wadau kunradhi,
sina kawaida ya kuingilia mijadala ya wadau ila kwa hili imenibidi maana kumekuwepo aina fulani wa uchafuzi wa hali ya hewa ambao si maadili ya globu hii ya jamii.
kwa kipindi kirefu sasa jina la peter nalitolela limekuwa likiibuka, hususan kwa marumbano baina ya wadau wachangiaji wanaojitambulisha kwa jina hilo. tatizo nililoliona ni vile mada husika huwa hazijadiliwi badala yake kumekuwa na majibishano ya nani ni nani.
kwa idhini yenu na kwa moyo mzito wadau naomba niliwekee karantini jina la peter nalitolela hadi hapo ufumbuzi wa namna ya kuendelea na libeneke pasina kuwa na haja ya kuchafua hali ya hewa utapopatikana.
wadau wote nawapenda na kuwaheshimu. ningependa pia kupata maoni toka kwenu na hata toka kwao wenyewe ili tujue namna ya kutatua changamoto hii.
hivyo naomba ikiwezekana na kama wataridhia wadau hao wawasiliane nami kupitia njia ya uani ya issamichuzi@gmail.com ili ikiwezekana niwapatanishe na mambo yaendelee kuwa mswano.
samahni kama nitakuwa nimemkwaza mtu. yote hii ni katika kuendeleza libeneke ambalo linazidi kunoga. nawatakia wikiendi njema woooote
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Tehe tehe utasikia Ndabagoye mwingine,wale akina Ndaki waliishia wapi,Eddo.

    ReplyDelete
  2. Aroo mimi ni Peter Nalitolela wa Mzumbe. Nimesoma Mbagala St. Antony.

    Kwenye ukoo wetu tuko Peter Nalitolela WATATU na wote tumesoma Mzumbe na St. Antony Mbagala kwa miaka tofauti.

    Na napenda kukufahamisha kuwa nilipata division ONE Mzumbe na division ONE Mbagala.

    Asante sana Balozi wa Zain. Hivi sasa niko nje ya nchi nikirejea Bongo nitapita kukusalimu Balozi ili kuondoa utata kwa wadau wa globu hii ya jamii.

    Ni mimi mdau wako Peter.

    ReplyDelete
  3. Michuzi mimi nina mawazo yafuatayo sijui kama yatasaidia.Wanablog wanaomfahamu Peter Nalitolela halisi wakupatie contacts zake(kuna wanablog wengi wamesoma naye naye).Ukishampata Nalitolela unampa maneno fulani ambayo atakuwa anayaweka mwisho wa comments zake.Hayo maneno au herufi mtakuwa mnazifahamu wewe na Nalitolela Original.Nalitolela original akiwa anatuma cooments zake anaweka hiyo siri.Kabla ya kupost comments zake unayatoa yale maneno.Ni kazi ya sekunde.Comments zingine za Nalitolela ambazo hazina hiyo 'siri' hakuna kuzipost.Kuzuia unamnyima Nalitolela halisi hake yake.

    ReplyDelete
  4. Mwe nimepitwa who is Peter Nalitolela?

    ReplyDelete
  5. suluhisho ni kwa bro michu kutoruhu kabisa jina hilo, mdau hapo juu kasema kuwe na neno la siri wakati wa mawasiliano kati ya michu na huyo peter lakini kama mdau wa juu kabisa alivyosema wapo jamaa zaidi ya mmoja ambao wote majina yao ni hayo na wote ni original kutokana na kuwa hayo ndio majina yao.
    kutoa utata ni kuzima tu mwendo wa anonymous tu kwa ujumbe wowote unaotoaka kwa jina hilo.. kwani sisi hatuna majina mbona tumeamua kuwa private..?? tuliona utata kama huo unaweza kutokea majina kama John christopher,Hassan Ali, Idd, athumani nk wapo kibao tu
    hauwezi kusema nani ni original na nani ni fake.

    ReplyDelete
  6. Yeah! kill that name. Hizi comments unazopokea I am sure ni zaidi ya mia kwa kila siku. Huo muda wa kuchuja hiyo secret word utaupata wapi? Wanafikiri una personal assistant nini? And they totally forgot that you need a life too.


    Si watumie tu anonymous? Sio lazima tuwajue kuwa ni wao wametoa comment fulani kama wanataka kujieleza sana wafungue blog zao ....Hapa waende kwa mwenda wa anonymous only wakupunguzie shida

    ReplyDelete
  7. Bro Mimposi, that could not be a big issue, majina yanaweza kufanana, hilo jina inawezakana ni la ukoo na peter ni very common name. Mimi naitwa mwakalebela nina mtoto wangu anaitwa David na kaka yangu pia anaitwa david so wote wanaitwa david mwakalebela but sio yule mchezaji wa yanga zamani. som Bro mimposi solution ni kwamba get intouch with all let them know each other inawezekana ni ndugu kabisa.

    Cheers

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...