makamu wa rais dk. mohamed ali shein na mkewe mama mwanamema shein wakipiga stori na mzee mizengo pinda na mama pinda walipowatembelea nyumbani kwao mpanda. dk. shein yuko katika ziara ya kikazi mkoani rukwa kukagua maendeleo na kuongea na wananchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Kweli wajameni cheo raha, hata mimi mbeba box wa majuu sina sofa kama nizionazo kwenye hii picha..IC

    ReplyDelete
  2. Kweli nimeamini Pinda sio Fisadi. We angalia nyumba ya wazazi ni sawa na nyumba za kawaida kijijini, angalia kwenye madilisha finishing. Ila kwa sababu uwezo anao kidogo awajengee angalau nyumba kidogo na hadhi ya wazazi wa Waziri mkuu. Sio kwamba tutamwona kafanya vibaya ni mojawapo ya shukrani kwa malezi mazuri waliyompa

    ReplyDelete
  3. Duh, kweli Pita noma, sakafu haijapigwa hata zulia!

    ReplyDelete
  4. dah,babu kochi linamlevya hilo kudadeki lazima asinzie tu,

    ReplyDelete
  5. Hapo wazee wamejitahidi, hongera sana. sofa kali utafikiri sio kijijini. Big up Waziri mkubwa.

    ReplyDelete
  6. Hivi wazazi wa Sokoine au kaburi lake lishawai kutembelewa, au wazazi wa Kawawa au Warioba washawai kutembelewa?

    ReplyDelete
  7. Anon 12:42 PM mbona mshamba wewe Zuria na joto la Afrika na Vumbi wapi na wapi najua nyumba wengine wanaweka lakini sio sahihi pili elewa hiyo nyumba ni kijijini hakuna AC sasa hilo vumbi wanapata wapi Hoover ebooooooooo

    ReplyDelete
  8. yani hilo sofa limewekwa juzi baada ya kupata uwaziri mkubwa, na hiyo nyumba haikuwa hata na ripu, ila maskini ya mungu ndo hivyo tena sasa hivi wanaona tbc yao vizuriii na maji ya baridi kwa pembeni kuna kafriji au wadau hamjaona.

    ReplyDelete
  9. mh!!!apo sio ofisi za chama kijijini tu??
    wee ngoja aonyeshe shamba lake na gorofa atalojenga km si kajenga,sii vibaya wala wizi mana nafasi na pesa yake vyamruhusu

    ReplyDelete
  10. Hivi ndivyo au maigizo?Kila kitu seems to be two days old with exception of walls,floor and window!

    ReplyDelete
  11. Hivi ndivyo au maigizo?Kila kitu seems to be two days old with exception of walls,floor and window!

    ReplyDelete
  12. Nakupongeza Peter Nyayanzwa Pinda kwa kuwaheshimu Baba yako na Mama yako hata katika utumishi wako wa umma.Si watu wengi wenye bahati hiyo ya kuwaenzi wazazi wao kijijini.Katika zile amri kumi za Musa hakika hii umeitkeleza vizuri, wazazi wako watapokubariki na watanzania tunabarikiwa vilevile

    ReplyDelete
  13. tv, fridge, leather sofas, mambo siyo mabaya.

    hayo yote yapo ndani ya uwezo wa waziri mkuu wa tanzania.

    ReplyDelete
  14. HAKIKA MUNGU NDIYE ANAYEJUA HALI HALISI YA WAZIRI KAMA KACHOTA AU LA MAANA KUNA WATU WAJANJA MAANA WANAJUA DUNIA WATU WAMEAMKA UNAWEZA KUKUTA PESA ZAKE ZIKO DAR KWENYE MAJUMBA.

    KUNA JAMAA YANGU KAJALIWA MALI KIBAO LAKINI ANAKAA KWENYE NYUMBA YA KUKODI UMKIMUONA UNAWEZA UKAMSADIA KUMBE NI BILIONAIRE WA SHILLINGS UKWELI NI MUNGU NDIYE ANAYEUJUA.

    ReplyDelete
  15. Akiwajengea au kuweka vitu vya thamani mtamwita fisadi asipoweka kitu duh kajisahau.

    Watazania ufisadi upo kwenye damu wote wanaolalamikia hawa mafisadi ni kwa vile hawakupata nafasi ya kupata hivyo vyeo. la sivyo nao wote wangekua hivyo hivyo.

    Inabidi tuoshwe kwa gharika

    ReplyDelete
  16. Hii zuga tuu. Picha hii imewakwa kumsafisha mheshimiwa. kama yuko transparent kihivii atuonyeshe account zake zote.!! wote tunawajua wazazi wa kijijini hawataki makuu.

    ReplyDelete
  17. Ehee hiyo TV mbona ni zile feki za Kichina?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...