LINO INTERNATIONAL AGENCY LIMITED
P.O. BOX. 53069
P.O. BOX. 53069
DAR ES SALAAM,
TELEFAX :+255 22 2120201,
Azikiwe Street,
Azikiwe Street,
4th Floor,
Mavuno House,
MOBILE: +255 753 764156,
PRESS RELEASE
11 November 2008
YAH: SHEREHE YA KUMUAGA MISS TANZANIA 2008 IJUMAA TAREHE 14 NOVEMBA 2008
Mrembeo wa Taifa, Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim ataagwa rasmi siku ya Ijumaa tarehe 14 Novemba 2008 katika viwanja vya ofisi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania, [T.I.C.]
Mgeni rasmi katika sherehe hiyo anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Mheshimiwa Laurence Marshal.
Katika sherehe hizo Mheshimiwa Waziri atamkabidhi Bendera ya Taifa, Mrembo wa Tanzania kama ishara ya kuwakilisha Nchi yetu katika Mashindano ya Urembo ya Dunia ambayo yanatarajiwa kufanyika Johannesburg nchini Afrika ya Kusini hapo tarehe 13 Desemba 2008.
Vodacom Miss Tanzania 2008 Nasreen Karim anatarajia kuondoka nchini siku ya Jumapili tarehe 16 Novemba 2008 saa 4.00 asubuhi na ndege ya Shirika la ndege la Air Tanzania ambao pia ni Wadhamini Washiriki wa Shindano la Urembo la Miss Tanzania kwa mwaka 2008.
Waandishi wa Habari wanaalikwa kuhudhuria katika sherehe hiyo ambayo itaanza saa 4.00 asubuhi.
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI.
Waandishi wa Habari wanaalikwa kuhudhuria katika sherehe hiyo ambayo itaanza saa 4.00 asubuhi.
HASHIM LUNDENGA.
MKURUGENZI.
Duh, Michuzi, hiyo heading yako imenishtua !!! Nilidhani Miss T ndo keshatutoka tena, that is, anaagwa kwa ajili ya Mazishi, God Forbid.
ReplyDeleteNawashauri kina Lundenga wambadirishie ndege maana hawa ATCL hawaeleweki kabisa Mshiriki wetu asije akakosa shindano kwa sababu ya madege yao yasiyonauhakika wa safari Nadhani watanzania wenzangu mtakumbuka sanaa inayoendelea ATCL hivi sasa wanakalisha watu Airport bila kuwa eleza kinachoendelea.
ReplyDeleteNi Laurence MARSHAL??? I thought it was Lawrence Masha!! Kukosea majina ya watu ni offence na huyo waziri ni mwanasheria by profession, shauri yenu.
ReplyDeleteMh. Balozi na Mkuu wa wilaya ya nanihii,
ReplyDeleteHivi waziri Laurance Marshal ameteuliwa lini kuwa waziri wa mambo ya ndani? na yule Lawrence Masha yu wapi siku hizi?
Anon wa 3:46
ReplyDeleteKumbe na wewe ulishtuka kama mimi, hii heading nikajua kuwa Miss TZ 2008 is no more, nafikiri heading muafaka ingekuwa, "MISS TZ 2008 KUKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA IJUMAA" Hii kidogo inatafisida michu angalia utakuja shitakiwa kwa kudhuru kwa heading zako maana kama mtu ana presha lazima atapata mshtuko.
Laurence Marshal?
ReplyDeleteHuyu miss TZ si ndo yule alikuwa akiishi Lamada Appartments na wenzie?
ReplyDeleteAbt ATCL, BP wamewanyima mafuta ya mkopo ndio maana ndege zao zinaahirishwa kila kukicha, wana deni kubwa sana.