KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!

MKUTANO WA CCM SHINA LA READING
WANACHAMA WOTE –CCM READING
WAKEREKETWA WOTE-CCM READING
WAPENZI NA WANAMAPINDUZI WOTE WA READING
TAREHE: 19/10/08 SAA 8 MCHANA HADI SAA 12 JIONI

MAHALI: UKUMBI 79 LONDON ROAD,
READING RG 1 5BY.

KADI ZIPO KWA WANACHAMA WAPYA. KUMBUKA KUJA NA PICHA. BEI YA KADI NI POUND TATU NA POUND KUMI NA MBILI ADA YA MWAKA MZIMA.

TUMEWAALIKA WAGENI KUTOKA:
MWAKILISHI WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA UHAMIAJI [IMO]
KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA NCHINI UINGEREZA [UK]
MWAKILISHI WA MUDA WA JUMUIYA YA WATANZANIA- READING.

AJENDA KUU: UCHAGUZI WA WAJUMBE 15 WA HALMASHAURI KUU YA TAWI LA CCM UINGEREZA.

KWA MAELEZO ZAIDI TAFADHALI WASILIANA NA:

MAIRA BENJAMINE MIGIRE- 07799212095
KATIBU WA CCM SHINA LA READING

WOTE MNAKARIBISHWA – KUTAKUWA NA CHAKULA (free of charge) NA MUZIKI BAADA YA SHUGHULI ZOTE.

KIINGILIO BURE!!!!!!!!

Akhasante.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. endeleeni huko huko

    ReplyDelete
  2. Yaani wanawatega wadau kwa kutumia pilau, duh si mchezo.... wakiongeza na tshirt na kofia lazima wawapate wachache wasiosoma alama za mda

    ReplyDelete
  3. wanamapinduzi? mapinduzi gani? CCM ilipinduwa nini na lini? hichi chama ni cha zanzibar? zanzibar ndiko kulikofanyika mapinduzi, tanganyika kumepatikana uhuru. hata sherehe za nchi (ooppss vile zanzibar ni nchi?) zanzibar hushereheka mapinduzi wakati tanganyika husherehekea uhuru.

    ReplyDelete
  4. Mmeanza; nasema mmeanza,tunatafutana ubaya hapa. Well!! napenda kuchukua nafasi hii kuwakumbusha wadau wote mtakaoenda kwenye huo mkutano kubeba papers zenu na ziwe halali, kwani atakayeshukiwa na wajomba mimi tena hapo sina lawama. Kunradhi kwa wale mnaoona upuuzi huu wa kubaguana kiitikadi ili hali sote ni ndugu na tupo ughaibuni kusaka maisha kama nitawabughudhi kwa hili. Narudia!!! sina utani kwa hili lazima wajomba watie timu, sijui iweje, lakini lazima watatia timu.

    Wakatabahu.

    ReplyDelete
  5. NA MIMI NATAKA KUGOMBEA UONGOZI CCM LAKINI NAULIZA TU KUWA NAFASI HIZI ZA UONGOZI ZINAINGIA KATIKA ILE MISHAHARA MIPYA YA CCM YA KIMA CHA MILIONI MBILI ? TUENDELEZENI MAPINDIZI

    Mkereketwa

    ReplyDelete
  6. CCM walijaribu kuileta Marekani lakini kutokana na kupingwa na wengi naona imeshindikana. CCM iishie huko huko kwa wanyalu Uingereza.

    ReplyDelete
  7. i have got one "pathetic"

    ReplyDelete
  8. You guys don't have life? Kila jumamosi ni mikutano ya CCM. You need a new hobby my friends

    ReplyDelete
  9. msituchanganye nyie mnaojiita watu wa ccm reading chama kipo kwa ajili ya matumbo yenu yaan mpaka karne hii mnawashabikia hao mafisad(magaidi)tuondokeen na uchawi wenu

    ReplyDelete
  10. kaka/dada wa hapo comment ya juu hata hapa u.k imepingwa hii iko kwa watu wa bara tu,watu wa visiwan wajanja na hao walioko ni hao hao tu hakuna wapya nan atakwenda kwenye huo upuuz wao na lazima niwashtue wajomba maana wengi wao wameoza ndio wanajitia ccm

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...