Haloo haloo kaka michuzi na Geita hatuko nyuma kwenye maswala ya wanawake hii ni kitchen party ya mwenzentu Veronica Peter tukimwandaa kuingia ndani ya nyumba.
Mdau Geita

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mmependeza.

    Mafiga matatu hayo!Tunaambiwa maana yake si nzuri kabisa.Sijui nyie mlimfundaje huyo biharusi kuhusu hayo mafiga?

    ReplyDelete
  2. kwanza hongera na shukrani Bro Michuzi kwa habari nje na ndani ya Tanzania.wadau naomba niulize huyo pembeni kwa bibiarusi mtarajiwa sio Magereth Mushi wa GGM(HR)?kama ndiye naomba nipewe e mail yake au contact zake napenda nimsalimu sio kwa ubaya au kuchafuliana hewa..
    Sam- Arusha

    ReplyDelete
  3. YOTE TISA........HAYO MAFIGA YALIYOSAPOT HICHO CHUNGU NATUMAINI NI 3..................KUMRADHI WADAU, what is ze real meaning for that?

    ReplyDelete
  4. Hongera sana bi Vero, baada ya hongera dada napenda kukuusia nami ingawa sikupata fulsa huko geita ila kwa vile dunia ni kijiji kwa siku hizi basi mwenetu tukae jamvini hapa tuongee kidogo yakupasayo kusikiwa nikiwa kama dadako, ya kwamba naamini ulipata masomo ya jikoni kwa ufupi na uyafanyie kazi kwa vizuri, tusije sikia kauli kama zile za wiki ilopita mara hujui pika au ujeuri mtindo mmoja, iwe isiwe kuna neno linasema ukishikwa nawe shikamana, na pia wanasema mwanamke ni kujiongeza katika kila nyanja usikubali wenzako wakakupiku kwa vile ulimkubali mwenyewe huyo baba mkamate kwa kufanya maisha yenu yawe ya furah kila siku,achana na yale maneno ya takataka wanayokuwa wanarusharusha wanawake wengine wasio na hekima na kukudanganya, naamini wewe una dini na dini zote zinasisitiza matendo mema kwa waume mf. kwenye madrasa ya ndoa ya dini yangu inatufunza kuwa mwanamke aangalie mambo mnne kwa mumewe
    1. Uangalie macho yake:- kwa maana ya kumfanya akuangalie wewe zaidi kuliko kuangalia kwengine, hapo ujiongeze kwa kujiweka sawa na nadhifu kwenye mavazi kujiremba na kumfurahisha na akufanye kuwa m-bora.
    2. uangalie pua yake:- kwa kuweka mazingira safi kuanzia mwili wako mpaka nyumba yako sio mume anaingia ndani anakutana na kupiga teke chupa ya nyonyo ya mtoto au toys au neppy iliyokwisha tumika au uchafu wowote.
    3. Uangalie masikio yake:- usimsikizishe maneno ya karaha au ya kumfanya asononeke iwe kwa mali au kwa madhaifu au kwa kutotoa siri iwe ya kitandani au ya mfukoni mwake.

    4. Uangalie tumbo lake:- kwa maana ya maakuli yaani jitahidi kuwa mbunifu iwe kwa mapishi ili apende mapishi yako, na awe na raha wakati anakula na kufurahi.

    Dada vero, nakumbuka usemi unasema nyimbo mbaya habembelezewi mwana, Nakutakia kila la kheri na fanaka katika maisha ya ndoa maana ni safari ndefu ila ukiwa unamaanisha utaipita safari hiyo kwa furaha na kuona yote unayaweza. ila ukiikataa hali kwa kutoridhika haraka na kukata tamaa haya mwaya! biblia inasema mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe. Narudia kuwa nakutakia maisha mema.

    ReplyDelete
  5. mmmmhhhhh mjomba misalo hapo juu sijui ni kweli chicken party au?

    ReplyDelete
  6. mmmmhhhh bwana misalo hapo juu umechesha kidogo,sio chicken party.

    ReplyDelete
  7. Wadau huu mimi naona kama ni ubaguzi wa jinsia. Iweze mwanamke anapoolewa anapewa jiko? Ina maanisha nini?

    ReplyDelete
  8. Chungun haiinjikwi kwa figa moja, hii ni story za zamani watu wa pwani walikuwa wanawafunda bibi arusi mtarajiwa, ni kwamba enzi hizo kabari sukari haijaingia sumu walikuwa wanaambiwa wasikae tu kumtegemea mmeo wao lazima wawe na mume wa pembeni kwani wanaume hawaaminiki anaweza kuuacha mara moja na ukaangaika bila ya mume mwingine kwa muda kwa vile hukuwa na wako wa kificho, basi ni bora ukawa nae ukiachika unaenda kwa wakificho wako mara moja. hii ilikuwa kweli enzi hizo kabla ya sumu hii iliyoingia, kwa sasa si vizuri na huyu mdudu aliyechafua sukari.

    ReplyDelete
  9. Misupu ebu turushie picha zaidi za hizi harusi kwenye ile web ya www.harusiyangu.com maana kule ndio tunaona mambo yote ya harusi

    ReplyDelete
  10. Hongera sana dada Vero umependeza sana ila ningependa kujua maana ya mafiga 3 tafadhari mwenye ujuzi anijuz pls nahitaji kujua.

    Mwanamke mpumavu hubomoanyumba yake kwa mikono yake mwenyewe bali mwanamke mjanja hujenga nyumba kwa mikono yake wenyewe (Mithai), mwanamke simama ktk sehemu yako kama mwanamke na asikudanganye mtu kwa maneno ya kusema maisha ya ndoa ni magumu si kweli na katu usiifananishe ndoa yako na ndoa ya mtu mwinginekila kwani kila mtu na mtazamo wake ijenge ndoa yako kwa mikono yako mwenyewe. Mungu akubariki.

    ReplyDelete
  11. Mafiga 3 kwa Geita ni kama ifuatavyo
    1-Jitahidi uwe na mume kutoka mgodini
    2-mume kutoka serekalini
    3-mume mfanyabiashara au kiongozi wa dini
    Ndivyo wanavyondanganya bi mtarajiwa.Hawamtakii mema mtarajiwa hao

    ReplyDelete
  12. is it chicken or kitchen...............

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...