TOT Plus taarabu kumsindikiza Dogo Mfaume
Na Mwandishi wetu, Bagamoyo
KUNDI zima la Tanzania One Theatre (TOT PLus Taarab) watamsindikiza msanii chipukizi anayekuja kwa kasi Dogo Mfaume ambaye atazindua albamu yake ya 'Kazi ya Dukani' mjini Bagamoyo siku ya jumamosi hii katika ukumbi wa Saadan Club.
Akizungumza na Dar Leo katibu mipango wa TOT, Gasper Tumaini amesema kuwa wamekubali kumsapoti Dogo Mfaume kutokana na kazi yake nzuri ambayo ipo katika albamu yake mpya ya Kazi ya Dukani ambayo inakuja kwa kasi ya ajabu.
Amesema kuwa katika onyesho hilo ambalo watashirikiana naye kwa upande wa muziki wa taarabu chini ya malkia wa mipasho Afrika ya mashariki na kati Khadija Kapa ambaye naye atatambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya za zamani.
"Unajua onyesho hilo litakuwa ni zuri na la aina yake kwani Dogo Mfaume ataitambulisha albamu yake ya Kazi ya Dukani na Khadija Kopa naye atambulisha nyimbo zake mbili mpya kwa wakazi wa Bagamoyo" amesema Tumaini ambaye hakupenda kutaja nyimbo za Kopa.
Amesema kuwa onyesho hilo ambalo litafanykika katika ukumbi wao wa nyumbani wa Saadan Club litaanza saa 2 usiku na wapenzi wao 20 wa kwanza wataingia bure na kuweza kuondoka na albamu ya Dogo Mfaume.
Mratibu wa onyesho hilo, Kuruthum Hadji amesema kuwa onyesho hilo litapambwa na maonyesho mengine ya utangulizi ya ngoma za kiasili kutoka katika vikundi vingi vya mjini Bagamoyo ili kuweza kumsapoti Dogo Mfaume ambaye sasa anatikisa na albamu yake mpya ya Kazi ya Dukani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...