

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mheshimiwa Michuzi Pole na kazi.
ReplyDeleteKwa kweli hiyo habari ya Babu wa mizimu imenikumbusha mbali sana.Nakumbuka wakati nasoma enzi hizo reli ya TAZARA ndiyo kwanza imefunguliwa tulikuwa tunapata huduma babu kubwa kwenye treni hiyo.Moja ya huduma ilikuwa tunawekewa miziki ile ya kizaire kama mikolo milekimingi,kamiki,kasongoyeye,andoya n.k.Kulikuwa na mtangazaji ambaye alikuwa anatangaza kila treni ilipokuwa inakaribia kufika stesheni fulani.Pia alikuwa akitutangazia tunapokaribia sehemu mbalimbali za kuvutia kama vile mbuga za wanyama, mahandaki n.k. Kwahiyo Treni ilipokuwa inakaribia Kisaki mtangazaji huyo (mara nyingi alikuwa mwanamke) alikuwa akitutangazia kuwa tunakaribia stesheni ya Kisaki,ambapo kabla ya kufika Kisaki mtaona upande wenu wa kuume/kushoto kuna kisima cha maajabu kinachotoa maji moto.Mtangazaji huyo alikuwa akitoa full story kuhusu Kisima hicho.Kwa kweli ilikuwa inafurahisha sana.Lakini siku hizi mambo hayo hakuna tena.TAZARA imeoza kabisa.Mheshimiwa enzi hizo TAZARA ilikuwa kweli reli ya uhuru. Kwahiyo Mheshimiwa Michuzi nafikiri itakuwa jambo la busara na faida kwa wengine kama ukaifuatilia habari hiyo kwa undani na kisha ukaturushia kwenye mtandao huu ili wadau wengine wa blog hii waweze kuipata story hiyo kwa undani ili Wajue maajabu ya Mkoa wa Morogoro.Hata kama utairusha kwenye daily news, yote sawa ili mradi utupatie link tuweze kuisoma
Ni mimi Mdau wako wa Cardiff
Saidi kalembo as know Safi Sana Kalembo tulikuwa naye pale High Commander Training Wings na alishastaafu miaka 5 iliyopita na sasa mkuu wa mkoa.DUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU Bongo hakuna watu wenye nguvu za kufanya kazi mpaka tuchukue wastaafu.
ReplyDeleteOkay labda anabusara na kiongozi Mzuri nani anajua?
Kenge
Kuna teknolojia za kuzalisha umeme kwa kutumia maji moto. Tunatengeneza hela ya kutosha kwa njia za utalii hapo? Tumeshafanya utafiti kuona kama tunaweza kufua umeme maeneo ya hapo?
ReplyDeleteWakatabahu,
Mdau
Namkumbuka Mh. Kalembo wakati huo alikuwa ni Brigedia wa kambi kule Biharamuro ni kiongozi safi sana anajua kunyosha watu maana wanajeshi walikuwa wanamuogopa kama simba. But ni mtu social sana nakumbuka alikuwa kila jioni anawakusanya wanajeshi bila kujali kama ni kopro au meja nakwenda kucheza nao mpira wa mikono alikuwa fiti sana kimazoezi. Pia sisi watoto wa kambini tulikuwa tunampenda sana maana hata akikuta wapi anasimamisha Land Drover yake ya kijeshi na kuwapa lifti kitu ambacho ni aghalabu sana jeshini.
ReplyDelete