JK akiwa na mgeni wake Rais wa Visiwa vya Madagascar Marc Ravalomanana wakipata vinywaji wakati wa dhifa ya kitaifa ya kumkaribisha mgeni huyo iliyofanyika Ikulu jijini Dar Kushoto ni Makamu wa Rais Dk. Ally Mohamed Shein, na kulia ni Mke wa Rais huyo wa Madagascar. picha na Anna Itenda wa Maelezo

Na Mwandishi Maalum
Rais Marc Ravalomanana wa Jamhuri ya Madagascar ambaye yuko nchini kwa ziara ya Kiserikali ya siku tatu iliyokuwa imalizike leo (Jumatano, Oktoba 8, 2008), ameongeza siku moja kwenye ziara hiyo.

Rais Ravalomanana ambaye aliwasili nchini juzi (Jumatatu, Oktoba 6, 2008) kwa mwaliko wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, sasa ataondoka nchini kesho (Alhamisi, Oktoba 9, 2008).

Kutokana na mabadiliko ya siku za kuondoka kwa mgeni wake, Rais Kikwete ambaye alikuwa aanze ziara ya Mkoa wa Mbeya kesho (Alhamisi, Oktoba 9, 2008), sasa ataanza ziara hiyo keshokutwa (Ijumaa, Oktoba 10, 2008), ili apate nafasi ya kumwaga mgeni wake kesho.

Hata hivyo, bado Rais Kikwete atawasili Mbeya kesho jioni, kama ilivyopangwa, baada ya kuwa amemwaga mgeni wake, tayari kuanza ziara yake keshokutwa.

Wakati wa ziara yake, Rais Ravalomanana amefanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, na pia ametembelea Zanzibar na mbunga ya wanyama ya Ngorongoro Crater mkoani Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...