyika. Ni vigezo gani vinaifanya serikali kuchagua nani wa kupeleka nje na nani wa kutosa? Mkumbe hela inayotumia ni ya wananchi hapo jamani. Serikali haina source of income zaidi ya taxpayers money.
Mkuu wa wilaya usibanie hili swali langu. Najua linagusa mahali pakali na pagumu...lakini ni lazima vitu kama hivi vizungumzwe na kuleta mwangaza zaidi katika serikali.
mtoto
Congrats serikali.Ugua pole Hamisi.
ReplyDeleteTunaomba serikali isifanye ubaguzi iwasafilishe wote nje kwa matibabu huyu mfanyakazi wa bandari naye wamwambatanishe maana ajari haikuchagua...na huyu David Kasembe nae wampeleke..
ReplyDeleteMdau Finyango
linatawakaba sana mliozoea kuzitumbua dollar, haya anayezitumaga amekuja, haoooo mmeliwa, mlidhani mnachuna kumbe mwatoa company tu, mwenye gauni lake amerudi.
ReplyDeleteWanawake wa kiswahili, gauni umelikuta unaambiwa mwenyewe yuko nje ya nchi, basi unajichukulia unavaa weee, vaa basi mara mojamoja akija asikute limechakaa sana, hapana, unavaa weee, na kuwatambia watu ooh gauni langu ohh la bei mbaya, haya mwenye gauni kaja huyooo, toba, tena kaja ghafla.Kazi kwenu.
Pole mgonjwa, mungu atasaidia utapona kaka, inshalaah..
ReplyDeleteWifi, kaa macho,bongo sikuhizi kumeharibika, watakuja wakufungie safari za Bagamoyo kutafuta msaada huko,utakosa bwana na KLM,utarudi kijijini kwenye kilimo.Kama uko busy sana, tupe sie hiyo nauli tukuendee safari,tukakukingeni.Salaam zako.
Mhu makubwa, Mgonjwa pole Mungu akuafu akujaalie salama. Haya kina dada msivunjane ndimi na kumwagiana uji wa mgonjwa bure, kwani mlikuwa hamjui huyu kaka ni mwislam, hapo bado kuna nafasi ya watatu zaidi mpaka watimie wanne ili kuonyesha uadilifu wake. Tena huyu kabila gani jamani mbona jina la ukoo afanania kama Mpare au mtu wa Tanga? Haya kazi kwenu piganeni vijembe na vikumbo humu ndani ya mtandao siye yetu macho, akiolewa wakwanza tutaja cheza ngoma, akiongezwa mwingine tutkwenda cheza ngoma pia maana si ndo kazi ya wapambe! Wenyewe wapiganaji wanajua mashemeji kama yu mmoja au wawili au watatu. Lakini wala huyo dada mchumba asikonde wala nini waswahili wasema kuku ukimchungua huwezi kumla!Kwani wanaume wote kwa ni POTENTIAL POLYGAMOUS! Hivyo hata hao waume zao waliotulia sasa hivi kwa wakati mmoja au mwingine walikuwa polygamists, wanaume wa kiafrika USIPIME!
ReplyDeleteHuu ni uungwana wa rais jakaya kikwete maana hata saed kubenea alienda tibiwa njee sasa kwa nini athumani asisaidie kama wanavyohoji wengine , utakumbuka kuwa kwanza ni mtumishi wa serikali pili ni moyo wa uungwana wa kiongozi tulienaye wa kuwajulia hali watu wa ngazi zote maana huyu athumani sio mpiga picha wake wala mwandishi wa ikulu lakini ni moyo wa wetu na uzalendo tulionao watanzania ndo unaotutofautisha na watu wengine haswa wakati wa shida ,tunamwombe mungu amuafu ili areje kwenye taaluma yake ya upashaji habari, mimi sio mwalimu wa historia lakini ikumbukwe hata Benjamin Mkapa naye alikuwa kama hawa waandishi mwanzoni mwa miaka ya 1970 sasa tusishangae siku ikaja ukasikia tuna Mheshimiwa Muhidin issa Michuzi -Mbunge wa Mbeya Mjini (CCM).
ReplyDeletejamani wabongo acheni umbea.nyie mliotangulia yanawahusu nini mpaka kumsema mchumba wake.tena mkome kwa umbea wenu.kama walikuwepo watajiju si wamechezewa nani aliwaambia wagawe.walidhani pipi.mwenye penzi la kweli kaja,hana tamaa wala nini kaja kwa pesa yake hamtegemei mwanaume.acheni hizo kutegemea kuchuna mabwana tafuteni kwa njia halali.tena hata kumwagiwa uji na chai hana huyo ni msomi hao wengine wamechujuka tu.kumbuka mwanaume hachuji wanawake tunachuja na kufubaa.sasa mnategemea kaka yetu ni mjinga anajua la aziz ni nani.acheni umbea kuweni na akili nyie wadau mliotangulia na style ya uji na chai.tena na wasiwasi walioandaika ni wanawake na wameshaonjwa na mdau wa ajali
ReplyDeleteuungwana au upendeleo? Inayotumika hapo ni hela ya wananchi. Wewe mueleze mfanyabiashara na mwalimu anayekatwa kodi katika mshahara wake kuwa hela yake inatumika katika kutoa huduma kwa watu rais atakaowaonea huruma kwenda kwa matimabu nje. Inaeleweka hapo jamani? Badala ya kumjengea barabara, shule bora, kuongeza mishahara ya walimu, nk. Hili jambo lifanyike kwa wote...sio kwa upendeleo. Ama sivyo wananchi waambiwe kabisa kuwa sehemu ya hela yenu inaenda katika kusaidia watu rais atakaowaonea huruma.
ReplyDeleteSina uhakika sana na swala la ajali kazini Tanzania. Lakini katika nchi nyingi kuna funds zilizoko ambazo zinatumika kukupa matibabu. Wanaziita Accident Compensation Scheme. Mtu yeyote anayeumia katika mazingira ya kazini (yani akiwa kazini) basi anakuwa entitled kupata hiyo compensation. Sasa akiamua kutumia kwenda kwa matibabu nje ni kivyake. Na hiyo hela inakatwa katika msharaha wako - kama insurance. Mimi nadhani hiyo ingesaidia zaidi katika situation kama hii kusudi huu usionekane kama upendeleo fulani.
Michuzi usinibanie...nawakilisha
mtoto