Hello bro michuzi.

Hapa ni Ladique ushelisheli. Nani kasema chai maharagwe sio gari nzuri?Angalieni wenzenu hapa wanazipamba zinapendeza watalii wanazipenda kwelikweli.

Hizo picha ni Ladigue, Seychelles.

Mdau Mtanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. SHELISHELI NI NCHI INAYOTEGEMEA SANA UTALII NA WANAJUA FAIDA YAKE HII NDIYO INAYOWAFANYA WAWE WABUNIFU NA WASAFI, SISI UCHAFU NI JADI YETU NA HATUJALI CHOCHOTE. GARI HIZO MPE MTANZANIA MWEZI MMOJA UTALISAHAU LITAKAVYOKUWA LIMECHAFUKA.

    ReplyDelete
  2. Naungana nawe Anon wa kwanza, Hizi gari zipo miaka mingi zenjy ila ukiziona huwezi kujua ni jamii ya gari hizi tunazoziona kwenye picha, baadhi ya wamiliki wa huko zenjy wanachojali li flus(furushi) tu wakabidhiwe jioni baada ya makusanyo, matengenezo na urembeshaji au umaridadi wa hiyo gari anaachiwa mteja ajihudumia mwenyewe pale anapokaa aangalie kama pako mzeni au la! na usipoangaklia wawezatoka na kunguni unaposhuka.
    Tuige mazuri, utalii umeshamiri zenjy pia weupe na weusi wanamiminika sijui wanazungumzaje wakifika makwao juu ya mbavu za mbwa zile wakilinganisha na wanazozikuta sisheli.
    Mandhari na hali ya hewa inataka kulingana na ya pemba kwani hata mashelisheli (atunda adimu kuyapata bara, ukiyakuta ujue hiyo nyumba hapo ni kwa mpemba) yalojaa pemba yanapatikana kwa wingi huko sisheli

    ReplyDelete
  3. hizo zinaitwa strollers siyo chai maharage

    ReplyDelete
  4. lakini hii gari ikiwa bongo si tutaisha? nakumbuka kule mbagalla zile chai maharage zilivyokua zinakimbizana. Si wangetumwaga tu kila siku

    Hizo ni nzuri just for sight seeing

    ReplyDelete
  5. ASANTE SANA OCTOBER 15, 2008 7:22PM KWA KUTOFAHAMISHA KUWA NAWE KIMOMBO UNAKIJUA MUNGU AKUREHEMU. HATA HIVYO INAELEKEA UNA MAKENGEZA KWANI HAUJAWEZA KUTUONESHA TOFAUTI KATI YA HIZO NA ZILIZOKO HAPA, LICHA YA TOFAUTI YA USAFI TU. SIKU NYINGINE UKIKUTA MTU ANAKUKARIBISHA SIMA USISEME HII SIYO SIMA NI UGALI, INATEGEMEA UKO WAPI. anko, ulirudi lini toka shelisheli? uliwaacha hawajambo huko?

    ReplyDelete
  6. Anon wa oct.16,2008 10:14 umenipa kucheka sanaaa,

    Na hilo analoburura dume la ng'ombe linaitwa rikwama/toroli(gari la ng'ombe) tofauti yake limewekwa kipaa tu kumstiri mbebwaji asipate jua, sijui huko sishel wanaitaje wenzetu.
    Nakumbuka siku moja tulikwenda ukweni pemba, sasa gari hazifiki huko kijijini kwetu basi bankwe akatutolea hilo rikwama litupeleke mpaka barabarani na mizigo yetu, nilifurahia sana kwani ni mara yangu ya kwanza kupanda gari hiyo, ila wifi zangu walivaa kizoro/nikabu almaaruf ninja ili wasionekane kwani wakiona aibu kupanda gari la ng'ombe ambalo linaonekana ni usafiri hafifu. waima sikutaka kuwahoji sana nikafikiri pia labda ni katika tamaduni zao kwamba ntu nke hajitandazi hadharani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...