ndugu, jamaa na marafiki wa watoto waliokufa kwenye disko toto siku ya iddi wakinwa nje ya hospitali ya mkoa ambako maiti zimehifadhiwa
Na Mwandishi Maalum, Tabora
JK amemuagiza Mkuu wa mkoa wa Tabora Bw. Abed Mwinyimsa kuchunguza na kubaini chanzo cha vifo vya watoto 19 waliokuwa wakishiriki disko toto, tukio lililotokea jana jioni mjini humo.Pamoja na watoto hao kufa wengine 16 wapo hospitalini Kitete kwa matibabu.
Watoto waliofariki ni Veronica Wanigu(7)Beatrice Makelele(14)Jacob Gerald (12)Salma Hamisi(12)Hadja Waziri(10) Rehema Moto (12)Seleman Idd (11) MrishoSeleman (10)Abdalah Rehan (14’)Agatha Manigu(12) Paulina Emanuel (11) Mohamed Kapaya (15) Ramla Yenga(15)Habiba Shaaban (14).Wengine ni Donald Kasela (12)Mwanahamisi Waziri (11) Ashura Jabal (12) na Yasin Rashid (11).
Waliolazwa hospitali hospitali hadi sasa baada ya wengine kumi kuruhusiwa ni Msimu Rehani (14) Naomi Joseph (13) Tatu Amani (15) Kulwa Idd(12) Sakina Ally (10) na Jumanne Abdallah(11).
Rais kwa kupitia Waziri Athuman Juma Kapuya amesema kwamba amesikitishwa sana na tukio hilo na kutuma salamu zake za rambirambi kwa mkuu huyo wa Tabora na wafiwa.
Kutokana na agizo hilo serikali mkoani hapa imeunda tume maalumu itakayoshirikisha wadau mbalimbali ili kubaini chanzo cha tatizo hilo na kuhakikisha halijirudii tena.Kutokana na msiba huo, Rais Kikwete ametoa ubani wa shilingi laki tano kwa kila marehemu ambapo shirika la hifadhi ya jamii(NSSF) ambalo jengo lake ndilo lina kumbi hizo limetoa shilingi tano kwa kila marehemu na shilingi laki moja kama pole kwamajeruhi, na serikali ya mkoa wa Tabora imetoa shilingi elfu hamsini kwa kila marehemu.
Mitaa mingi ya mji huu imebaki kuwa na watu katika makundi makundi wakijadili tukio hilo na wengine wakilia kwa kupoteza watoto au ndugu zao.Mkuu wa Mkoa ameagiza kufungwa kwa kumbi zote za disko na dansi mpaka atakavyotangaza vinginevyo.
Naye Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Tabora amesema kwamba wamiliki wa kumbi mbili za disko Bubbles Night Club, Shashikanti Patel na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Projestus ambaye anamiliki Top Five disco sound wanashikiliwa na polisi mjini hapa kufuatia tukio hilo.
Watu hao wanatakiwa kuisaidia polisi katika uchunguzi wake.
Msanifu wa majengo aliyesanifu jengo hilo la NSSF ambako tukio hilo lilitokea John Mlundwa alisema kuwa kumbi hizo zilijaza watoto kinyume na uwezo wake na kuongeza kuwa kumbi hizo zilijengwa kwa matumizi ya mikutano na matumizi ya ofisi na siyo matumizi ya sherehe za watoto kwani watoto wanatakiwa kustarehekatika maeneo ya wazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

 1. NILISIKIA NSSF IMETOA SH. LAKI TANO KWA KILA MTOTO ALIYEFARIKI NA SI SH. TANO KAMA ULIVYOANDIKA.

  ReplyDelete
 2. shilingi tano kwa kila marehemu?!!!! i hope ni kosa la ku type ama vyenginevyo......

  Nawapa pole ndugu na wazazi waliofiliwa na vipenzi vyao, mola awape moyo wa subira.

  ReplyDelete
 3. Maeneo ya Wazi ya wapi mjini Tabora?Je,kuna uwanja wa mabembea na michezo ya watoto japo mmoja tu katika mji mzima wa Tabora?Kosa la nani?Asitafutwe mchawi hapa au kurushiana lawama.Poor Leadership in Government Institutions is the cause of all this.Mpaka watoto zetu wafe ndipo viongozi wakurupuke na kujifanya wanahusika kwelikweli kumbe usanii tu!What a Pity?Viwanja vyao vya michezo vingekuwepo mtoto gani angefikiria aende disco aache mabembea?too much politicking!Nothing Doing,eti tuna Doctorate Degrees!Za kubandika ukutani?

  ReplyDelete
 4. Nawapa pole wafiwa na wanatabora wote kwa janga hili la kitaifa. Tunajifunza nini kwa hili?
  1. Maafa na ajali zinazomaliza maelfu ya watanzania ni vitu vya mpito tu na serikali haitilii maanani kuyapunguza. Ripoti za chang'ombe, Kisutu, muhimbili zimefanya nini kupunguza majanga haya?
  2. Tutaunda tume 100 lakini hazisaidii kumaliza majanga kwa sababu ya kutokuwa makini na kujali maisha ya watu wa kawaida.
  3. Kama watoto hawatakiwi kwenda disco, je serikali mkoani tabora hawakuona hilo? 4.
  Kama wanaruhusiwa kwa masharti, basi NSSF (mmiliki), Mpiga Disco (mkaribishaji)na Manispaa (dhamana ya ukaguzi) wawajibishwe kikamilifu.
  Watanzania mliopo nyumbani wakumbusheni viongozi majukumu yao kwa kupinga haya mambo. Wanasheria wasaidieni waathirika na hakikisheni wanapata "fair and adequate compensation" na iwe fundisho kwa wengine.

  ReplyDelete
 5. JAMANI, MBONA HAMTUELEZI CHANZO CHA VIFO VYENYEWE?????...KILA BLOG NIKIENDA HAKUNA HATA MOJA INAYOELEZEA CHANZO CHA VIFO HIVI VYA KUSIKITISHA!!!CMON MEN. POLENI SANA JAMANI

  ReplyDelete
 6. Jamani watu wa Tabora na wafiwa wote poleni sana.
  Nimesoma comments za Architect/Mbunifu wa Jengo nikasikitika sana. Eti ukumbi umejengwa kwa matumizi ya mikutano na ofisi wala sio matumizi ya sherehe za watoto!!!! What an answer from a qualified architect?
  WANAOTUMIA KWA MIKUTANO NI WATU, WATOTO NAO NI WATU, issue ya kukosa hewa inahusika vipi hapo?
  au consumption ya hewa kwa watoto ni kubwa kuliko ya watu wazima? Je huyo DJ wa watoto hakuona hali inavyoanza kuwa mbaya then akaomba msaada polisi? Je (watu wazima)waliokuwa wanahudumumia watoto hawakuathirika? Ilikuwaje watoto wote 19 wafe at a go? hakuna aliyeanza kuumwa then wengine washtuke? Kuna maswali mengi sana.
  TUTAUNDA KAMATI HADI LINI?????

  ReplyDelete
 7. Poleni sana wafiwa.
  Tukio kama hili likitokea nchi za magharibi wahusika(wana ulinzi,wamiliki,wafanyakazi) wa jengo huwa wanafunguliwa mashtaka ya mauaji,sio huko kwetu.Nina imani wamiliki wa jengo na wafanyakazi wa humo wataondoka bila kesi wala nini.Na huwa nachukia watu wanavyosema "hii ni mipango ya Mungu,au Mungu ndiye alipanga kuwachukuwa hawa watoto".Tukio huwa linaonekana ni la uzembe lakini watu watamsingizia M/Mungu kwa kilichotokea.Inauma sana kuona sherehe inapogeuka kuwa Msiba.Sijui ni lini watanzania tutajifunza kufuata na kujali kanuni za usalama.Inasikitisha sana.Nasema tena POleni Watanzania wenzangu

  ReplyDelete
 8. anony wa 2:27 PM, iliposemwa kwamba ukumbi ulijengwa kwa ajili ya mikutano za ofisi na si sherehe za watoto...
  point haikuwa kutoafutisha kati ya watoto nawakubwa. Point ilikuwa kutofautisha idadi ya watu. Katika mkutano wa kiofisi the number of people in the hall would be far much less than idadi ya watu ktk sherehe iwe ni sherehe ya wakubwa au watoto.

  Kuweka watu wengi kuzidi idadi kunahatarisha usalama kutokana kwanza na uwepo wa hewa; pili uwezo wa jengo kuhimili uzito/purukushani; tatu inapotokea dharura, ni vigumu kwa watu kutoka nje. Ndio mana ukumbi wowote uliojengwa kubeba watu wengi, lazima uwe na double doors zinazofunguka kwa nje, ili watu waweze kusukuma na kukimbia maafa.

  Mwisho naomba kutoa salamu za rambirambi kwa wafiwa wote na wakazi wa mkoa wa Tabora kiujumla. Naungana na wadau hapo juu wanaosema tume zimetosha sasa. Maana tunapatatume kila kukicha, katika ufisadi, ajali, migomo, matatizo ya Muhimbili, n.k. Lakini hatuoni mapendekezo ya tume hizo yakifuatwa. Inatupasa watanzania sasa kuachana na mambo ya zima moto... tabia ya kuunda tume kuchunguza kilichokwishatokea. Inatupasa tuchukue juhudi za makusudi kukemea uzembe, ubadhirifu, wizi, ufisadi, n.k.

  ReplyDelete
 9. Kutupiana lawama ndo mamabo yetu kila siku hakuna anayekubali kubeba mzigo.
  hilo jengo naamini halikuwa mara ya kwanza kutumika kama sehemu ya disko toto, harusi au graduation party. Hakuna aliyesema halifai.
  Huyu msanifu majengo anaposema halikutengenezwa kwa ajili hiyo ni muongo sana.Anatakiwa sasa yeye ndo ashtakiwe namba moja , kwani kama msanifu mkuu wa mkoa wa Tabora alikuwa wapi kuandika, kushauri au hata kuagiza kufunga ukumbi huo kwa matumizi ya namna hiyo.
  Hapa nje tunaona maeneo kama hayo yanaruhusiwa kufanya shuguli kama hizo ila , idadi ya watu inazingatiwa sana kuhusiana na vyombo vilivyopo.
  Watu kama hawa wanaotoa habari potofu sasa wakati huko mwanzo hawakutoa dukuduku lolote kimaandishi, au hata kwa mdomo katika vikao vyao vya kazi au hata kuwanyooshea kidole halmshauri ya mji Tabora, au mji mdogo Tabora au hata Wilaya au mkoa, ndio wanaofaa kuwajibishwa kwanza.
  Halafu wakafuata sasa wenye hisa ndani ya hilo janga. Pia tujue ukweli. Maana huenda waliomba msaada au kupiga simu na bado Fire, ambulance hawakufika.
  Ni swala la kuwajibisha watu wengi na sio lawama ili waliokuwa wanatakiwa kusema wabaki.
  Waliotoa vibali vya disco liwe linapigwa hapo pia washirikishwe na serikali ikubali kushindwa katika mambo muhimu ya raha kwa watoto.
  Juzi tumeona dar - Coco beach watoto walikuwa wengi lakini watu wakuwasaidia wakati wanaogelea -ZERO. Mmeuza viwanja vyote vya watoto kuchezea kwa mafisadi halafu mnasema watoto walikuwa waende wakacheze nje wapi?
  kazi watu wa serikali na mashirika TZ ni kwenda kunywa mipombe jioni na nyama za kuku na mbuzi kwenye mibaa na kusema tunajenga nchi.Acheni uzembe.

  ReplyDelete
 10. 1.John Mlundwa awe wa kwanza kuwajibishwa na asiachiwe kuzungumza kupotosha ukweli.
  Huwezi kuwa mbunifu majengo wa NSSF halafu hufuatilii matumizi yake kihalali .
  2.Aliyetoa kibali cha disco lichezwe hapo pia akamatwe.
  3. Aliyeruhusu idadi kubwa ya watu, mwenye disco, DJ nk wanastahili kuhojiwa kwanza na sio kuwekwa ndani , kawani bado tunahitaji kujua ukweli mwingi kutoka kwao. Maana wao wanajua kila kitu na tukio na kuwaweka ndani huenda ni kuficha ukweli wa hali halisi kabla na wakati wa tukio.Baada ya kujua ukweli basi tuwaweke ndani.
  Ila wale ambao husaini vibali vy a majengo, sherehe, kuchukua kodi ya pango na kubaki maofisini ndio wanataliwa kwanza kufungwa. Kwani bila wao kusaini hizo documents watu wa Disco, na DJ wasingeweza enda pale in the first place.
  Kuna mabwalo mengi sana ya chakula katika shule za sekondari mjini Tabora, vyuo na vyuo vya ualimu nk kwa nini havikutumika hivyo? Kwani masaa ya disco toyo huwa saa saba hadi saa kumi na mbili jioni.
  Waliotoa vibali na kusaini vibali ndio wawajibike.
  Tuwape pole sana mama zetu , baba zetu, na ndugu zetu wote Tabora.
  jakaya Kesho uwe uko Tabora kujionea hali halisi na sio kusubiri taarifa toka kwa mkuu wa mkoa.

  ReplyDelete
 11. Jamani Tanzania si tambarare siku hizi na sheria zetu ziwe tambarare....make sure hao watu waliohusika kupoteza masiha ya watoto hao wanakua sued mpaka penny yao ya mwisho.

  Sijazaa mtoto bado lakini naelewa uchungu wa kufiwa na mwana....Ninaona this through mama yangu....since my brother passed away my mother and our family in general never be the same.....

  Watu wanauchu wa hela na kujaza watoto mpaka suffocate. Kwanza iweje watoto wa miaka saba wawekwe na kwenye jumba moja na watoto wa miaka 15 and up?

  ReplyDelete
 12. Hivi huko kutakuwa na bia? mimi naondoka kesho asubuhi kuelekea Tabora sina mwenyeji lakini kutokana na huu msiba mzito nategemea kukutana na mtu yeyote atakaye nipa hifadhi ya taifa. mazishi ni lini kuna mtu anataarifa jamani?

  ReplyDelete
 13. Anon wa 03 october 8.37 pm,

  Ulimwenguni kote shughuli ya architect (mbunifu wa majengo) kazi yake huisha anapokabidhi jengo kwa mmiliki baada kupewa hati ya inayohisi kuishi wanadamu ndani ya jengo (occupation certificate).

  Manispaa kazi yake ni kukagua jengo na kutoa occupation certificate ikiwepo na inspection zote baada ya hapo (umeme, usafi, matumizi ya jengo etc) walau mara moja kwa mwaka.

  Architect hana kosa kama use of building ni mikutano na likatumika ndivyo sivyo hilo ni kosa kwa mmiliki wa disko na manispaa, kwa kuwa, kuna marekebisho yanatakiwa kufanywa na kabla ya marekebisho inatakiwa hati ya change of use, etc.

  Disko linahitajika hewa zaidi ya jumba la mikutano kutokana na idadi ya watu ni wengi na wanakuwa na joto hivyo kiasi cha ubaridi na hewa ni nyingi zaidi inahitajika.

  Vile vile milango ya kutokea kwenye tahadhari inatakiwa kuweza kupitisha idadi ya watu kadhaa katika muda wa dakika kadhaa kwa usalama.

  Idadi ya watu wanaotakiwa kuwemo ndani ya ukumbi wakati wowote ule inatakiwa isizidi, ndio maana kumbi za ulaya utakuta watu wanangoja nje mpaka wengine watoke, wakitoka wawili wanaruhusiwa ndani wawili.

  Sasa haya yote si lazima architect awepo, kwa mikataba ya kusanifu majengo kazi ya architect inakwisha baada ya kupeana funguo na mwenye jengo (n.b ukishapita muda wa guarantee miezi 6 etc)

  naomba niwakilishe,
  Mdau mhandisi msanifu ughaibuni

  Kumbi feki nyingine zote zinatakiwa zifungiwe kufanya harusi, send off etc kama hazijatimiza mambo haya ya kimsingi.

  ReplyDelete
 14. Mdau, mhandisi msanifu ughaibuni taratibu ulizozisema ziko ughaibuni na zinafuatwa kisheria huko ughaibuni na pia anatakiwa msanifu wa hapa TZ kuzifuata, Kwani msanifu majengo amesomeshwa hizo sheria na taratibu na vitabu vya nje sio vya kiswahili.
  mhandisi Msanifu wa jengo ndio mwenye mamlaka ya jengo na mhandisi majengo hufuata alichoidhinisha mhandisi msanifu majengo.Makubaliano mengi ya makabidhiano hulenga jengo linapokuwa likijengwa hadi likikamilika, bado mhandisi msanifu majengo hukagua kuangalia kama linaenda na usanifu aliyoupanga.
  Jengo limekwisha , sawa ,leo ni jumba la mikutano, lakini linatumika kama Disco toto Tabora na kumbi zote mbili zinajulikana Tabora siku zote kwamba ni za disko. Huwezi niambia kwamba msanifu majengo hana habari au hajui lolote juu ya jumba alilolisanifu.
  Ki-Utaratibu anatakiwa kupitia kila jengo alilosanifu na kuangalia umakini wake kwa mda aliosema yatadumu. Mara nyingi kikomo huwa miaka ishirini (hadi hamsini ikibidi)kulingana na mkataba na baada ya hapo mwenye jumba/jengo hubeba lawama na jukumu pekee yake.
  Makbidhiano ya miezi sita ni kumpa mwenye jengo au kazi muda wa kuona kipi anachohisi hakikufanywa vizuri na kukirekebisha kwa gharama za mhandisi msanifu majengo au mhandisi ufundi majengo.
  Ieleweke unapobadili matumizi ya ghorofa au kusudio la awali la ujenzi wa jengo etc bado kuna wahandisi watashirikishwa(akiwemo msanifu wa hilo jengo wa awali) kukubaliana na uamuzi huo na marekebisho kadhaa lazima yafanywe kulingana na rekebisho hilo.
  Juzi Tabora tumeona John Mlundwa (Mhandisi Msanifu majengo) alikuwa wa kwanza kusema halikujengwa kwa ajili hiyo, huko ni kujiondoa lawama.
  Hiyo sehemu wameenda watoto sio mara moja ni zaidi ya mara hamsini na hapo hapo hiyo pia ni night club kulikofanyika sherehe hizo inajulikana Tabora nzima kwa miaka mingi sana.
  Kama msanifu jengo amekuwa wa kwanza , kwa nini hakusema mwanzoni hata kumuandikia memo RC au DC au hata Mbunge wake kama alihisi kutakuwa na madhara na jengo alilolisanifu yeye linatumika isivyopaswa.
  Hii ndio ninasema sasa, kwamba TZ tumezoea kuona vitu vinafanyika na kusema sio changu au sio mimi , acha mpaka tukio litokee.
  Mhandisi msanifu ni mtaalamu angesema tu au kuandika kwa wakuu wa manispaa nk kulalamikia matumizi yasiyo mazuri kwa jengo alilolisanifu. Kwani anapokuwa anaandika CV zake huwa analiweka hilo jengo kwamba ni jengo alilofanya kazi yake vizuri.Kwa nini bado aliweke kama hana mamlaka nayo .
  Simtetei na wala simuonei anatakiwa yeye ndio awe wa kwanza na wengine wafuate. Ni sawa na jengo likindondoka Dar na ikaonekana msanifu alifanya kazi yake vizuri basi mhandisi ujenzi atashitakiwa na sio mhandisi usanifu kama mkataba ulikuwa atalikagua likiisha. Ikionekana ni wote walisaidiana kuficha madhambi basi wote watashitakiwa.
  Jengo halina hewa ya kutosha, halina madirisha ya Exit, halina idadi ya watu wanaotakiwa kuingia kwa kipindi fulani na hakuna wakuuliza kila mtu nasema sie yeye.
  sasa nani wa kukamata kwanza ni Juhn Mlundwa, then waliosaini jengo kuwa Disco,waliokuwa wanachukua kodi kila miaka, then waliokubali kupiga mziki na kuendelea.
  matangazo yaliwekwa na kila mtu aliyaona Tabora nzima na ndio maana watoto walikubaliwa kwenda hapo, ni sehemu inajulikana kwa kila mtu aliyewahi fika Tabora.
  Ninawapa pole wafiwa sana.
  Lazima akamatwe mwenye ,makosa toka Mwanzo na sio mtu baki aliyefanya kwa kupitia watu wengine waliokubali madhambi yake kwa rushwa walizomuomba ili aruhusiwe kupiga mziki.

  ReplyDelete
 15. Peter Nalitolela wa Oct 3 9:51natumai sio wewe uliyeandika kwamba unaenda Tabora kwa ajili kuna bia. Japo naona e ya rangi ya njano unayokuwa ukiitumia kama nembo yako. Bado naamini sio wewe.
  Peter ninayemjua mimi aliye Canada hawezi andika hivi, kwani ni msomi.
  jamani kama kuna mtu anamchafulia huo jamaa (Peter) jina lake basi aache au michuzi uwe unamtoa.
  Maana anachafulia watu majina.

  ReplyDelete
 16. Nawapa pole wafiwa wote

  ReplyDelete
 17. Anon wa october 04 2.06 a.m

  Poleni wafiwa,

  Naona hii ni moja matokeo ya siasa kuingilia mambo ya kitaalam, manispaa hazifanyi kazi zake zimejaa wanasiasa badala ya kuwa na wataalamu wa kutosha kukagua michoro na majengo na kuweka mifumo sahihi ya kufanyia kazi za kitaalamu.SIASA + UTAALAMU = MAJANGA

  Msanifu majengo (architect), na consultant wengine wote, mkataba wao unakwisha(liability) jengo likiwa limekabidhiwa kwa mwenyewe, na siyo miaka ishirini, hilo halipo ulimwenguni popote.

  Kuwepo kwenye CV haimaanishi kuwa anatakiwa awe analipitia na kulikagua.

  Manispaa ndio inatahusika na kuhakiki matumizi ya jengo ni kama kwenye kibali cha jengo.Mfano mzuri ni magereji na viwanda uchwara kwenye maeneo ya nyumba za kawaida.

  Msanifu majengo (architect) atakuwa na makosa kama katika kusanifu hakwenda sambamba na viwango vya jengo lolote la kawaida kama vile kutokuweka milango ya hatari, ngazi maalumu za wakati wa hatari na kuingiza hewa ya kutosha ndani kutoka nje (viyoyozi vingi huwa vinapoza hewa iliyopo ndani haviingizi hewa kutoka nje), vifaa vya kutahadhirisha na kuzima moto, taa za wakati wa tahadhari etc. kwa hili, hata huyo msanifu wa manispaa anayepitia ramani za majengo na kutoa rukhsa ya ujenzi, (building permit)atakuwa na makosa.

  Hii imetuonesha sehemu moja tu lakini kuna uozo mwingi sana katika manispaa na mipango miji, mapaka ajali zikitokea ndio tunaunda tume amabazo hatusikii zilichofanya na tunarudi pale pale kwa kuwa SIASA inatawala.

  Mhandisi makini aliyechoshwa na siasa.

  ReplyDelete
 18. WAFIWA POLENI SANA,

  HUU NI WAKATI AMBAO TUNGEPENDA KUSIKIA VIONGOZI WA TANZANIA ASSOCIATION OF ARCHITECTS NA INSTITUTION OF ENGINEERS WAKITOA MATAMKO RASMI KWENYE VYOMBO VYA HABARI KUHUSU HALI HALISI YA MAJENGO TANZANIA NA KUTUELEZA JINSI UTAALAMU WAO UNAVYOWEZA KUSAIDIA WAKIACHIWA KUFANYA KAZI ZAO.TUNATEGEMEA PRESS CONFERENCE KUTOKA KWA CHAIRMEN WA HIZI INDEPENDENT INSTITUTIONS.

  WAANDISHI PIA HUU NI WAKATI WA KUWAHOJI WATAALAMU NA SIYO MADJ NA WANAMUZIKI.

  ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...