




Kituo hicho ambacho kilianzishwa January mwaka 2006 chini ya Mkuruigenzi wake mkuu Ruge Mutahaba, kinalea na kuibua vipaji katika maigizo, madansa wa muziki na ngoma za kisasa na kiasili pamoja na waimbaji.
Baadhi ya vipaji, kwa upande wa muziki, ambavyo vimeibuliwa kutoka katika kituo hicho ni wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya, Mwasiti Almasi na Hafsa Kazinja. Mwasiti alitamba na wimbo wake uitwao Niambie wakati Hafsa aliwagusa wengi na wimbo wake wa Pressure. aliomshirikisha Banana Zorro. Dada yake Banana, Maunda Zorro, pia ni mmoja wa vijana wanaolelewa kituoni hapo.
Msanii Shaggy alipotua bongo kwa maonesho kadhaa hakuamini macho yake pale alipokuta kambi hiyo yaa vijana wapatao 100 wakijifua katika kuimba, kucheza na kupiga ala. Alimwambia Ruge kwamba kabla ya miaka 5 Shaggy watano wataibuka toka THT.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...