Nikiwa mwanablogu wa Kitanzania niliyepata inspiration ya kuanzisha blogu kutokana na kazi yako nzuri,napenda kukupongeza kwa kuteuliwa kwako kuwa Balozi wa ZAIN.
Blogu kama yako zimekuwa vyombo muhimu zaidi vya mawasiliano ya kielektroniki kuliko hata vile vya asili (radio na runinga) na vya chapa (print media-magazeti) hasa kutokana na ukweli kwamba in most cases blogu zinakuwa updated mara nyingi katika siku na hivyo kuwasilisha habari mpya mapema zaidi.
Kadhalika,blogu ziko “kirafiki” zaidi kwa maana ya ushirikishwaji wa hadhira katika utoaji michango ya mawazo na contents.
Kuteuliwa kwako kuwa Balozi wa ZAIN ni ishara ya kutambuliwa kwa mchango wa blogu kwa jamii yetu,na unastahili pongezi zaidi kwa kutuonyesha njia .
Pengine baada ya mafanikio hayo makubwa vyombo vyetu vya habari vitaangalia uwezekano wa “kuiga” trend ya vyombo vya habari vya kimataifa vinavyotoa fursa kwa blogu kwenye tovuti zao.
Hongera sana na Idd Mubarak (in advance)
Evarist Chahali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...