habari za kazi,Kwanza kabisa napenda kuanza kwa kukupongeza kwa kazi yako nzuri ya blog hii ambayo inatuhabarisha mambo mbalimbali yanayoendelea nchini kwetu na hata habari zingine za watanzania waishio ughaibuni na pia habari za kimataifa.
Nami napenda kuwafahamisha watanzania wenzangu kuhusu yaliyojiri katika jiji la Geneva nchini Switzerland mwishoni wa wiki iliyopita.
Ile Jumuiya ya watanzania waishio nchini Switzerland (TAS) ikimaanisha Tanzania Association in Switzerland iliyoanzishwa katikati ya mwaka huu,hatimaye juzi jumamosi ilizunduliwa rasmi na Mheshimiwa Spika wa Bunge la Tanzania,Mheshimiwa Samuel Sitta ambaye yupo nchini Switzerland kwa ziara fupi ya kikazi.
Mheshimiwa Sita alikuwa ameongozana na waheshimiwa wabunge wengine 5 ambao nao pia wameliwakilisha bunge letu tukufu la Tanzania. Kilichonivutia zaidi ni jinsi ambavyo baina ya wabunge hao kulikuwa na mbunge mmoja kutoka chama cha upinzani CHADEMA na pia mbunge kutoka Visiwani Zanzibar.
Aidha sherehe hiyo ambayo ilifana kwa kiwango cha hali ya juu sana ilifanyika nyumbani kwa Mheshimiwa Balozi Martin Lumbanga na watanzania zaidi ya 60 kutoka mikoa mbalimbali ya Switzerland walihudhuria.
Pamoja na mambo mengine mengi watanzania hao walipata fursa ya kujadiliana na Mheshimiwa Spika pamoja na ujumbe wake mambo mbalimbali ya maendeleo na hali halisi inayoendelea kule nyumbani Tanzania.
Mheshimiwa spika pia alipanda mti wa kumbukumbu wa jumuiya hio hapo nyumbani kwa balozi.
Tunazidi kutoa wito kwa Watanzania wote waishio nchini Switzerland kujiunga ili kuweza kuwa na umoja utakaoweza kuwakutanisha katika matukio mba limbali ya kijamii zikiwemo sherehe na katika shida pia na hata katika matukio ya kitaifa.Aidha pia tunatoa changamoto kwa watanzania wengine waishio nje na nyumbani kuunda jumuiya mbalimbali ili kuweza kuwakutanisha na kuwaunganisha.
Mungu Ibariki TAS.
Mungu Ibariki Tanzania.
Mungu Ibariki Tanzania.
hongereni wana TAS.
ReplyDelete