Kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania leo imechagua washindi wengine wa muda wa maongezi katika mfululizo wa draw zake za kila wiki za promosheni yake ya Endesha Ndoto Yako 2 ambapo mkazi wa Rifiji Mkoa wa Pwani Yassin Pepeta (28) ameibuka mshindi wa zawadi kubwa ya wiki ya Muda wa Maongezi.
Droo hiyo iliendeshwa na Meneja Masoko wa Zain Kitengo cha Wateja KELVIN Twissa mbele ya waandishi wa habari na msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ambapo wateja wapatao 1,101 wa Zain watawekewa muda wa maongezi wa thamani ya Tshs 7.6m ambapo mshindi wa kwanza alipata muda wa maongezi wa Tsh 100,000, wateja mia muda wa maongezi wa Tshs 25,000 na wateja wengine 1000 muda wa maongezi wa Tshs 5000 .
Zain imeongeza draw za kila wiki katika promosheni yake ya Endesha Ndoto 2. Zawadi za awali katika programu hiyo ni simu za mkononi aina ya Blackberry na Nokia zinazotelewa kwa washindi wa Ndoto Points na magari aina ya RAV 4 pamoja na zawadi kubwa ya Land Cruizer itakayotolewa mwezi Desemba.
‘’ Tunaomba wateja wetu waendelee kushiriki katika promosheni yetu ya ndoto ili waweze kujishindia zawadi hizi za muda wa maongezi na kunufaika kwa kuwa sehemu ya familia ya Zain,’’ alisema Twissa.
Kelvin alisema zawadi hizo za muda wa maongezi ni utekelezaji wa matakwa ya wateja ambao waliomba zawadi ziongezwe katika promosheni ya Endesha Ndoto 2 ili watu wengi zaidi wanufaika.
‘’Siku zote Zain inawasikiliza wateja wetu ili kukidhi mahitaji yao na hilo ndilo limetufanya kuwa mtandao unaoongoza Tanzania.,’’ alisema na kuongeza kwamba Zain imezindua promosheni hiyo ya uaminifu ili kuwazawadia wateja wa Zain kwa kuwa katika mtandao wa Zain.
Hadi sasa Zain imetoa magari mapya aina ya RAV 4 sita. Gari la saba litakabidhiwa mwezi huu Mkoani Tabora. Zain itatoa jumla ya magari 11 mwaka huu.

Ebwana jamma nawakubali wako juu. Kevin Kichwa. Jamaa ni creative. Big up bro, keep it real
ReplyDelete