juu ni jengo ambalo disko lililosababisha vifo vya watoto 19 wakati wa sherehe za iddi jana. ukumbi wa disko ulikuwa ghorofa ya juu. chini ni mfanyakazi wa mochuari (picha imemegwa kwa sababu maalumu) akishughulikia maiti za watoto hao katika hospitali ya mkoa wa tabora leo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

 1. Poleni Tabora.
  Tukio kama hili linahitaji Rais Jakaya kwenda kutoa pole, hasa inapozingatiwa kwamba huwa anahudhuria ajali za watu ambao huwa wanamajina pale Muhimbili. Hili ni swala kubwa na sio kumtuma Mh. Kapuya.
  Anatakiwa kuwasili katika eneo la tukio na kukagua , kutoa pole na pia kuhutubia wananchi.
  Pia ni wakati wa TZ, hasa Fire marshal kuanza kuangalia uwezo wa sehemu za disco kuchukua kiasi fulani cha watu na njia za tahadhari (Exit)kama hali kama hii ikitikoea.Ikiwa ni pamoja na kuwa na Genereta, na wasaidiza wa haraka.

  ReplyDelete
 2. taarifa hizi zinasikitisha mno.na nadhani wengi wa victims hao watakuwa hao hao watoto tu.Mungu alaze roho zao pema peponi.

  ReplyDelete
 3. may the lord rest their souls in peace. those were angels of the Lord. Nawapa pole wanafamilia wote.

  ReplyDelete
 4. Sasa mbona habari yenyewe haijakamilika, wamekufa na nini? Moto, jengo limedondoka, sumu au? tupeni habari kamili.

  ReplyDelete
 5. HAWA WATOTO SIJUI NI WA LINE POLICE SASA SIKU YA IDD WALIKUWA WANATAFUTA NINI KWENYE MADISCO? INASIKITISHA LAKINI INAUDHI SANA WAZAZI WALIKUWA WAPI WAKATI HAWA WATOTO WANAJILUSHA? HALAFU WAKIVUTA BANGE WATUWALAUMIWE. SASA MICHUZI NI KWELI HIVI WAMEKUFA HAWA WATOTO AMA NI MAJERAHA TU? NI MIMI PETER NALITOLELA WA MUZUMBE CHUO KIKUU ALSO FINISHED HIGH SCHOOL ST. ANTONY MBAGALA FOR THOSE WHO REMEMBER ME A SMART KID!

  ReplyDelete
 6. kaisome hapa http://spotistarehe.wordpress.com/2008/10/02/breaking-news/
  jamani Mungu anakataza Maasi kuwapeleka watoto Disco si haki.
  Mungu awarehemu Marehemu woote.
  Mdau JJM
  A Town

  ReplyDelete
 7. Na wewe Peter Nalitolela vipi..watu wanaongelea maafa huko Tabora wewe unaleta zile zako za CV au kujitangaza hapa...hazitusaidii kitu kwenye habari kama hii ya majonzi...serikali ifanye uchunguzi wa haraka sana na raisi inabidi kwenda Tabora yeye mwenyewe... RIP

  ReplyDelete
 8. wewe nalitolea kweli umesoma chuo kikuu? mbona akili ni za chekechea? umeambiwa jngi limeanguka sasa na watoto 19 wamefariki sasa unauliza kama n moto au sumu? na kuhoji kama wameumia tu na kupta majeraha? unataka michuzi atumie kiswahili gani rahisi zaidi ya hicho. mimi nimesoma mzumbe two different programmes wakati wa idm na baada ya kuwa chuo kikuu nashangazwa na analysis hii.

  poleni sana wafiwa.

  ReplyDelete
 9. WEWE UNAEJIITA WA MZUMBE CHUO KIKUU UNA AKILI KWELI. SASA HUU SI WAKATI WA KUWALAUMU WAZAZI MAANA JANGA LIMAESHATOKEA. HAYO MAMBO YA WATOTO KUVUTA BANGI SIJUI UMEYAPATA WAPI NA HAPA SI PAHALA PAKE. NASHUKURU UMESEMA A SMART KID MAANA AKILI NI ZA KITOTO. AU HUJUI MAANA YA KID? KID HAWEZI KUSOMA CHUO KIKUU NI MTOTO MDOGO SANA.

  ReplyDelete
 10. Peter, elewa kwamba baada ya mfungo katika sikukuu ya IDD watoto huwa wanaruhusiwa kwenda disko, beach au mjini kutembea. Hivyo mikoani hilo Disco ndo sherehe yenyewe.
  Baada ya kula Pilau la heshima ujue kwamba kiu ya maji ni muhimu na ndani ya chumba cha Disko TZ ambalo halina hewa ya kutosha ni matatizo makubwa sana.
  Tuwape pole hawa wazazi wa watoto na sio kuwalalamikia kuwaruhusu kwenda Disko baada ya mfungo. Huu sio wakati wake. kama ni lawama basi ni hawa wenye disco na wenye hiyo nyumba ya disco na sio wazazi.
  Msaada ulitakiwa kuwepo , kama sio siku hiyo basi ni swala la kujifunza ili lisitokeee tena baadaye.Tumeshayaona haya katika meli- MV Bukoba la madhara yanayoweza letwa na idadi kubwa ya watu katika chombo au sehemu moja.

  Haya mambo yamesemwa sana lakini bado sehemu kama za Rumande na Cell za polisi bado huingiza watu wengi huku zikiwa bado hazina uwezo huo. Maana huwa hazina hewa na idadi ya watu wanaoingizwa humo haziizingatii uwezo wa hizo remand au cell. Tufuate sheria. Watu waliokuwa wanachukua tiketi wafungwe na majengo yawe na hewa na sio vyuma/nondo vya kuzuia watu kama inavyoonekana hapo juu katika hiyo picha.

  ReplyDelete
 11. huyu mwehu nalitolela ameibukia wapi tena? mbona nalitolela wa mzumbe hakuwa hivi? ni nini kimempata mpaka anaongea takataka kiasi hiki! maisha yamekuwa magumu kiasi hiki mpaka mtu tunaye mjua alikuwa smart leo anaandika vitu visivyo na kichwa wala miguu? ameambiwa watu wamekufa 19 halafu anauliza eti ni kweli? loh!

  ReplyDelete
 12. Mara moja kwa mwaka sikuu ya chrismas au Edd watoto huruhusiwa kufurahi/kutembea/hata disco toto si mbaya. Hakuna wakulaumiwa hapa!

  Mungu anajua kwanini imetokea hivyo. Pia ni Mungu tu atawapa nguvu wafiwa/wa Tabora na watanzania wote kwa ujumla. Poleni sana. May the souls of our beloved angels RIP! Grandma

  ReplyDelete
 13. Wewe Peter Nalitolela umeonyesha jinsi ulivyo na fikra ndogo kama za hao walioshindwa kuzuia hilo janga. Nafikiri ulikuwa "Smart Kid" kwa kuvaa tu lakini kichwani ni kweupe. Serikali ijifunze kuzuia majanga badala ya kuunda tume za uchunguzi wakati sababu zinajulikana. Ukweli ni kwamba majengo mengi ni mabovu na yanatakiwa kuthibitishwa ubora kabla ya matumizi. Serikali msiwe kama Peter Nalitolela kwa fikra fupi na kutuma salam kwenye misiba.
  Kwa wafiwa, poleni sana na msiba huu ni mkubwa tena wa kitaifa.

  ReplyDelete
 14. Inalilahii Waina Ilayhi Rajihuni jamani kwanza tunatakiwa kuwapa pole wafiwa wote na M/mungu awape moyo wa Imani katika kipindi hichi na awalaze mahara pema peponi Amini.
  Hikisha sio kuleta uho ujinga wa kutangaza C.V hapa.
  Mimi Nawapa pole sana Wafiwa;
  Mdau Ndambe
  uk

  ReplyDelete
 15. TUNAWAPA POLE KWA WALE WOTE WALIOFIWA NA M/MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI [AMIN] HUU SIO WAKATI WA KUTANGAZA SERA ZA C.V AMBAZO HAZINA FAIDA NDANI YAKE KINACHOTAKIWA NI KUWAPA POLE WAFIWA KWA MSIBA ULIYOTOKEA. mdau ASHA.

  ReplyDelete
 16. Wadau, huyo anayejiita Nalitolela si Nalitolela original. Ni jamaa mhuni tu anayependa kukaa na kuanza kuitumia key board yake kuharibia watu majina. Kama mtakumbuka aliwahi pia kutumia hata jina la Michuzi mwenyewe. Ni rahisi tu kugundua kama anayeandika ni Nalitolela mwenyewe au huyo fala mchawi. Kama maoni kiandika Nalitolela halisi basi pembeni ya jina lake huwa kanatokea kamdoli ka rangi ya orange na jina lake huwa la bluu vivyo hivyo kwa Michuzi au wadau wengine ambao ni mablogger. Ninamfahamu Nalitolela halisi siku nyingi hawezi kuwa na upeo mdogo wa ufahamu kama huyo mtanzania mwenzetu hapo juu aliyejiita Nalitolela. Tena huyo hata Mzumbe bado mpaka leo hajajua kuitamka eti MUZUMBE yaaakhh anatia kinyaa.
  Poleni sana jamani wadau wa Tabor, R.I.P marehemu wote.

  ReplyDelete
 17. Mmakonde utamjua tu mwacheni huyo Nalitolela

  ReplyDelete
 18. Loh poleni sana wazazi,jamaa,ndugu na marafiki wa hawa watoto.We learn through mistakes.Yaaani ni habari ya kusikitisha sana sana.Kwa wale wenye watoto wanaweza kuhisi uchungu walio nao wazazi wa hawa marehemu.Mungu azilaze mahala pema peponi roho za hawa watoto.
  Balozi michuzi.Wewe picha umeikata kwa sababu maalum lakini kuna chombo kimoja maarufu cha habari TANZANIA kimeibandika picha hiyo hiyo nzima kwenye moja ya magazeti yake ya leo.Maadili ya kiuandishi yanasemaje kuhusu picha zinazoumiza roho/nyoyo kama hii?Michuzi wewe ni mwandishi mkongwe unaweza kusaidia hapa kitaaluma.

  ReplyDelete
 19. I DON'T KNOW WHEN WE ARE GOING TO WAKE UP....THE PEOPLE ORGANIZED SHOULD BE CONVICTED OF MURDER PLUS TERRORISM ACT..

  ReplyDelete
 20. Kweli, Hbari hii inasilitisha sana. Mimi mji wa Tabora umepata pigo kubwa, nakumbuka wakati nikiwa Kazima secondary, Tabora miaka ya tisini, starehe pekee katika mji huo ni kwenda disco, hapa pale Mwanaisungu nafikiri ni karibu na hapo bubbles maeneo ya posta. Ukiingia disco baada ya dakika tano unavua shati ukumbi unatoa fukuto kama tanuru kwa jinsi wanavyoziba watu wasione ndani na kuingia bure. Najaribu kupata picha siku ya sikukuu watoto wamechanga vihela vyao kwa madhumuni ya ku enjoy, bahati mbaya ukumbi mdogo na labla mmoja mji mzima while demand kubwa na tamaa ya pesa kama kwenye daladala wanavyosema halijai na ukumbi pia haujai. Vifo hivi ni pigo na fundisho kwa Authorities kuwa safety precautions sholud't be impaired with greed for money. Natumai serikali yetu itaamka na kuanza kuangali maisha kwanza kwa watu kuwajibika badala ya pesa na rushwa.

  Mungu awalaze mahali pema watoto ambao ndiyo kwanza walikuwa wanaanza kuandaa ndoto zao katika maisha

  ReplyDelete
 21. Halafu michu sababu ya kuikata hiyo picha ni kwamba, motuary imejaa, wamelaza miili miwili miwili picha kamili nimeona ila ilipaswa utoe yote maana maendeleo hayaji kwa kuficha hali halisi.

  ReplyDelete
 22. wazazi kuwaruhusu hao watoto kwenda kuburudika huko disco si mbaya.nakumbuka enzi zangu hiyo Disco Toto huwa inaanza mchana saa 6 hadi saa 1 usiku.baada ya hapo watoto woote hutimuliwa na ndipo inapokuja zamu ya watu wazima.
  wazazi huruhusu watoto kwenda huko kutokana na muda kuwa si USIKU na pia husisitiza yule aliye Mkubwa awe anawaangalia wenye umri mdogo.hiyo ndio style ya jamii yetu ilivyo na si mpaka wazazi wawepo kuwatizama watoto zao wakisakata rhumba.
  tatizo hapo ni uroho wa pesa kwa hao wenye ukumbi kwa kujaza watoto bila kufikiria usalama.na nina imani hiyo itakuwa fundisho pia kwa wengine wenye tabia kama hizo.
  Mungu Mkubwa,wamekufa hao 19.maana kama ingetokea moto basi tungekuwa na msiba mkubwa mno Tanzania.
  R.I.P.

  ReplyDelete
 23. TUWEKE MBELE HEALTH AND SAFETY PRACTICES. TOTALLY UNNECESSARY AND AVOIDABLE DEATHS. SIJUI LINI TUTAJIFUNZA!!

  ReplyDelete
 24. jamani kwani nalitolea kawaambia kasoma mzumbe chuo kikuu? kasema wa mzumbe chuo kikuu labda anafagia au kusafisha choo mbona mnaassume tu kuwa kasoma chuo kikuu alichosema ni kuwa kasopma mbagala ila hatujia kama alipasi huko but ofcourse it is very unlikely kuwa alipasi hiyo mbagala

  ReplyDelete
 25. Nafikiri huyu jamaa anayejiita Peter Nalitolela ni feki Peter.
  Na sio yule wa Canada mwenye blog inayoitwa Economics and Forum.
  Tafadhali huyo feki aache mambo ya kuharabia watu majina.
  Tuwape pole Tabora na hatua za haraka zichukuliwe ili hali kama hii isitokee.

  ReplyDelete
 26. MIMI PETER NALITOLELA NAOGOPA KUNA MUTU ANATUMIA VIBALI VYANGU VYA MUZUMBE KUFANYIA KAZI..........!!!

  MICHUZI HIVI MIMI NIMEWAKOSEA NINI WANA BLOG? MBONA HAWATAKI MIMI KUTUMIA JINA LANGU KAMILI? KWANI TANZANIA NZIMA HAKUNA MTU ANAITWA MICHUZI NI WEWE PEKE YAKO? AMA KUNA KINA JUMA ABDALLAH WANGAPI, KUNA KINA JOHN MOSHA WANGAPI KUNA KINA MASSAWE WANGAPI? SASA IWEJE MIMI PETER NALITOLELA NIONEKANE FAKE NA HUYU MWINGINE ANAYE JIITA PETER NALITOLELA HATA MUZUMBE KWENYEWE HAJAFIKA ANASEMA MIMI NILIYE MALIZA ST. ANTONY MBAGALA KISHA KWENDA MUZUMBE CHUO KIKUU SIYO PETER NALITOLELA NIMEOMBA WAKINA NALITOLELA WAJITOKEZE NILIWEKA MPAKA EMAIL HAKUNA ALIYEJITOKEZA SASA MATUSI YA NINI? MIMI NITAENDELEA KUTOA MAONI HATA KAMA NITATUKANWA NI HAKI YANGU KUTOA MAONI NA NINA AMINI SASA KWELI WATU WOTE WAMEKUFA, NA KUTOKANA NA MAONI YANGU MKUU WA MKOA AMEFUNGA MADISCO YOTE NA WALE WAHUSIKA WAKO NDANI,KUMBE USHAURI WANGU NI MZURI SANA. KAMA KUNA PETER MWINGINE ALIYESOMA MZUMBE AJITOKEZE HUMU HUMU BASI, IKIWEZEKANA NA PICHA ZAKE TUZIONE, NAANZA KUHISI KUNA MTU ANATUMIA VIBALI VYANGU VYA SHULE KUFANYIA KAZI NA ANAOGOPA ATAUMBUKA SASA.

  ReplyDelete
 27. lakini ni vigumu kuelewa uhusiano wa hawa kina Nalitolela in this blog! I remember reading a comment which also say something about Bill O`reilly and the same comment I saw from Michuzi`s daughter come from nalitolela and mentioned Bill O`reilly! So I can`t tell who is a real Peter Nalitolela, I guess they are so many Nalitolelas therefore lets not be judgementals. Kila mtu awe ana concentrate na maoni yake basi.

  ReplyDelete
 28. Poleni wote.
  Michu hii nongwa jaribu kutoa sharti ya picha na comments kuanikwa kwa watu
  kama hawa Nalitolela .

  ReplyDelete
 29. CNN news inasema hawa watoto wamekufa kwa kukosa hewa. Ni kweli JK angeenda huku this is a big tragedy. Inatangazwa nchi za nje huku kwa CNN na wao hawaonyeshagi anything about our country sana. Jana nilivyoona nilishtuka sana wao walisema ni madancer wamekufa.....Mijitu mingine imezidi kuwa greedy hayo madirisha si ajabu walikuwa watoto zaidi ya 500 kwenye hicho chumba.

  Kwa vile kanchi ketu basi tu....hapo ingekuwa vipi hamna kuchukua sijui ubani au mkono wa pole.....wangesubiri msiba usihe wawasue mpaka nao wajue kumbe kuendesha biashara kiholela ni dhambi....wafilisini hao watu na vijumba vyao uchwara visivyojali uhai wa watu  Poleni sana wafiwa

  ReplyDelete
 30. Jamani pomoja na kutowa pole na rambirambi, pia PETER NALITOLELA hakukosea kutowa lawama kwa wazazi waliocha watoto zao wa under age kwenda alone kwenye Disco, according to UN CHILD RIGHTS ACT ambayo Tanzania pia imeridhia, hawa wazazi wanamakosa na wanapashwa kushitakiwa, ingekuwa huko majuu hawa wazazi wangekiona cha moto na kama wana watoto wengine ambao ni under age wangenyang'ywa na kulelewa na serikali under SOCIAL WELFARE DEPARTMENT, na wangepelekwa shule kujifunza namna ya kulea familia na kifungo juu, ni makosa kwa mzazi kumuacha mtoto wa under-age akienda peke yake sehemu kama hizo, pia mmiliki wa jengo anatakiwa ashitakiwa under CORPORATE MANSLAUGHTER LAW, hii itaenda down to the architecture aliye-construct jengo hilo hata kama ni kuanguka au hata moto, au hata kukosekana kwa hewa, how on earth that happens. HIVYO NALITOLELA HAKUKOSEA HATA KIDOGO KU-RISE CONCERN ZAKE, It is time now we have to change our old outlook, and we have to see things now holistically through 21st century's eyes. Nilisoma kwenye internet pia mzazi mmoja huko huko nyumbani alikwenda shambani na MARK II yake na watoto wawili alipofika shamba akawaacha watoto kwenye gari na yeye kuzunguka zunguka kuangalia shamba na madirisha ya gari yakiwa wazi, mtoto mmoja akatoa kichwa nje, na huyu mwingine kwa bahati mbaya akabonyeza button ya kupandisha kioo na kumbana mwenzane kooni hadi akatoa macho na kufa hapo hapo, baba aliporudi garini anakuta mmoja amekufa kwa kunyongwa na hicho kioo, hapa ni makosa a mzazi huwezi kuacha mtoto au watoto garini bila ya mtu mkubwa, ni hatari sana mambo mengi yanaweza kutokea kama vile moto nakadhalika, sijuwi iliishaje hii kitu, lakini alipashwa ashitakiwa na kula kifungo cha muda mrefu sana lupango kwa kusababisha kifo, huku kwa wenzetu huruhusiwi hata kuacha mtoto chini ya miaka kumi na mbili nyumbani pekee yake hata jirani wakijuwa unafanya hivyo watakuiita polisi.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...