RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mwandishi wa habari na vitabu maarufu nchini, Ben Mtobwa, aliyefariki dunia Jumapili iliyopita, Novemba 9, 2008, mjini Dar Es Salaam.

Rais amemwelezea marehemu kama mwanataaluma mzalendo ambaye aliitumia kalamu yake kwa busara na kwa ajili ya kuleta maelewano ndani ya jamii ya Tanzania.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete ameieleza familia hiyo: “Naungana nanyi wote katika wakati huu mgumu na wa majonzi makubwa mliyonayo kwa msiba huo mkubwa uliowapata. Tunaelewa machungu mliyonayo”

Amesisitiza Rais Kikwete katika salamu hizo za rambirambi: “Nimemjua marehemu Mtobwa kwa miaka mingi katika ujenzi wa taifa letu, hususan katika masuala yaliyohusu utaalamu wake wa masuala ya habari na uandishi.”

“Marehemu Mtobwa alikuwa mwanataaluma mzalendo, aliyetumia kalamu yake kwa busara na kwa nia ya kuleta maelewano ndani ya jamii yetu. Alijali maadili ya taaluma yake na kutimiza vyema wajibu wake katika jamii kwa mujibu wa maadili hayo.”

Amemalizia Rais Kikwete: “Naungana nanyi wote katika kuomboleza msiba huu mkubwa. Kwa pamoja tumshukuru Mungu kwa kumwezesha Ndugu Mtobwa kutoa mchango wake kwa taifa letu.”

Marehemu Mtobwa anatarajiwa kuzikwa leo kwenye shamba lake Bunju A mjini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Micu hulali wewe!?! Hii umei-post saa tisa kamili night kwa time za huku na huko ni around saa tano usiku! Utaachika aisee!

    ReplyDelete
  2. BEN MTOBWA WENGINE HAWAMJUWI SAWASAWA, TOA PROFILE YAKE, SIYO JUU JUU TU.

    ReplyDelete
  3. katika uandishi wa riwaya, wachache walikuwa wanakufikia. Ustarehe Katika Amani, Ben. R. Mtobwa.

    ReplyDelete
  4. wadau mnaokumbuka tukumbusheni kazi alizoandika Mtobwa.
    hamad

    ReplyDelete
  5. Mungu ampumzishe pema Ben Mtobwa, Amina.
    Wadau nikumbusheni, ni marehemu aliyekuwa mwandishi wa riwaya za Joram Kiango au? Manake Kiango alikuwa anachuana vikali na Willy Gamba.

    ReplyDelete
  6. Anony wa 8:47 umeatia, marehemu alikuwa wmandishi wa riwaya za Joram Kiango. Niliipenda sana tutarudi na roho zetu. Marehemu alikuwa mahiri katika kuandika riwaya zinazihusiana na ujasusi kama "Roho ya Paka" na "Salamu Kutoka Kuzimu".

    Pia alikuwa mwandishi wa riwaya zinazozungumzia watu wa kawaida wanaohangaika na maisha mjini, mfano "Dar Es Salaam Usiku". Riwaya yake iitwayo "Zawadi ya Ushindi" inayohusu maisha ya kijana Mtanzania kwa jina la Sikamona aliyejitolea kupigana vita dhidi ya Amini. Baada ya kurudi kutoka vitani, mchumba wake Rukia akajitolea kuwa zawadi yake ya ushindi, japokuwa Sikamona 'Sika' alikuwa kajeruhiwa vitani na uso wake umeharabika vibaya vibaya hajitamani; nusura ajiue. "Zawadi ya Ushindi" ilianza kutumika kama sehemu ya ufundishaji wa fasihi andishi katika somo la Kiswahili, na ilikuwa inatumika katika kujibia mtihani wa taifa wa kidato cha 4 kuanzia mwaka 1997. Hii ilimpa marehemu umaarufu na heshima zaidi sio katika nyanja za uandishi wa kuburudisha tu, bali pia katika elimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...