Kaka Michuzi, Habari za Masiku, Nimepotea lakini Sijatoweka, Mara hii naibukia kijijini Nyawilimilwa wilayani Geita, Mkoani Mwanza kuwaunga mkono Majirani wa mgodi wetu wa Geita Gold Mine katika harakati za kuboresha miundombinu ya elimu kwa jamii yetu, Japokuwa walimu walikuwa wamekwa “Straiki” viongozi wa kijiji walikuwepo na wanafunzi walinipa kampani.



Simon ShayoCommunity & Sustainable Development Superintendent

AngloGold Ashanti - Geita Gold Mine

P. O. Box 532, Geita, Mwanza, Tanzania.

Office: +255 28 2520500, Ext. 1880 Fax: +255 28 2520502Cell: +255 784 580 308

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Simon Shayo kumbe uko Geita Gold Mine? haya kazi njema mkuu

    ReplyDelete
  2. Usipolipa kodi ya dhahabu ni rahisi kutoa vijisenti shuleni.
    Hivi sakata la ng'ombe wa wanakijiji wanaokufa kwa kunywa maji yaliyochanganyika na maji ya mgodi wenu limeisha vipi lakini? Au wananchi wasiwe na wasiwasi wa jitihada zao za kujitegemea kwa ufugaji, mtawapa misaada?

    ReplyDelete
  3. Hee Babu shikamoo....
    Naona uko kwenye BOT ya madini best... I cant u...
    Poa sie tupo tu huku na Bibi yetu wewe endelea kupiga mzigo babu..
    Honoratha(Dotho)Ernest.

    ReplyDelete
  4. Honourable ( honoratha ) uko wapi siku hizi ?? tuwasiliane
    vicki
    akitoti@yahoo.com

    ReplyDelete
  5. Anony wa 7.15 hulijui unaloongea. Nafikiri wewe ni mmoja wa wale ambao wako busy kuongea yale unayoyadaka kwa wenzio wakiongea au kwa kusoma kwenye magazeti ya udaku bila kufanya uchunguzi (research). Kwenye dunia ya leo "no research no right to speak". Kwenye maendeleo ya jamii, mining comapnies zinafanya mambo makubwa kuliko ambavyo serikali yetu ingeweza kufanya kwa kipindi cha miaka 100 ijayo. Nakushauri ujiunge na Management Forum pale British Council na unaweza kupata opportunity ya kudiscuss na watu wanaochambua kuhusu mchango wa sector mbalimbali (ikiwa ni pamoja na ya madini) katika uchumi wa nchi. Naomba usione sifa tu kupata wenzio matope. Hakuna mtu anayefanya mabaya au mema tu - You have to strike a balance everytime you want to discuss such a sensitive issue.

    ReplyDelete
  6. He umepata kazi ulikaa bila kazi muda mrefu mpaka nikaogopa. Hongera, Mungu akutangulie. Wasalimie matwins

    ReplyDelete
  7. Kudos Simon. Keep up the good work.

    ReplyDelete
  8. Hii tabia mbaya sana. Huwezi kuwa na mgodi mkubwa namna hiyo hapo Geita na shule ya msingi iliyo jirani ikawa mbaya na chafu hivyo.
    Jaribu kuwambia hao jamaa wa mgodi wavunje hiyo shule ya msingi na kujenga kubwa mpya. Yenye hadhi sawa na ardhi ya hao watoto wanaoitumia kupata mabilioni ya dola zao.
    Pia wambieni wajenge shule ya sekondari mpya jirani na maeneo hao. Na sio kupiga picha na watoto wa kisukuma huku ukiwa umewapa shilingi laki tano tu, amabza hata hazijengi vyo viwili vya shule.
    Oneni aibu nyinyi waTZ kwa kutumiwa na wazungu wa mgodi hivyo.

    ReplyDelete
  9. jamani hii tabia ni mimi tu ndo ninaiona au hata nyinyi mnaiona.
    katika nchi za wenzetu huwezi tumia email ya kazi kwa shuguli za kuwasiliana na watu wa blog, ku-chart etc.
    Ninaona TZ, watu wengi sana wanaofanya kazi katika haya makampuni ya nje wanatumia sana email address za kazini kwao katika kututumia mambo ambao hayatakiwi kufanywa katika saa za kazi.
    Kama hii ilikuwa na uhusiano wa kikazi basi ingeenda intranet na ikawa ya kwao watu wa geita gold mine.Kuileta katika blog ni makosa makubwa sana. Tofauti ya mambo ya Zain huwa yanaonyeshwa tu na huwa hazina email address za akina Kelvin, njuju, kavishe etc.
    Kuna wakati fulani email address za BOT zilikuwa ziko wazi katika blog na hiyo ni makosa makubwa sana.
    Ndugu Simon Shayo wa geita gold mine jifunze matumizi ya vifaa vya kazi kama email na compyuta zao sio jambo zuri wakati wa kazi.
    Suala la kuonyesha cheo chako ka kutumia blog halifai.Ni hali ya kuonyesha uchovu wa exposure na ujinga wa kiakili.

    ReplyDelete
  10. naanza kwa KUNUKUU STATEMENT HII "Honourable ( honoratha ) uko wapi siku hizi?" WEWE unamtaka wanini? KAMA wewe ni mhimu kwake mgekuwa nawasiliana acheni mambo hayo ukiona jina tuuuuu, unataka kuwasiliana na mtu angelikuwa men ungetafuta email yake? TAFAKA CHUKUA HATUA, HAKI SALAMA

    ReplyDelete
  11. Jamaa alikaa bila kazi siku nyingi sana kama alivyosema mchangiaji hapo juu. Hapo anaonyesha washkaji zake kwamba amepata kazi. Mwacheni awape na email ya kazini.

    Saimon acha ushamba, wenzako wana kazi kubwa lakini hawajitambi kama wewe. Sasa wewe kupata hako kakazi ndo unajionyesha kwenye blog, si tabia nzuri. Masters umemaliza lakini?

    ReplyDelete
  12. Jamani wanadamu kweli kazi ipo!!!

    Yaani wasipokuona unaamka asubuhi kwenda job basi wewe uko juu ya mawe . yaani Simon umeecha mapesa yote yale ya consultancies umeenda mgodini? ndo maana siku hizi sikuoni ukija kuchukua cheque kule mahali rafiki ok big up endelea kusaidia jamii . waache waliogizani wabaki hivyo hivyo sisi twaendelea kuzitafuna bila ofisi!!!!!!!

    ReplyDelete
  13. eeh masters kamaliza siku nyingi, tena sio ya UDSm, kamaliza Uingereza chuo babu kubwa. mwacheni Simon, maisha yake super, consultations bado anazo kibao, na bado anapublish makala kwa kwenda mbele.
    Big up Simon

    ReplyDelete
  14. naanza kwa KUNUKUU STATEMENT HII "Honourable ( honoratha ) uko wapi siku hizi?" WEWE unamtaka wanini? KAMA wewe ni mhimu kwake mgekuwa nawasiliana acheni mambo hayo ukiona jina tuuuuu, unataka kuwasiliana na mtu angelikuwa men ungetafuta email yake? TAFAKA CHUKUA HATUA, HAKI SALAMA

    Hivi we anony unamatatizo gani?? hujaona watu wanatafutana baada ya kupoteana miaka mingi, acha ushamba, mshamba mkubwa wewe na mdogo wa fikra awe mwanaume au mwanamke wote tunaweza kuwatafuta, ndio maana hata michuzi anawekaga misaada kwenye tutaz ya watu waliopoteana, mshamba wewe eti haki salama nyoooooooooooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...