Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani Dr Ally Y. Simba, Jana(27/9/2008) alikutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wa Italy Bw. Abdulrahaman A. Alli katika hotel ya Universo ya Mjini Roma, Italy.
Katika mkutano huo Mwenyekiti huyo wa Italy alifuatana na Katibu Mkuu wake Bw. Kagguta N. M. Pamoja na mambo mengine, viongozi hao walijadiri kwa kirefu mifumo ya Jumuiya za Watanzania ughaibuni pamoja na matatizo wanayokabiliana nayo katika kufanikisha malengo ya Jumuiya hizo.
Kama ishara ya kuziweka Jumuiya hizi karibu zaidi, Dr Simba alimkabidhi Bw. Abdulrahaman katiba ya Jumuiya ya watanzania wa Japan.
Viongozi hao walikubaliana kundelea kuwasilina na kubadirishana habari za Jumuiya zao.
Mwisho kwa niaba ya vinogizi na wanajumiya wa Japani, Dr Simba alitoa shukurani zake za dhati kwa Viongozi hao wa Italy kwa kukubali kukutana naye. Dr Simba aliondoka Jana Jioni kuelekea Palermo kikazi
Jamani huyo ni mwenyekiti wa Watanzania Napoli..Mbona sisi watu Wa Roma hatumjui??Anaitwa mwenyekiti wa Watanzania Italia kwa kuchaguliwa na watu gani na waishio wapi??? Jamani naomba tuandike vitu vya ukweli..
ReplyDeletedada wamekosea kuandika...huyo ni mwenyekiti wa pili wa watanzania wa Napoli, wa kwanza alikuwa Prof. Tandika.
ReplyDeletedada wamekosea kuandika...huyo ni mwenyekiti wa pili wa watanzania wa Napoli, wa kwanza alikuwa Prof. Tandika.
ReplyDelete