Pole sana kwa kazi Mh. balozi.
Naomba kupitia Blog yetu ya jamii nimtaarifu ndugu Theodora Lindasimba afike katika ofisi za Dawasco Kisutu ili aweze kuzichukua nyaraka (Documents) zake muhimu.
Aidha kama kuna mdau yeyote anayemfahamu ndugu Theodora Lindasimba aliyesoma Sekondari ya Makongo (1985) na kisha kujiunga shule ya sekondari Weruweru amtaarifu ya kuwa Documents zake muhimi alizopoteza anaweza kuzipata kwenye ofisi nilizotaja hapo juu.
Kama atafika mwenyewe ama atamtuma mtu kujamchukulia, tafadhali anatakiwa aje na vitambulisho halisi vinavyomtambulisha yeye binafsi ama mtu aliyemtuma, vingenevyo hataweza kupatiwa nyaraka hizo muhimu kwake. Naomba kuwasilisha.
Mdau Dar-es-salaam.
Kwanza nakupongeza Mheshimiwa Michuzi kwa kukubali mtandao huu wa jamii kutumika kwa shughuli za kijamii.Pili nampongeza mdau kwa moyo wake wa kiungwana wa kutafuta namna ya kumsaidia huyu ndugu yetu aliyepoteza nyaraka zake muhimu.Lakini mimi najiuliza je huyu mtu aliyepoteza atakutambuaje wewe unayetaka kumpatia nyaraka zake? Maana nijuavyo mimi kwenye ofisi zetu za kiswahili kama hujataja jina la mtu unayetaka kumuona hapo kwenye ofisi watu watakuangalia tu kama pilipili hoho.Ingekuwa vyema basi walau ungemtajia jina lako au hata namba ya ofisi(kama ipo)au chumba gani ili iwe rahisi kwake kukupata kiurahisi.Maana tatizo letu wabongo, wewe unataka kutoa msaada lakini wengine watataka "kuchukua advantage". Nawaomba wabongo tuwe na moyo hou wa kusaidiana tukiwa ndani ama hata nje ya nchi yetu.Hivyo ndivyo tulivyolelewa.Hongera mdau
ReplyDelete