Maelfu ya wakimbizi wa Burundi waomba kuwa raia wa Tanzania
Na Mwandishi Maalum, Urambo, Tabora
Na Mwandishi Maalum, Urambo, Tabora
FAMILIA 8,307 za wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya wakimbizi ya Ulyankulu, wilayani Urambo, Mkoani Tabora, wameomba uraia wa Tanzania, Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameambiwa leo, Ijumaa, Oktoba 24, 2008.
Akiwasilishiwa taarifa ya utendaji wa Serikali katika Wilaya ya Urambo katika siku ya pili ya ziara yake ya siku nane katika Mkoa wa Tabora mjini Urambo, Rais Kikwete ameambiwa kuwa familia hizo zina jumla ya wakimbizi 40,886.
Taarifa hiyo imesema kuwa baada ya baadhi ya wakimbizi kukubali kurejea nyumbani kwao Burundi, kiasi kubwa cha wakimbizi wameomba uraia wa Tanzania baada ya kuwa wamekaa nchini kwa miaka mingi kama wakimbizi.
Baada ya kuwa amejulishwa habari hizo, Rais Kikwete amesema kuwa ni vyema kuachia mchakato wa kuomba uraia kuendelea kwa kushughulikiwa na taasisi husika, na kuwa baada ya kuwa umekamilika Serikali itachukua uamuzi kuhusu wapi wataishi wakimbizi hao.
Hata hivyo, amesema kuwa wakimbizi hao hawataruhusiwa kukaa katika eneo hilo la Ulyankulu, na badala yake watahamishiwa katika sehemu mbali mbali nchini.
“Tuachia mchakato uendelee wa kuwapa uraia wa Tanzania kama wanazo sifa za kupata uraia huo. Lakini lazima kusema kuwa wakishakuwa wamekubaliwa kuwa raia wa Tanzania watasambazwa nchi nzima, kwa sababu hawaombi kuwa raia wa Ulyankulu, bali raia wa Tanzania,” amesema Rais Kikwete.
Ameongeza: “Wajue na wajulishwe kuwa wanaomba kuwa raia wa Tanzania, na siyo kubakia Ulankulu. Vinginevyo, wakiendelea kubakia katika eneo la sasa la ukimbizi wataendelea kuwa wakimbizi. Lakini kwanza tuangalie maombi yao na kuyachambua vizuri.”
Akizungumzia suala la mauaji ya albino kwenye kikao hicho, baada ya kuwa amepongezwa na wilaya kwa msimamo wa Serikali yake kuhusu mauaji hayo, Rais amesema kuwa ni ujinga kudhani kuwa ukikata na kupata kidole cha albino basi utaweza kupata utajiri.
“Sasa kama utajiri si wangeupata albino wenyewe kwa sababu wao wanacho kila kitu – wanayo mikono, wanazo nywele, wanavyo vidole, sasa kwa nini kama viungo hivyo vinaleta utajiri wasiwe matajiri wakubwa wa nchi yetu,” ameuliza kwa mshangao Rais Kikwete.
“Ni lazima watu wanaotaka kuwa matajiri wajue kuwa utajiri ni matokeo ya kufanya kazi kwa bidii, kwa maarifa na kwa nidhamu na siyo kuchuna ngozi ama kukata na kukimbia na viungo vya albino,” amesema Rais Kikwete.
Rais pia ameonyesha mshangao wake kwa baadhi ya watu na taasisi zinazoilaumu Serikali kutokana na mauaji ya albino.
"Kuilaumu Serikali kwa ukatili huu siyo jawabu. Hakuna mtu wa Serikali anayewashauri wauaji hao wa albino kuwafukuza wenzetu hawa na kuwakata viungo vya miili yao.
La msingi ni kwa taasisi wote, watu binafsi na Serikali, kushirikiana katika kutafuta jawabu la ujinga huu.”
Mengi aliyosema Mheshimiwa rais ni kweli lakini bado anakataa serikali yake kulaumiwa kwa hilo na huo ni Upumbavu kwa sababu kama serikali yake ingeunda Tume kuchunguza mauaji hayo hapo ndipo Taasisi na watu binafsi wangejitolea kutoa siri nzima ya mauaji hayo.
ReplyDeleteInakuwaje BBC wametuma mwakilishi wao kwa muda mfupi tu na wameweza kupata habari nyingi kuhusu mauaji hayo, Je Serikali Imechukua hatua gani kufanya uchunguzi kuhusu habari hizo kwani kuna mtu aliojiwa na akasema rafiki yake alishafanya na akawa tajiri na pia yule mwandishi alimuhoji Mganga ambaye alionyesha baadhi ya vitu ambavyo ni viungo vya albino na hapo SErikali ilichukua hatua gani?
Nadhani Rais anatakiwa kuwaambia wananchi Serikali inafanya nini kuhakikisha mauaji hayo hayatokei.
Ni kazi ya serikali kuhakikisha sheria zinafuatwa na sio swala la watu binafsi au Taasisi ambazo sio za Serikali kufuatilia maswala ya mauaji ya Albino.
Kama Serikali inashindwa kufanya kazi zake basi wabinafsishe mahakama na Polisi kwa watu binafsi na wao watafanya kazi kwa uhakika zaidi.
Kenge
Hapa JK nampa tano, kama hawa jamaa watapewa uraia lazima wasambazwe kwani wakiachwa Ulyankulu watatengeza kaburundi kao ndani ya Tanzania, lazima wajichanganye na watanzania wengine. Vinginevyo itakuwa mbegu mbaya nchini.
ReplyDeleteduh! uraia wa bongo pia lazima mtu uombe? tena m-burundi! kama washakaa sana bongo na wanaongea kiswahili cha Tabora basi hawa ni watanzania na hakuna haki yoyote ya kuwanyima. Hawa ni waafrika na wanatakiwa waishi popote wanapotaka hata hapo ulyankulu. Kwanza warundi wanaokimbilia Tanzania wengi i warundi wanaozungumza kiswahili huko burundi na ukirudi nyuma miaka 120 tuu hawa wote ni watanzania waliohamia burundi kwa kufundisha dini ya kiislamu, kupiga taarabu au kufanya biashara.
ReplyDeletemichuzi juu juu zaidi au sio mkuu wewe upo juuu sana
ReplyDelete(Nadhani unapenda sana comment kama hizo maana ukijaribu kua tofauti kidogo na maoni utakayo basi upost comment,labda ndio maana watoa comment wamepungua,kua fare kidogo na uache uoga maana watu wengi tunatoa comment zisizo za matusi wewe unazibania kisa zinaonesha kuikosoa sana serikali,basi usitoe mana ambayo utaona inaweza kuwashawishi watu kucomment kivingine..nb bana na hii mzee
mchangiaji wa tatu unashangaa kuwa uraia wa tanzania unaombwa? na kwa nini usiombwe? hivo unaidharau nchi yako kiasi hicho? sijui ulipo na wala ufanyalo lakini kaa ukijua tanzania ni nchi yako na ndio kwenu, ukitaka usitake, badili jina, uraia na hata rangi ya ngozi yako, lakini kwenu ni tanzania na utakuwa mtu dhaifu sana tena sana kama unadharau ulikotoka. eti uraia wa tanzania nao unaombwa! grow up.
ReplyDeleteWatu wa nchi hizi mbili Rwanda na Burundi inabidi tuwe waangalifu sana kabla ya kuwapa uraia, huwa hawaachi kukumbuka mambo ya kwao. Tusipoangalia tabia ya kuchukiana ya kwao italetwa kwetu. Kuna jamaa toka kule nilisoma naye shule ya msingi hadi sekondari lakini baada ya muda huo wote bado alirudi kwao kwa siri kupigana vita, sasa hivi yupo ktk serikali.
ReplyDeletewatanzania ikiwa raisi anazungumza haya yafuatyao chini inatisha sana.
ReplyDeleteserikali jukumu lake kuhakikisha amani ya ndani na nje inatendeka na siyo kuzungumza kama haya maneno yasiyokuwa ya maana mbona msafara wa raisi ulipopigwa na mawe huko mbeya mara wahusika wameshakamatwa kwavile raisi ndio MUNGU mtu na hajui kama wananch ndio wamemweka tatizo sisi watanzania hatujui kupima mambo ukiangalia raisi kikwete kwakweli mambo mengi yamemshinda tangu achukue wadhifa inasikitisha lakini huu ndio ukweli chukulia yafuatayo:
majambazi yanazidi kutanda na kuua.
Mafisadi ndio wenye kauli serikalini,
Maalbino mauaji kibao.
shida ya kazi na mishahara duni kulinganisha na maisha yalivyopanda kibao.
Sheria hazitekelezwe kwa mafisadi.
Kitu alichokiweza Raisi ni kula starehe za kutembea mikoani na sehemu zingine duniani hii hakika anastahili sifa.
haya soma haya maneno ya raisi wetu kiasi inanifanya nilie kwa uchungu na KUMUOMBA MUNGU awasaidie hawa maalbino inaanza hapa:
Rais pia ameonyesha mshangao wake kwa baadhi ya watu na taasisi zinazoilaumu Serikali kutokana na mauaji ya albino.
"Kuilaumu Serikali kwa ukatili huu siyo jawabu. Hakuna mtu wa Serikali anayewashauri wauaji hao wa albino kuwafukuza wenzetu hawa na kuwakata viungo vya miili yao.
La msingi ni kwa taasisi wote, watu binafsi na Serikali, kushirikiana katika kutafuta jawabu la ujinga huu.”
Nchi inaonekana imeendelea kama inafuata sheria zake kwa msimamo mmoja. Kila swali la jamii lazima huwa na jibu na bunge ndio kazi yake ya kutunga sheria, kupitisha sheria au kubadilisha sheria.
ReplyDeleteHuku Ulaya, mtu akiingia kwa haki, basi baada ya miaka kadhaa, hupewa uraia au katoka ulaya, afrika au china. Kama hajavunja sheria basi hamna sababu ya kutompa uraia.
Lakini Tanzania, bado wanasubiri Raisi aamue, kama vile hakuna bunge wala sheria za Uhamiaji. Wabunge wanapewa pesa nyingi lakini sioni wanalolifanya kuifanya Tanzania ije juu kiuchumi na kijamii.
Kama wadau wanavyosema hapo juu, kama hawakufunja sheria basi wapewe uraia kama wamekaa kwa muda mwingi na wanajua lugha na utamaduni wetu (Nchi zenye sifa za maendeleo, mtihani huu ni wa karatasi, ukipasi, unaenda kuapishwa kuwa raia na jaji na kupewa cheti chako cha uraia).
Irahisishe pia mambo ya sheria za kibiashara au kuwasaidia wananchi wapate haki zao haraka makortini. Watu wanasubiri miaka 10 kupata haki mpaka hivi leo.
Watu bado tunasubiri sheria kupitishwa ili turuhusiwe kuna na pasi mbili kihalali, sitegemei leo wala mwakani swali hili kupitishwa bungeni. Tunaambiwa bado wanakusanya maoni ya wananchi, wakati nchi nyingi duniani zimesharuhusu na wananchi wao wameweza kuisaidia uchumi wao kwa kupeleka dola bilioni 25 (Filipino), Dola Bilioni 20 (Mexico na India). India peke yake inapeleka bilioni 5 kutoka Saudi Arabia peke yake kila mwaka na kadhalika.
Je, sisi tutaamka lini waungwana?
(source: The Economist, March 10th 2006 issue, www.theeconomist.com).