Kiasi cha Sh bilioni 11.7 kimetosha kumtoa nje kwa dhamana mtuhumiwa anayedaiwa kuwa kinara wa ufisadi Jeetu Patel (kulia) na wenzake watatu.

Kiasi hicho ni kutokana na wizi wa Sh bilioni 22.7 anazodaiwa mtuhumiwa huyo na wenzake hao kuiibia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutoka katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kwa kutumia kampuni nne.

Jeetu na wenzake katika kesi zote katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wamekuwa wanawasilisha hati moja yenye kiasi wanachotakiwa kudhaminiwa washitakiwa wote kama ilivyoamuriwa na mahakama.

Jeetu ambaye jina lake kamili ni Jayantkumar Chandubahi Patel katika kesi hizo anashitakiwa kwa pamoja na Devendra Patel, Amit Nandy na Ketan Chohan.

Hati hizo ambazo zimewasilishwa mahakamani hapo zimethibitishwa na wakaguzi wa serikali ambao wamethibitisha kuwa na thamani ya kiasi hicho kwa kila kesi.


Leo washitakiwa hao walikamilisha taratibu za dhamana katika kesi iliyoko mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi Euphemia Mingi. Kwenye kesi hiyo, Jeetu, Nandy na Patel walidhaminiwa baada ya kutoa hati ya mali ya thamani ya Sh bilioni 5.4.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kesi imeshaisha hiyo. Hosea anaweweseka tu. Njii hii bana. Kuna baniani na wezake tu!

    ReplyDelete
  2. Huyo jeetu mwenyewe unaweza kusema teja,,duh

    ReplyDelete
  3. Sheikh Michuzi vipi mjasiriamali Johnso Lukaza Make kuna post yako mjo ulimpamba sana ukataka vijana wakitanzania waige mfano wake. Ati yuko kwenye real estate kumbe pesa yote ya wizi. Haya rudia tena sifa zako unazotoa bila kuchunguza.

    ReplyDelete
  4. jamani hawa wahindi wanaonewa hivi pesa zitatoka bila wakubwa kujua aibu tupu sijui civil rights imepotelea wapi.

    ReplyDelete
  5. HII DANGANYA TOTO TU MCHEZO NDO USHAISHA HAPO

    ReplyDelete
  6. End of story!!!!!!!!!!!!! jamani huu mchezo si mu uhamishie kwenye kada na cd ili watu waone mzima kuliko kuwaachia watu wa magazeti tu wauelezee. tulijuwa hapa ni kaole tu

    ReplyDelete
  7. Aliingia gerezani kweli huyu jamaa?
    Hapa kama tunaangalia zeComedy tu.

    ReplyDelete
  8. Tatizo la Watanzania tunapenda sana kusifia watu wenye vijisenti na kujigongagonga kwao kwa saaana! Wenzetu nje mfanyabiashara anajulikana wazi anafanya biashara gani. Huku utasikia magazeti yanampamba mtu ati MFANYABIASHARA MASHUHURI lakini anafanya biashara gani...'wizii... wiziii mkubwa..'- kajisemea Masanja wa Orijino Komedi

    ReplyDelete
  9. Tusubiri hicho kifungo cha nje na kesi vitakavyokwenda kabla hatuja-judge

    ReplyDelete
  10. Lukaza na nduguye wako free kwa dhamana,mama komu yuko free na yule mama mwingine sijui naibu katibu au nani wako free wooote kwa mali zao za nusu ya thamani ya vijisenti waloopoa BOT, mpo hapoooo na kesi imekwisha no ushahidi na hakimu kalamba dume teh teh hahahaaaa,,,awa watu hawatakiwi kufungwa lupango yan haina maana yoyote mana mihela bado watatumia ndugu zao adi vizazi bora wapewe kazi za community kwa idadi ya vijisent wavoopoa watengeneze nchi,,wakifungwa hasara kodi je??
    YANI ZINGA LA CARTOON TOM &JERRY

    ReplyDelete
  11. Naona hii sheria ya dhamana haimpi haki yule ambaye hajaiba. Kwa nchi masikini kama Tanzania, kima cha chini ni laki mbili tatu kwa mwezi, hii dhamana imeshamwadhibu mtuhumiwa hata kabla ya sheria kufanya kazi yake. Yule ambaye hana fedha ataoza bila ya kuwa na dhamana ambayo anaweza kutoa kutokana na uwezo wake.

    Serikali inataka kuwaonyesha IMF na wenzake wanaotupa misaada kuwa iko mbele katika vita vya wizi wa mali ya umma lakini hapa haki hamna kwa yule aliyeburuzwa mahakamani. Mbele ya sheria, hata wakishinda, itakuwa vigumu serikali kuridisha fedha kwa vyoyote. Wananchi wengi waliowahi kwenda mahakamani kushitaki au kushitakiwa wanajua kuwa hapa ni dhuluma tu katika picha hii. Pesa haiwezi kuibiwa benki kuu ya Tanzania bila ya mkubwa kujua.

    ReplyDelete
  12. Anon uliyesema bila benki kuu kujuwa ni kweli haiwezekani, semak ina Bilal si kafa na mwenzake sijui kakimbilia wapi hii kesi bwana haiendi kokote itaishia juu juu tu hizi pesa za dhaman ndio kama zinazorudishwa pesa za dhamana zinaenda wapi? kama si deal tena hapo wote wezi washitakiwa na wahukumu kudadadeki wanasema orijino komedi sawa na bajaji zinaletwa kwajili ya vilema wanapewa wanaojiweza kufanya tax. kazi kwlei kweli.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...