hi Kamanda,
Mdau katika pita pita zangu nilipita njia ya kwenda Manyara katika kijiji cha Namilolo, in the middle of no where nikakuta hiki ki ghorofa kimejengwa katika mlima. Nikaambiwa kuwa ni cha ma sister. Nilishindwa kujizuia kukipiga picha. Siyo mtaalamu wa kupiga picha ila nataka tu watanzania wengine waone hii kitu.
cheers.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hayo ndiyo yale tuliokuwa tunadanganywa kama wamekuja kutoa msaada mbona wamejitenga na jamii na kujenga li-mansion kwenye prime location.. hata huko ulaya wasingeweza kutanua kiasi hicho...ukichunguza sana utakuta kuna kibiashara ka madini kanaendela taratibu ndio ufisadi huo..

    ReplyDelete
  2. Waswahili bwana!!umeshaambiwa ni kigorofa cha masister,kwani masister hawatakiwi kukaa sehemu nzuri??au masista hawawezi kupata misaada kujengewa nyumba kama hizo?mbona misheni nyingi Tanzania ni bomba sanaa,mie sioni hajabu katika hilo..hili sio libeneke la taswira tafuta nyingine picha..mdau Norway

    ReplyDelete
  3. Kweli Mdau amejitahidi kupiga Picha japo Focus sio Clear nampa hongera kwa hilo ila wakati mwingine awe mualifu katika Majina au Jina la eneo husika na kama ni mgeni ni bora aulize kwa mwenyeji kwani kwa walio wageni wanaweza wasijue lolote ila kwa sisi tulio wenyeji wa Mkoa wa Manyara hasa Wilaya ya Simanjiro tunaona kwamba amekosea,Kwanza nyumba hiyo ni ya mtu binafsi ambaye ni Mzungu na sio ya Masista na Mwenye nyumba amekuwa Mdau Mkubwa wa Maendeleo katika jamii hasa katika Mradi wa Maji na Afya na Jina la Eneo ni NEMALULU na sio NAMILOLO,la nyongeza ni kwamba inasadikiwa kuwa huyo Mzungu amejenga kaburi lake tayari ndani ya hiyo nyumba yake.

    Mimi,
    Ole Maika Baraka.
    Simanjiro-Manyara.

    ReplyDelete
  4. ofkoz masister wanakaa sehemu bomba ata kuwe porini,,,nao ni watu,,ila pia annon wa 1,,mmhh yawezekana sana tu

    ReplyDelete
  5. Mdau uliyetoa picha nashindwa kukubaliana na wewe......mimi ni juzi juzi tuu nimepita hiyo njia ya simanjiro (vumbi jepesi kama unga wa ngano)....nikabahatika kuiona hiyo castle....wenyeji walituambia ni NYUMBA YA MZUNGU TENA KAJENGA KABISA NA KABURI LAKE HAPO HAPO.....tulibaki midomo wazi wote........kha!

    ReplyDelete
  6. hata mimi niliambiwa ni ya mzungu sijui alikwenda kusaidia nini huko africa na wala hakutaka tena kwenda kwao....sasa alivyosema ni ya masister nikajua ni nyingine lakini kuizoom ni ile ile

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...