Mh. Balozi
Nimeona darasa ulilotoa kwenye post ya jua.
Nimeona darasa ulilotoa kwenye post ya jua.
Naomba somo zaidi katika kuchukua taswira kama hizi.
Mdau O.P.
-----------------------------------------------Mdau O.P.
Kwanza asante kwa kuendeleza libeneke. Pili hongera sana kwa picha mwanana. Kwa kweli umejitahidi sana sana, hasa ukizingatia kwamba hiyo Olympus FE-170 point-and-shoot uliyotuia haikupi uchaguzi (choice) mkubwa wa mambo mengi kama vile kuvuta (zoom) ama kuweka chujio (filter) kwenye lenzi yako.
Vile vile hapo shimoni Ngorongoro huna uchaguzi wa muda wa kwenda, hivyo umelumangia hivyo hivyo na kijua cha mchana (nadhani ilikuwa kati ya saa 7 na 9 ) hivyo ikabidi utumie mwanga uliopo ambao kwa ukali wake picha kutoka vyema si muda mzuri. Muda mzuri wa kupata picha nzuri ni masaa mawili kabla ya machweo ama baada ya jua kupanda. Ama ukiwa na bahati kuwe na mawingu mazito kiasi, na hakuna mwanga mkali kama huo ambao unapunguza sana utamu wa rangi.
tukija kwenye taswira 1. hapo sina neno kwani ujumbe umeukamata inavyotakikana, na huyo dada anayeinama na kamera kaongeza nakshi, kadhalika na huyo aliyekaa kiti cha mbele na kufunga kioo inajieleza yenyewe hali halisi ilivyokuwa. Na wewe ungesogea kushoto zaidi ingekuwa mswano, ila najua gari hairuhisiwi kukanyaga nyasi nje ya barabara. labda kwa kuibia kama jamaa yule wa kule. hivyo umesamehewa kwa engo hiyo.
taswira 2. inajieleza yenyewe kwamba umemuonea huyo twiga wa kushoto. kwa nini umemkata kichwa wakati ungebalansi na kula nafasi ulioacha wazi kulia ingekuwa bomba sana. milima inaonekana vyema ila ukungu (hue) wa buluu umeondoa chachandu ya rangi. hapo ungekuwa na kamera yenye kubeba chujio (filter) hasa ile ya skylight ukungu ungepungua kama si kutoweka kabisa.
taswira 3. Naam! hiki kitu kimetulia. ujumbe umefika, na uhai upo (jamaa aliyesimama kuleeee) maana wadau wengi wanasahau kuweka uhai kwenye picha za namna hii. wengi wangeishia kupiga magari tu, ambapo picha ingekufa kwa kukosa kiumbe hai. Yaani kama unapiga picha milima ama uwanja ama sehemu yoyote ya wazi kama hii usisahau kuweka kiumbe hai, hata kiwe kiduchu kama kuku. pia kwenye hii picha hivyo vijiwe vimatengeneza fremu njema kwa mtazamaji, kwani vijiwe vinafanya jicho lako likimbilie kwenye ujumbe ambao ni magari. tatizo katika snepu hili ni muda uliopigia. jua ni kali sana na rangi haijakolea inavyotakiwa. lakini kama zilivyo zingine, hukuwa na uchaguzi. msafara kama huo unakuwa noma pale unapotaka kupata picha tamu. lakini hongera na asante tena kwa kuendeleza libeneke hili. natumai wadau 'walevi' wa taswira wataendelea kutuletea burudani zaidi.
-michuzi
Picha nzuri,mabruuk
ReplyDeleteNakubaliana na Michuzi kama alivyoeleza, nami noamba kuongezea kidogo.Picha ya kwanza the camera was pointing downwards, that automatically distorts what is called linear perspective and loss of three dimentional representation, suggestion, you should have taken the picture from ground level, and while you were at it you should have told the gentleman leaning on the rear wheel to lift his head up and possibly stand with arms akimbo
Samahani
The pictures are nice
Wakatabahu
Ama kweli starehe ya mtu ndo shetani wake. Yaani hapa wakati mie nanufaika na karibu kila maelezo yanayotoka kwako, kuna jamaa yangu wala haelewi kwanini mtu "upoteze muda wako kuchunguza picha inayoonesha kila kitu". Anadhani sisi tunataka kuwa sahihi katika kila taswira tutoayo.
ReplyDeleteAnyway, Shukrani kwa mara ya tena Kaka na naamini wengi wataleta taswira zao nasi tule darasa kimachabo.
Blessings
chonde chonde. picha mbona mswano tu. sasa wajameni siku hizi si kuna huto tudijito kamerazz unapiga picha milioni moja unatupa zote na kuweka hiyo moja iliyokubali. tusionazo tukalagebaho.
ReplyDeleteUSISAHAU KUWEKA KIUMBE HAI! MBONA KWENYE PICHA INAYOONESHA MAGARI YUPO BINAADAMU AMESIMAMA NADHANI NI DEREVA SASA HUYU KWANINI TUSIMUONE KUWA NAYE NI KIUMBE HAI LICHA YA KUWA NI DEREVA?
ReplyDeletewadau naomba msaada,mimi nimeshazama crater mara mingi sana ila mika kadha sasa sijapiga hizo dili,hizi Bama(Magari)yako wapi exactly hapo shimoni yako kule chini picnic site ama?
ReplyDeleteoi acha kujaza blog napicha zako zaa ajabu...baada yaku post picha za kilimanjaro,serengeti ur busy advertising other countries wat was that all about?ama ujui kama this is apublic blog?na hata picha moja huja tokea,be apatroit post TANZANIA NATURE,bwana michuzi toa upuuzi wahuyu jamaa.excuse my language i just hate seeng none patroits
ReplyDeletewee annon 8.34am ivi hujasoma ujumbe kwa makini??eshasema kiumbe yupo/uhai upo apo,,,aalaa soma b4 ujjibu utumbo apa
ReplyDeleteAgain kwa mdau wa September 29, 2008 12:27 PM. Sijajua unaulizia magari yapi. kama ni picha ya tatu hapo ni serengeti seronera airstrip. tehe tehe
ReplyDeleteHata mie nimenufaika na hilo somo yaani nina mapicha kibao mengine nimewakata watu masikio, mengine wanyama nimewakata vichwa, wengine mabata wanaonekana nusu. Yaani Michuzi shukrani kwa kweli sasa nitaanza kuwa makini ninapopiga picha, maana nikiangalia picha nilizopiga nakujiuliza hayo maswali uliyoweka hapo juu nakuzifanyia postmortem naona ni kichekesho. Shukrani kwa somo na wala usichole maana tumenufaika na ninaamini tutaendelea kunufaika.
ReplyDeletePROUD TANZANIAN, kama unadhani wewe ni mtanzania halisi kwanza ungeanza na jina lako. Ushatukuza u-magharibi kwa kutumia jina la lugha yao. Pili unaonekana kuwa "wana-be Proud Tanzania" maana hata hujui hizi picha ni za Tanzania na hiyo yaonesha kuwa hujui upondacho. Unaanza kumwambia mtu atangaze Kilimanjaro ama Serengeti wakati picha zenyewe ni za Serengeti. Yaonesha kwako utalii ni Kilimanjaro pekee. Huo ni ufinyu wa uelewa. Tatu angalia hata namna unavyoandika lugha yako ndugu yangu. Unaweka "baada" kwenye "badala" na pia unatumia maneno 31 ya kiingereza na 27 ya kiswahili na kujiita Proud Tanzanian? HizHayo ndio twaita majungu.
ReplyDeleteKaka Michuzi nashukuru kwa kuweka maoni ya huyu jamaa maana naamini ni wakati muafaka wa kuongeza elimu ya kutoa tongotongo kwenye hizi akili zilizoandamwa na utumwa wa kiakili.
Ni funzo tu kwako na hutakiwi kujibu Proud Tanzanian
Manuliza wapi? Eti kwa watu? Hamuamini kama hapo ni Bongo, TZ kwenye mavumbi eeh? Hapo ni Tanzania mwanawane na wala si mapicha ya ajabu ajabu. Shauri ya kukaa kwa watu sana hata mambo mengine ya kwenu hamuyajui! Bongo tambarare!!
ReplyDeleteMkuu wa wilaya ya nanihi/balozi wa Zain hapo unaniacha hoi na huo uchambuzi wa picha...nafikiri ufungue shule/darasa mtandaoni ili tuweze pata hii elimu ya taswira maana nimenogewa na hiyo shule unayotoa...
ReplyDeleteNgorongoro shimoni hakuna twiga mkuu umejikanganya
ReplyDeleteMichuzi somo bab kubwa asante sana, nitatafuta ze camera wis ze chujio next time.
ReplyDeleteAsante jamaa aliyenisaidia kumtoa tongotongo mtu. And the bodies of those magari are made in tanzania.
And to bongo boy, no one said twigas r @ ngoro shimoni. that malanja area and the mlima on the back ground is lemakarut