njia kuu ielekeayo el mourada nje ya jiji la khartoum
katikati ya jiji la khartoum
mojawapo ya alama za jiji la khartoum ni hilo jengo ambalo ni hoteli inayomilikiwa na libya
barabara zaa khartoum ni pana na safi na zina alama zote muhimu
hapa ni katika ukingo wa mto nile ambapo inakutana white nile na blue nile. angalia maji ya upande wa kuume ambayo ni mekundu (blue nile, maji yake yakitirika tokea ethiopia) na upande wa kulia ni meupe (white nile ambayo maji yake yanatiririka toka lake victoria upande wa kaskazini) katika sehemu inayoitwa al-mogran

The fulana's
ReplyDeleteWe kwenda zako acha kutu kambaisha sisi, vekesheni wapi ,uko na JK huko , muone kwanza na kifulana chako !
ReplyDeleteAs salaam aleikum Sheikh Michu!
ReplyDeleteHongera kwa kuwa huko mwezi huu mtukufu wa Ramadhan - Tatizo hapa ni FULANAZZZZZZ!
Kwikwikwikwikwi!!!!
Kweli hii blog yako, ukienda vichakani kunya unatuambia, ukiwa bila shaka! haya uwenatuambia na unapotoa huduma nyinginezo.....!
ReplyDeletehi Bro michuzi hiyo fulana ndio uniform yako? maana naona picha nyingi ni kifulana kitaimba alleluya
ReplyDeleteKaka Fulanaz inatalii kushinda mimi ziara njema mchunge JK asije akaacha kufunga
ReplyDeletekakaaaaa wewe kila siku vekesheni?
ReplyDeleteRamadhan Kareem Sheikh Michuzi!!!
ReplyDeleteWadau msikalie kupiga kelele fulana fulana, si mumuulize mkuu wa wilaya ya tegeta ina siri gani hiyo fulana...!!!!
Mdau
mmnh hiyo fulana si bure, tushakuweka alama kwa hiyo fulana, ingekuwa na mdomo ingesema jamani nimechokaaa lol!!
ReplyDeleteSasa wewe Michuzi kila trip ni vekesheni!? au huijui maana ya vekesheni?
ReplyDeleteSwali Ni Kwamba!..Hiyo FULANAZ Unaitunza Vipi?..Manake Haichuji..lol...Ur The Greatest Michuzi!..Pamoja!
ReplyDeleteMshukuru Sana JK Usingepanda Ndege
ReplyDeleteMichuzi, tunacheza nao hao hivi karibuni usisahau kuchukua mchanga ndani ya 18 na katikati ya uwanja niletee niufanyie kazi. Nitafute ukirudi.
ReplyDeleteKuna mdau hapo juu ana hasira kweli unaposema uko vacation ....Big bro take it easy ....watu wengine sijui njaa au vipi....
ReplyDeleteKwani akisema vacatio nyie inawauma nini...?????????????? kazi yake naimind sana tu ninavyopenda kutembea hata mimi ningeringa kama ningekua na kzi inanitembeza allover the world like him
Cha kusikitisha ktk watu ambao wanashangaza kwa vitimbwi kama watanzania na vilevile wepesi kulaghaiwa ,sasa huyu kaka wa watu yuko kazi au vekesheni tatizo ni nini , hatuwezi kuandika mambo ya maana mpaka tumtusi mtu yeye anajaribu kutuonesha kile ambacho watu wengi tulikuwa hatukioni kama picha na habari za nyumbani, jamani imefika wakati tutambue michango na kazi za watu sio tusubiri mpaka afe ndo tuseme ukweli wetu wa maoni huyu kwa mtazamo wangu ni mtu maarufu sana kiasi cha kuwa tishio pale atakapoamua kuingia kwenye siasa za tanzania
ReplyDeleteKAKA MICHUZI FULANA NI YAKO BWANA HIYO INAONYESHA NI JINSI GANI ULIVYO MWANA UCHUMI NA MAENDELEO NDIO YANAKUJA KWA KUWA HIVYO ILI MRADI TU HAINUKI KIKWAPA, SASA HAPO SUDAN UKIPATA MUDA NENDA HAPO KWENYE SUPERMARKET KUBWA KULIKO ZOTE SUDAN NI KARIBU NA AIRPORT INAITWA AFRAA UKALE ICE CREAM ZA KILA AINA UKITOKA HAPO BASI UENDE KUNA SOKO MOJA KUBWA SANA UKAJIONE MWENYEWE KARIAKOO YA HAPO PIA USIHAU KUPANDA BAJAJ ZIPO NYINGI SANA HAPO ZINAITWA TUKTUK,USISAHAU HAIRUSIWI KUNYWA LAGA WALA KUVAA KAPTULA JAPO JOTO LA CHINI NI NYUZI JOTO 40.
ReplyDeleteKAMA WEWE NI MTU WA GYM AU SWIMMING BASI NENDA CLUB MOJA INAITWA GERMAN CLUB LAKINI SIKU YA ALHAMISI NI SIKU YA KINA MAMA PEKE YAO KINA BABA NOOOOOP,
USISAHAU KABISA KUPIGA PICHA CHAKULA KIKUU CHA WASUDAN KINAITWA FUUUUUUL
BALTAZAR
KIPEPEO TOURS
Michuzi achana na waosha vinywa. Kula vekesheni yako kiulaini.
ReplyDeleteKazi nzuri mkuu wa nanihii. Asante kwa kutupa vidokezo vya Khartoum. Sijui wabongo elimu yetu inatusaidia nini. Hata mtoto wa darasa la saba atatambua kuwa Michuzi anatumia lugha ya picha, istilahi, utani, nk. ikiwa ni katika jitihada za kufanya anayotupeperushia yasitu-bore, km mkuu wa nanihii, vekesheni, nk sio lazima kuyachukulia katika maana zake za msingi. Nyie watu mmepata elimu kiasi gani? Ngumbalu?
ReplyDeleteSwali kwa mkuu wa nanihii: 1)utamaduni umenipita kando, mkono wa kuume ni upi? na unahusianaje na mkono wa kulia?
2) Je vakesheni itakufikisha hadi Darfur ili uweze kutumegea ya huko?
Twende mbele turudi nyuma ingawaje hawa jamaa ni maskini kuliko sisi lakini infrastructure zao zinapendezesha macho.Angalia hizo barabara zilivyopana na safi kama vile mamtoni.Kwa muonekano huu hapa inaonyesha wapanga mji wa sudan walikwenda hadi form 4 wa kwetu waliishia form 2.Barabara za home zimefinyana kama nyanya ktk tenga.Sidhani hawa jamaa wana shida ya kupanua barabara kila muda.
ReplyDeleteI've never been there.Im judging from the appearence of the photos
NAKUUNGA MKONO MTOA MAONI WA SEPT 07,2008 10:35 SAWA KABISA ULICHOKIANDIKA. KAZI IPO YA KUILIMISHA WATU HATA YASIO YA MUHIMU ITABIDI KUELIMWISHWA TUKITEGEMEA NI RAHISI KUELEWA LAKINI BADO AU SIJUI NI ROHO MBAYA.... NAMFAGILIA SAAANA BWANA MICHUZI .
ReplyDeleteasalam aleykum kaka michu, naomba unisaidie hilo hotel hapo khartoum mbona liko na shepu ya bomu? na hivyo basi linamaana gani kwa sudan na Libya? naomba majibu kaka.
ReplyDeletemdau
ETM
mdau Mbigiri, kwa mujibu wa takwimu za shirikala fedha duniani, IMF, pato la ndani la taifa kwa kaya (per capita GDP) la Sudan kwa mwaka 2007 ni dola za kimataifa 2,171.874 (nafasi ya 123 duniani), wakati Tanzania ni 1,255.956 (nafasi ya 156 duniani). Wakati takwimu za Benki ya Dunia inaonyesha kuwa pato la Tanzania ni takribani dola za kimataifa 1208.622 (nafasi 123) na Sudan ni 2087.768 (nafasi 145). Hivyo hawajatuzidi umasikini (kama ukichukulia wastani kwa kaya). Sema tu kwa wenzetu hawa naona kutakuwa kuna "magepu" makubwa kwa ajili ya vita, ukame, n.k. Uwiano wa maisha kati ya tabaka la juu na ndugu zetu wa Darfur ni tofauti sana.
ReplyDeleteNakubaliana nawe kuwa kwa picha chache hizi za Khartoum, inaonekana kimiundombinu jamaa wametuacha mbali. Hii ni pamoja na matatizo yote yaliyowakumba. Fikiria bila ya hivyo wangekuwa wapi. Naona wanayumia vyema mafuta na pamba... sis dhahabu yetu vipi jamani?
Hawa viongozi wa kibongo, hawana mpango wowote. Ukimsifia mtu tuu unapewa post. Michuzi mara nyingi unasafiri kutokana na taaluma yako ya uandishi, pia ni mwajiriwa wa Daily News. Unapata muda gani wa kuangalia matatizo wilayani kwako? Kweli kwenye fungu huenda nyongeza, kodi za ndugu zetu zinaliwa bure bure tuu, hata kama mtu hafanyi kazi, ili mradi umsifie kiongozi fulani na usiandike maovu ya serikali. Kaka Michuzi uache unafiki, hata kama hukuweka comment hii. Sio Sudan, UK, tuwekee na picha za Manzese uwanja wa fisi na vijijini huko bongo, tuone hayo anayosema huyo rais "maisha bora kwa kila Mtz". Judgement day is coming.
ReplyDeleteukimaliza hiyo vekesheni mstue mista president akatembelee kule Darfur tuone napo kukoje!
ReplyDeleteAnonym. wa 5.22AM, nakuunga mkono kwa 101% ulonena. Wanamipango miji wa kwetu kutwa nzima wanawaza ufisadi, sio wabunifu hatakidogo. Naona ukilinganisha wanamipango miji wa huko (Khatum) na wa kwetu ambao wamekulia na kusomeshwa ndani ya nchi ya amani,hata hiyo F 2. umewapendelea. Ni wababaishaji kinoma, wao kuwaza kuuza viwanja mara mbili mbili, hapo aaakh, wanazodegeree haswa!!
ReplyDeleteMimi naona serikali inahaja ya kulibebea bango suala la wana mipango miji wetu, yaani bado mawazo yao yapo miongo saba ilopita.
Ah, inakera ndugu zanguni.
MICHUZI, MKONO WA KUUME NDIYO MKONO WA KULIA....AU MWENZETU MIKONO YAKO YOTE YA KULIA? KIINGEREZA NINGEKUELEWA, HATA KISWAHILI PIA? MH..
ReplyDeletemkono wa kulia ni wapi?ki-kwako uvosimama ktk picha au sie watazamaji tuonavo??
ReplyDeleteafu mkono wa kulia na kuume...sijaelewa apa..nijuavo ni sehemu moja
ebu mnieleweshe
Mbona huko city center magorofa yanahesabika???? yaani hata mwanza inaifunika khartoum LOL
ReplyDelete...ila kwenye usafi nawapa big up hao janjaweed
Kakaz...........Fulana Isi the mosti travelled fulanaz in the Worldi............Cozi of thati i wanti to buyi iti fromi you kama memorabilia..........Naomba offeri yako?????????????????????
ReplyDeleteramadhan Karim.........
Wow asante kwa kutuelimisha. mimi nikisikia sudani nakumbukia tu zile picha za njaa na vita tu .Kumbe kuzuri hivyo na kusafi hivyo.Hata kama wanasehemu zilizomasikini kama kwetu lakini jiji lao lisafi bwana.
ReplyDeleteAchana na waosha vichwa hapo juu...fulana yako...vacation yako...watu wanaona donge hawawezi kutalii kama wewe at kama sio JK asingepanda ndege...so what.....Wivu umewajaa sana tu ....
Unaesema city centre maghorofa hakuna hujui ulisemalo wenzako wana mipango miji.weye unataka paonekane kama huko kwenu hata parking ni issue??kama kariakoo??tembea ujionee sio kukaa hapo bongo ndo ukafikiri miji yote iko hivyo,hovyoooooooooooooo.
ReplyDeletecha chandu - uk
HII NDO FAIDA YA KUWA MWANACHAMA WA OIC KIKWETE AKISAFIRI LAZIMA ASAFIRI NA MICHUZI MWISILAMU MWENZIE,WANAFUNZI WALIOKUTANA NAO SUDAN WOTE NANIHII NAFIKIRI WALIKWENDA KUFUTURU NA JK.
ReplyDeleteINASIKITISHA MH.MKUU WA WILAYA YA NANI HII NDUGUYO HANA SERA.UKIPENDA POST HII AU ACHA.
HIVI MICHUZI HUNA FULANA NYINGINE ?? MBONA KILA SIKU HIYOHIYO ??
ReplyDelete