Miriam Odemba akiwa anaonyesha mavazi ya kila siku (casual wear) katika jumba la duka la Robinson Mall.
Miriam Odemba akiwa amepozi baaada ya kumaliza maonyesho ya mavazi. Miriam amevaa gauni lilobuniwa na "Maua Mazuri" kwa kutumia khanga kutoka nchini Tanzania.
Miriam Odemba akiwa amepozi na mwenyeji wake Karla Henry wa Philippines.

Mrembo wa Miss Earth Tanzania 2008, Miriam Odemba ambaye ni mzoefu katika masuala ya uanamitindo ameanza mashindano ya Miss Earth nchini Phillipines ambapo ameweza kuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wa pale.
Hivi karibuni, Miriam aliungana na washiriki wenzake katika maonyesho ya mavazi yaliyofanyika katika jengo la duka la Robinson Mall. Miriam hivi sasa anatabiriwa na wataalam wengi kufanya vizuri katika mashindano hayo kutokana na kile walichosema ni mvuto wa sura, uwezo mkubwa wa kutawala jukwaa (catwalk) na kujiamini katika mahojiano na vyombo vya habari. "Tanzania imetoa mrembo ambaye ameonyesha umahiri mkubwa" aliandika Marco Ramirez ambaye ni mtaalam wa masuala ya urembo huko Philippines:

"Well, this one [Miriam Odemba] has surprised me so much. She is a kind of contestant that appears to be a great contender for the crown. Her charm is effortless and that what makes her my sentimental favorite for the crown. I don't want Miriam to be wasted here. Ever since, no black beauty has ever won the coveted title. Winfred did not win the title in 2002; Miss Bosnia and Herzegovina (the actual winner) relinquished her crown a few months after. Who knows Miriam might be the chosen one. With that super hot personality and style I dare say that she will earn the judges' nods."

Mashindano ya Miss Earth yatafikia kilele tarehe 9 November huko Manila, Phillipines ambapo warembo 93 watawania taji la Miss Earth na mataji mengine. Miss Earth pia ina mashindano mengine madogo yanayomwezesha mshiriki kujizolea umaarufu na zawadi ndogondogo kwa mfano kuwania taji la vazi la ufukweni, kipaji, nguo ya jioni nk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. rock girl.ur my girl i will always give u 200%.waonyeshe watu who r u dear.

    ReplyDelete
  2. jamani kaka michuzi mbona huyo mtaalam wa mambo ya urembo huko philipine amesema mpaka sasa hilo taji la miss earth halijawahi kuchukuliwa na mrembo mweusi wakati si ukweli.Miss Earth 2002 alitoka Kenya,anaitwa WINIFRED OMWAKWE.Ebu cheki tafadhali.Asante

    ReplyDelete
  3. Keep it up Miriam!!

    ReplyDelete
  4. Sijafuatilia kwa karibu sana masuala ya urembo mwaka huu, inamaana Miriam na wengine waligombea kinyang'anyiro hichi Tanzania na akaibuka mshindi kuiwakilisha nchi ama amefikaje kutuwalikisha huko?

    ReplyDelete
  5. yan annon wa 9.25 am
    sawa kbs kafikaje fikaje ukooooo??heeee aya mambo jamaniiiii???

    ReplyDelete
  6. Kaka michuzi,pole kwa comment yangu ya 9.44,ni kweli hakuna mrembo mweusi aliyechukua,huyo mkenya kumbe alivuliwa taji,now I know.

    ReplyDelete
  7. Go Miriam full suport,I saw the way you rock in your professional profile of U.S.A in www.blackmodels.wordpress.com nice work am proud of you african qeen

    ReplyDelete
  8. DADA UMEPENDAZA NA "ROHO YANGU IKOMIKONONI MWAKO" HALA HALA USIJE IDONDOSHA "IKAVYNJIKA"

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...