Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na balozi wa Zimbabwe nchini Angola ambaye zamani alikuwa balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Chipo Zindonga kabla ya kikao chake na mabalozi wa nchi za Afrika nchini Namibia kwenye hoteli ya Safari Court jijini Windhoek
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akiongozwa na Meneja Mkuu wa Kiwanda cha kukata almasi cha NAMCOT DIAMONDS cha Windhoek, Bw. Kfir Teichman kukagua shughuli za ukataji almasi wakati alipotembelea kiwanda hicho akiwa katika ziara ya kikazi nchini Namibia


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. hii style ya kuweka mkono mfukoni wakati unasalimiana na watu ambayo mheshimiwa rais anayo sasa naona na mheshimiwa waziri mkuu anaiga. sio tabia nzuri jamani

    ReplyDelete
  2. MAZUNGUMZO KWENYE PICHA YA JUU KABISA:

    Mh Pinda: Kuna Bwana mmoja alikuwa anapiga piga picha sana itakuwa ulishamwona kwenye Sherehe mbalimbali pale Dar.
    Mh Zindonga: Ehee kafanya nini tena huyo Bwana?
    Mh Pinda: Naye kateuliwa kuwa balozi kama wewe
    Mh Zindonga: Kapelekwa Nchi gani?
    Mh Pinda: Zain
    Mh Zindonga:Zain ni nchi gani?
    Mh Pinda: Ni Kampuni ya Simu, alianza na ukuu wa Wilaya
    Mh Zindonga: Wilaya gani?
    Mh Pinda: Kuna Wilaya mpya tumeanzisha Njia ya kwenda Bagamoyo kabla hujafika Bunju

    ReplyDelete
  3. Sie TANCUT tumeiua bila sababbu za msingi na tuna madini zaidi ya aina 100 yote yanakatwa nje ya nchi.Aibu gani hii?Hebu viongozi wetu TAZAMENI!

    ReplyDelete
  4. Jamani,swali kwa wadau mliosoma Mlimani shule ya msingi (Chuo kikuu) miaka ya 90-2006: Hamuoni kama Mh.Pinda anafanana na mwalimu Nyamzaba?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...