Huduma ya One Network Yatambulika Pamoja na Kubadilisha Jina Kutoka Celtel Kwenda Zain katika nchi 14 Africa.
Zain Group imeshinda tuzo ya Kampeni Bora Ya Afrika ya Mwaka ( Best Pan African Initiative Campaign of the Year Award) ambayo inatambua huduma ya kwanza duniani inayoondoa mipaka ya One Network ambayo kwa sasa inaunganisha nchi 16. Zain pia imeshinda tuzo ya Kampeni Bora ya Masoko ya Mwaka kwa kuzindua chapa ya Zain kwa siku moja katika nchi 14 kwa mkupuo pamoja na kuunganisha vituo vyote kupitia satellite na kuweka rekodi katika Bara la Afrika.
Tuzo hizo zilitolewa hivi karibuni Mjini Cape Town, Afrika Kusini katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Cape Town mbele ya watu 3, 500 kutoka mataifa 72 na viongozi 221 kutika makampuni mbali mbali ya ya simu ambao walikuwa wanahudhuria mkutano uliondaliwa na kampuni ya Kimataifa ya Ushauri wa Masoko na Mawasiliano ya Informa Telecoms & Media.
Mgeni rasmi alikuwa François Pienaar, Nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya Springboks ya Raga kuanzia Juni 26 1993 hadi Agosti 10, 1996.
Chris Gabriel, Ofisa Mtendaji Mkuu za Zain Africa alisema baada ya kupokea Tuzo kwamba “ Ari mpya na chapa mpya ya Zain imethibitishwa na wateja wa zamani wa Zain pamoja na wateja wapya wanaojiunga na mtandao wa Zain kila kukicha katika nchi zote baada ya kubadilisha chapa. Huduma ya One Network inawavutia wateja wengi kwenye mtandao wa Zain kutokana na manaufaa yake na huduma hii inachochea harakati nyingi za kiuchumi katika mipaka na kuwawezesha wateja kuendelea kuwasiliana na ndugu na jamaa zao kwa bei nafuu,””
Zain ilishinda tuzo hizo zinazoheshimika katika mkutano huu.
Tuzo hizo hutambua na kuzawadia juhudi bora sana katika mawasiliano barani Afrika.
Wakitoa tamko majaji waliipongeza Zain kwa kuelewa soko la Afrika inapokuja kwenye suala la mawasiliano yanayogusa wateja. ‘’Zain imedhihirisha manufaa yanayooneka ambayo yanagusa soko la Afrika, na imefanya mashirika na wateja wahusike katika ubia kati ya nchi na nchi, ikibadilishana uzooefu na ujuzi miongoni mwa menejimenti yake,”” walisema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...