KWA NIABA YA FAMILIA YA ASHURA KASHEBA WA LONDON TUNAPENDA KUKUMBUKA MPENDWA WETU NDALA KASHEBA TOKA UIAGE DUNIA 22 OCT 2004 AMBAPO MWEZI HUU AMETIMIZA MIAKA 4 TOKA UTUTOKE.
UCHESHI WAKO NA UKARIMU WAKO KATU HAUTASAULIKA KWANI UMEBAKI KUWA KUMBUKUMBU KUBWA SANA KWETU.
JAPOKUWA SIKU ULIPOTUTOKA ILIKUWA SIKU YA MAJONZI MAKUBWA SANA KWETU , TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUPA UJASIRI MKUBWA. SISI TULIKUPENDA LAKINI MWENYEZI MUNGU ALIKUPENDA ZAIDI.
FAMILIA YOTE, WATOTO WAKO WOTE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI TUNAKUOMBEA MAPUMZIKO MEMA NA MWENYEZI MUNGU AIWEKE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YAKE PAMOJA NA NDUGU WOTE WALIOKWISHA TUTANGULIA MBELE ZA HAKI
AMIN.
WAKO MPENDWA MKEO,
ASHURA KASHEBA
LONDON

balosi mohamed maharage akisalimiana kwa furaha na freddy supreme ndala kasheba siku mwanamuziki huyu mahiri alipotumbuiza mabalozi waliokuwa wakikutana katika semina elekezi huko ngorongoro

kasheba akitumbuiza mabalozi ngorongoro

nilibahatika kusikiliza kazi za kasheba wakati akirekodi albamu yake ya mwisho ya 'yellow card' katika studio za makuti huko ilala shariff shamba takriban mwaka mmoja kabla hajatutoka. albamu hiyo, ambayo kwa kiasi kikubwa ilitabiri mauti yake, ilikuwa moto wa kuotea mbali kwani ilihusu yeye kuzushiwa kifo na kuja na neno 'yellow card' kwamba maradhi yaliyomkumba wakati huo na baadaye kupona yalikuwa kama kadi ya njano toka kwa jalali kwamba siku zake zilikuwa bado. aliwasema sana watu wanaozushia wenzao umauti.
unaweza kupitia picha na habari zake zilizopata kutundikwa kwenye globu hii ya jamii kwa
kubofya hapa vile vile tembelea
madarakanyerere.blogspot.com ambako mdau nambari wani wa butiama madaraka anamzungumzia hayati kasheba
RIP Maestro. Tunakukumbuka
ReplyDeletembona hakuna hiyo habari kwenye madarakanyerere.blogspot.com?
ReplyDeleteMwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahala pema peponi,Ameen.
ReplyDeleteIn God we trust.
Mjusi