Pssst! KUNRADHI; ILA NAOMBA WADAU 'WALEVI' WA TASWIRA WAWE WANALETAGA TASWIRA KATI YA MOJA NA TATU TU ILI NGOMA IWE INANOGA. ZIKIWA NYINGI INAKUWA TAMU KUPINDUKIA KIASI HATA RADHA INAPUNGUA. AU MNASEMAJE WADAUZZZZZ???
Michuzi usharudi kutoka vikisheni....?
Chukua picha hizo..za vikisheni yangu niliyo kuwa Kigali....utaona kuna kigali city.Na zingine ni taswira na mie niingie kwenye libeneke...hilo la taswila.
Buswelu.
--------------------------------------
mdau biswelu asante kwa taswira nzuri. mie nsharudi kaka!
kwa kuanzia taswira 1 na taswira 2 zinafanana. ushauri ni kwamba jua sio lazima lionekane kupata picha nzuri ya machweo. huo mpira wa njano unaweza ukaacha uzame wote na mwanga wake utaosalia ungeweza kufanya mambo yawe mswano. kuwepo kwa huo mpira kumevuruga muonekano ikizingatiwa vichaka na paa la nyumba pekee vingetosha kupendezesha.
taswira 3. ungekuwa na kamera ya kuvuta (zoom) ingeleta maana zaidi ya nini unataka kutuonesha. hapo unatichanganya, tuone paa la nyumba ama ndege, maana kama huko kujikuna haonekani vizuri kwa umbali uliopo. inaonekana kama ndege asiye na kichwa juu ya paa. ila picha nzuri, mwanga mwanana wa jioni umekwivisha rangi inavyotakiwa. huo ndio muda hasa wa kupiga picha za nje.
taswira 4. umechemsha. hakuna uhai ama kiumbe hai. hilo guzo la njano kifuani pako la nini. ulikuwa unaogopa kuchungulia nini? hahahaa. hapo ungeweka mtu anayeangaia maji chini, sio lazima aonekane wote. vinginevyo picha haieleweki unataka kusema nini
taswira 5. acha papara. sio kila ukiona kitu unajifotolea tu bila kuangalia nini unataka kusema na picha yako. ona sasa upande wa kuumeni umekata jengo. ulikuwa unaibia nini. adobe ya jina imependezesha picha kuliko ulivyodhamiria, kuweka jina tu. jina lisingekuwepo uwazi wa anga ungechukiza, hasa ukizingatia hakuna kiumbe hai. siku ingine ngoja kandege kapite ili kuua uwazi usio na umuhimu kama ulivyoweza kuua kwa jina
taswira 5. sasa hiyo nguzo mbona umeikata denge? we huoni kwamba ingepndezesha mambo kwa kutoigusa kwa juu? kwa chini haina neno. picha nzuri sana japo ulipiga wakati hakuna mwanga mzuri wa jua na uhai upo kibao.
taswira 6. dah! naona neshno la amahoro hapo. bonge la picha hili. ila kibao cheupe chini shoto kimeharibu. ungekikwepa kwa kubetua kamera juu kidooooogo kisionekane, maana hapo kinaharibu pozi. jicho linaanza kukimbilia hapo kwabla ya kwenda amahoro. milingoti ya taa za amahoro zimekula kwa uzuri sana uwazi wa anga. isingekuwepo picha ingedoda. hongera.
taswira 7 na taswira 8. mmmhhh. hapa ulitaka kuonesha nini? magari? boda? maua na miti. picha zako zina makelele hadi masikio yanauma. yaani hukuwa makini kuonesha stori yako. ili picha ieleweke stori unayotaka kutoa ipewe kipaumbele (prominent) kuliko mazingira ambayo yanakuwa visindikiza tu. pia naomba uwe makini na sehemu nyeti kama hizi. wengi hawaruhusu kupiga picha kabisa ama bila idhini. sehemu nyeti zote kama vile kambi za jeshi, uwanja wa ndege, vituo vya polisi, ikulu na kadhalika huwa hawaruhusu. sijui kwa huo rwanda sehemu hiyo ya boda.
taswira 10. hii ndio picha bora katika hizi. ni nzuri. imetulia. inaeleza kila kitu. nimependa ulivyoweza kukamata viumbe hai vyote vikiwa vinaelekea kumoja. pia uliposimama pameleta maana ya kila kitu. hongera kwa hii.
-michuzi
Anko michuzi hii dili ya twasira nimeipenda sana.... lakini katika mitazamo yako yote nimeona unaongelea tu editorial picture ambazo zinakitu hai ndani yake..... kwamtazamo wangu sio picha zato lazima kuwe na kiumbe hai..... kwamfano hiyo twasira ya maporomoko ya maji..... mpiga picha angekuwa chini akawa anapiga maji kwa kuangalia kwa juu au yangekuwa yanaporomoka vizuri kwakweli ingekuwa bomba sana....
ReplyDeletePicha za nature peke yake ndo zinazopendwa sana na wapiga picha wa fani..... lakini kweli kama ingekuwa picha ya kuweka gazeti basi mtu angechungulia kidogo....
Thank you for the taswiras. Very informative indeed. I laways thought Bugando Hill Hospital was in Mwanza (Tanzania). Now I know it is in Kigali. Please confirm whether this is the Kigali in Rwanda or just a place in Mwanza.
ReplyDeleteOh, i wish ningelikuwa na kamera, ningelivunja rekodi ya kutuma picha kwa (taswira)!
ReplyDeleteHata hivyo hii imekaa vizuri, na nafikiri baadaye itafuata video, ili watu wafaidi zaidi
M3
Asante sana mdau uliyekuwa Kigali,Balozi Michuzi mimi nadhani Wadau wakutumie nyingi tu ila wewe uchukue 3 ambazo unaziona ni nzuri zaidi.Lakini kama ulivyosema,wewe unazweza kuziona nzuri mwingine akaziona mbaya.Kwa ujumla mimi binafsi napenda tu kuona maeneo kadhaa tofauti tofauti.
ReplyDelete