Mgomo wa walimu wa shule za umma uliokuwa umepangwa kufanyika kuanzia jana nchini kote, haukutekelezeka kama chama chao kilivyokusudia kutokana na baadhi ya walimu kuendelea na kazi.
Katika mikoa mingi nchini, uchunguzi umeibaini kuwa walimu wengi waliingia madarasani na kufundisha, ingawa kwa mikoa michache wengine hawakufanya hivyo na kubaki nje ya madarasa au wanafunzi kuamuriwa kurejea nyumbani.
Mikoa ambayo walimu walitekeleza mgomo huo ni pamoja na Mara, Kigoma na baadhi ya sehemu za Mkoa wa Tabora. Kwa Dar es Salaam, baadhi ya walimu walifundisha kama kawaida na wengine walikataa kuingia madarasani ingawa walikuwa wakirandaranda nje ya maeneo ya shule zao.
Lakini kwa mikoa mingine, walimu wengi walipuuza agizo la Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, la kuwataka kugoma jana, ili kuishinikiza serikali kulipa madai yao, licha ya kwamba imekwisha kupeleka fedha hizo katika halmashauri zote nchini kuanzia Jumamosi iliyopita.
Tayari Wizara ya Fedha na Uchumi imepeleka zaidi ya Sh bilioni 10 kwa halmashauri 132 nchini ili kulipia malimbikizo hayo ya madeni ya walimu kupitia Benki ya Makabwela, NMB, na jana baadhi ya mikoa imeanza kuwalipa walimu.
kwa habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Inaonyesha jinsi tusivyo na umoja. Hao walioenda shuleni hebu watuambie kweli wao wanategemea mshaara wa ualimu kula au wana yao

    We need unity.....wenzenu siku hizi kila kitu ni YES WE CAN wao sijui slogan ao niaje. Walivyoonda tu serikali imewataka waende shuleni basi wakanywea....that is toooooooo sad.

    ReplyDelete
  2. WEWE KIBARAKA ULITUMWA KUWAKATISHA TAMAA WADAI HAKI TUPE TAKWIMU YA IDADI YOTE YA WALIMU NCHINI, IDADI YA WALIOSHIRIKI DHIDI YA WALIOKATAA KUSHIRIKI, HAPO TUTAKUELEWA. WAPO VIBARAKA WENGINE WALIOANDIKA KWEYE MAGAZETI YA JUMATATU WAKIDAI KUWA WALIMU WAMEANZA KULIPWA WAKATI HIZO PESA ZILIKUWA HAZIJAFIKA MIKOANI. MAFANIKIO YA MGOMO HUO NI PALE WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI DAR WALIPOSHIKI MAANDAMANO KWENDA KWA MKUU WA MKOA NA KUMPA UJUMBE KUWA WALIMU WALIPWE, SASA IWEJE WEWE MTU MZIMA AKILI ZAKO ZIWE NDANI YA MAJI? KWANI MGOMO WA WANAHABARI WALISHIRIKI WANAHABARI WOTE? WAPO VIBARAKA WALIOKATAA KWA MADAI KUWA WALIOANDAMANA NI WAPINZANI.MBONA ULIFANIKIWA KWA KUFIKISHA UJUMBE.KAZANA TUU KUMFURAHISHA BWANA LAKINI MALIPO NI LAZIMA YATAFANYIKA TUU.

    ReplyDelete
  3. Kidogo natoka katika mjadala huu, naomba kukumbusha ule mjadala wa zanzibar sio nchi, huu ni mfano mwengine, umoja wa walimu nchini tanzania hauhusu zanzibar, kwa maana nyengine haukuvuka bahari! kwa ufupi hata kama walimu wote wangeligoma basi zanzibar wasingeligoma kwa sababu mbili moja mishahara yao hailipwi na serikali ya tanzania, ya pili umoja wa walimu hautambuliki zanzibar (au niseme nchini zanzibar)

    ReplyDelete
  4. Usidanganyike na baadhi ya walimu kuwepo mashuleni!Ukadhani mgomo wao eti umedoda.Kwenye suala hili la malipo ya haki zao walimu wapo pamoja na hakuna atakaye watenganisha kwa kuwatisha au kuwarubuni.Teachers have always been smart people all their life!Ndiyo maana wakaitwa Waalimu.Hivi kweli unaweza kumlazimisha Mwalimu afundishe darasani kama Hataki?Forget it.Sasa wanao jidanganya kwamba mwalimu akienda shule basi automatically atafundisha watoto darasani huyo kajidanganya,awe Waziri au babu yake waziri!Mwalimu anaweza kuingia darasani akapiga stori weeeee mpaka muda wa kipindi ukaisha.Utajuaje?Tusicheze na walimu hata siku moja.Hadi hapo walimu wote watakapo lipwa haki zao ndipo muafaka utakapo patikana.Lakini tabia iliyozuka ya kuanza kuwatisha walimu oooh mtafikishwa mahakamani,oooh mtafungwa,oooooh mtafukuzwa kazi,,,na maupumbavu kibao,ni sawasawa na kumwaga petroli katika moto,ukidhani utazimika!Nilimsikia waziri leo asubuhi kupitia Tv channel mojawapo akijifariji kwamba ooh mgomo haukufanikiwa,kwasababu walimu wengi tu wamekaidi wito wa viongozi wao wa chama cha walimu na wameamua kwenda shuleni!Hiyo ni furaha ya mwendawazimu baada ya kuliona jalala!

    ReplyDelete
  5. Hiki kichwa cha habari chenyewe hakionyeshi upendo kwa walimu hawa wanafundisha watoto wetu.

    Walimu wa Dar-es-salaam ni wabinafsi na hawana upeo wa akili kwa kushindwa kujua madhara ya wao kutokugoma kinyume na matakwa ya viongozi wa vyama vyao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...