Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili katika mji mkuu wa Sudan wa Khartoum mchana wa leo (Jumapili, Septemba 7, 2008) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.Kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Khartoum, Rais Kikwete na ujumbe wake wamelakiwa na mwenyeji wake, Rais Omar Bashir na mkewe, Widad Babiker.
Rais ambaye ameambatana na mkewe, Mama Salma Kikwete amewasili Khartoum akitokea moja kwa moja Swaziland ambako alihudhuria sherehe za miaka 40 ya uhuru wa nchi hiyo na sherehe za miaka 40 pia ya kuzaliwa kwa Mfalme Mswati wa Tatu.
Viongozi hao wawili baadaye leo watakula futari na baada ya hapo wataingia moja kwa moja katika mazungumzo yatakayofanyika kwenye Ofisi ya Rais Bashir kwenye jengo la Friendship Hall.
Kesho Rais Kikwete amepangiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bunge la Sudan, Ahmed Ibrahim Eltahir na Makamu wa Rais, Ustaz. Ali Osman Mohammed Taha.
Kabla ya kuondoka nchini Sudan kurejea nyumbani, Rais Kikwete atakutana kwa mazungumzo mengine na Rais Bashir kabla ya viongozi hao wawili kuzungumza na waandishi wa habari.
Inatarajiwa kuwa viongozi hao wawili watazungumzia masuala yanayohusu uhusiano wa miaka mingi kati ya Tanzania na Sudan, na kuhusu masuala ya Afrika na kimataifa.
Mwaka huu, Tanzania na Sudan zilishirikiana katika kuchangia jeshi la AU, ambalo lilikwenda Comoro kumng’oa kiongozi mwasi, Kanali Mohammed Bakari kutoka Kisiwa cha Anjoun.
Kuhusu masuala ya Afrika , inatarajiwa kuwa Rais Bashir atamweleza mgeni wake na mwenyekiti wa AU kuhusu hali ilivyo katika eneo Darfur na jitihada zinazofanywa kupunguza mateso ya wananchi wa eneo hilo la Sudan.
Katika hilo, viongozi hao wanatarajiwa kuzungumzia mipango ya kuundwa kwa jeshi la pamoja la AU na kimataifa kwenda kulinda amani katika eneo hilo la Darfur.
Pia viongozi hao watajadili amri iliyotolewa mwaka huu ya kukamatwa kwa kiongozi huyo wa Sudan na kufikishwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uharifu (ICC) kutokana na mchango wa Serikali yake katika Darfur.
Pia Rais Kikwete anatarjiwa kupata maelezo ya undani kutoka kwa mwenyeji wake kuhusu maendeleo ya jitihada za kuleta amani ya kudumu katika eneo la Kusini mwa Sudan.


Michuzi, naona haupo likizo... Anyway ukipata picha za futari za Prez huko Sudan, tafadhali tuwekee hapa...
ReplyDeleteSwaumu njema
Tehe teh tee!
ReplyDeleteMichouzi bwana. Anajifanya kaenda Vakeshen Katum kwa gharama zake kumbe kadoea lifti ya Ndege ya Rais bwana!
Tehe teh tee!
HAHAHAAA NIMEFURAHI SANA KWA MHESHIMIWA RAIS KUTEMBELEA SUDAN KWA KWELI KUNA MENGI SANA YA KUJIFUNZA PALE SUDAN NA NI JINSI UTAWEZA KUTAMBUA TANZANIA TUNA BAHATI NZURI SANA TUMEJALIWA NA MUNGU.
ReplyDeleteMHESHIMIWA RAIS USISAHAU KUMUOMBA BASHIRI AKUPELEKE KITONGOJI KIMOJA KINAITWA OMNDURMAN HAPO KHARTOUM,KUNA FUNDI MMOJA ANATENGENEZA SANDLES NZURI SANA ZA NGOZI NA MIKOBA MIZURI SANA NAJUA UTAIPENDA KWANI NI PURE LEATHER.
UKIPATA MUDA PIA HAPO HAPO KHARTOUM UKAONE BLUE AND WHITE MAHALI MAHALI ILIPOKUTANA
BALTAZAR
KIPEPEO TOURS
SIJUI MKITOKA SUDANI MTAELEKEA WAPI? NASIKIA CHINA KUNA MICHEZO MINGINE NI VIZURI MKAENDA HUKO KUANGALIA KWANI NYIE NI WAPENDA MICHEZO.
ReplyDelete