Mubaraka akiwa pamoja na Mama yake Mzazi Zuhura Jumanne
Mubaraka akiwa pamoja na Rebecca Brady kutoka Facingthe World Charity
Wanzilishi/Wawakilishi wa Association of Tanzanian Women in Diaspora(ATWID). Kutoka kushoto ni Makrina Kalinga, Susan Mzee, MubarakaJumanne, Zuhura Jumanne na Rebecca Brady

Mtoto Mubaraka Jumanne aliwasili Uingereza tarehe 14/11/2008 pamoja na Mamayake mzazi Bi Zuhura Jumanne, kwa ajili ya matibabu.

Wanahitajika watu wa kujitolea kuwajulia hali pamoja na msaada wowote wakati wakiwepo hapa Uingereza. Facing World Charity wanastahili pongezi kwa kumwezesha Mbaraka naMama yake kupatiwa matibabu ya muhimu.

Tafadhali wasiliana na Facing the World office kwa ajili ya maelezo zaidi katika namba zifuatazo;

+44 (0) 207 352 0052
+44 (0) 207 352 6702
+44 (0) 77 2035 0817

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Tunawapongeza kwa kuweza kumfikisha mgonjwa huko kwa matibabu,sijui kwa nini mmesahau kama ni rahisi sana kufanya matibabu india,zaidi ya hapo UK,anyway acha iwe ni utambulisho wa kazi za ATWID,muweze kupata misaada kwa wafadhili!!!

    ReplyDelete
  2. Nawapongeza kwa kazi nzuri.nomba kuuliza kwani si ujinga
    1. Susan mzee ni mke wa Ayub mzee?
    2. Huyu mgonjwa anaumwa nini???

    ReplyDelete
  3. Anaumwa nini?

    ReplyDelete
  4. Nashukuru hawa watu wamewezakuelewa kuwa nyama choma na ccm nchi za kigeni wameweza kutambua njia nyingine za maana na faida kwao ili waweze kupata umaarufu wanaoutaka nyama choma na uccm nikupoteza muda wenu tu.

    ReplyDelete
  5. aumwa nini??mtoto
    wee annon wa kwanza kwani umeambiwa wanataka cheapest treatment??eti wangeenda india??kilaza

    ReplyDelete
  6. Suzan Mzee ni mke wa Mbarouk Mzee na ni mwanasiasa machachari anaefanya kazi anayoipenda.

    ReplyDelete
  7. 1: Hiyo mambo haiko wasi...
    2: Huyo sweater waliomvalisa mboni (---)?

    ReplyDelete
  8. Mbona humtoi maelezo ya kueleweka, ina-bore. Huyo mtoto anaumwa nini? Ntaenda kumuangalia nikiwa sijui anaumwa nini?

    ReplyDelete
  9. WOTE NIMEWAELEWA LKN HUYU ANON NAMBA4 SIMUELEWE SIJUI NYAMA CHOMA SIJUI CCM HAYO YOTE YAMETOKA WAPI? MBONA HAVIENDANI NA MADA YENYEWE UNAKURUPUKA TU. WEKA JINA LAKO BASI NAWE UJULIKANE.
    MDAU
    KISIJU PWANI

    ReplyDelete
  10. ANAUMWA NINI ??? MBONA HATUJUWI STORY YAKY!!!!

    ReplyDelete
  11. Waliomleta ulaya ni NGO ya hao wazungu haihusiani kabisa na hiyo ATWID kama mnakumbuka hapo awali hawa wazungu waliomba watanzania wajitolee sehemu ya malazi ya huyu mama na kujitolea kumtembelea hospitali kijana labda ndiyo hao ATWID watampa tafu huyu mama kumliwaza. Je amefikia wapi au Suzana Mzee kamkaribisha afikie kwake? Tunaomba adddress tuje tumjulie hali mgonjwa. Mdau UK

    ReplyDelete
  12. Tupe historia fupi ya huyo mtotoAnaumwa nini mpaka apelekwe Ulaya??

    ReplyDelete
  13. wewe anany wa hapo juu unaotaka kutafuniwa umeze, si umeekewa website ya hito organisation. Hebu nenda ukaone mwenyewe, acha kupenda vya kutafuniwa wewe umekaa kumeza tuu.

    ReplyDelete
  14. jamani wabongo mbona maneno mengi Susan Mzee hahusiki chochote na huyo mtoto wala msaada wake , yeye kaenda tuu kumtembelea halafu kaweka picha kwenye blogu, hata na wewe ukitaka piga simu facing the world nenda kamtembelee upige hizo picha umpe kak michuzi kama atakutoa humu. Mana kaka Michuzi nae ana maswahiba wake , hata haya maoni yangu sijui kama yataona jua.

    ReplyDelete
  15. SUSAN MZEE NI MTAFUTA SIFA HANA CHOCHOTE.ALIJIFANYA MTAALAM WA IT KUMBE SIO.ANAGANGA NJAA NA KUTAFUTA UMAARUFU KWENYE MABLOG.

    ReplyDelete
  16. MY WORD!!!!!!
    ABSOLUTE NONESENSE! ABSOLUTE NONESENSE!!!
    WAOSHA VINYWA!! SAGENI CHUPA MBWIE USUKUMIZIE NA PILIPILI, WHAT A BUNCH OF STUPID PEOPLE, LOADS OF CRAP!!!. WEWE ANONYMOUS NUMBA (15)USIONGOPEE WATU HAPA, UKWELI NI KWAMBA SUSAN MZEE ALISEMA KUWA ANAFANYA KAZI KATIKA IT COMPANY - HP(HEWLETT-PACKARD) NA NI SENIOR WARRANTY/LOGISTICS SPECIALIST ALISEMA HAYA KWENYE MKUTANO WA UCHAGUZI WA TANZANIA ASSOCIATION(TA) TENA KWA KIINGEREZA, NA KUONYESHA AWARD ALIYOIPATA, SASA KAMA WEWE HUKUNYAKA LUGHA SHAURI YAKO, MSILETE UNAFIKI HAPA, ETI ANAGANGA NJAA NA KUTAFUTA SIFA KWENYE MABLOG, UNAJUA ANALIPWA MSHAHARA KIASI GANI(£££££)SIFA?? SIFA GANI?? ANAWAKUMBUSHA NYIE WAOSHA VINYWA KUSAIDIA WENZENU WANAPOPATWA NA SHIDA,
    POLE SANA MGONJWA MUBARAKA NA MAMA MZAZI, NIMEPIGA SIMU KWA HIYO FACING THE WORLD CHARITY NA KUPATA MAELEZO MAZURI TUPO PAMOJA NANYI TUTAKUJA KUWATEMBELEA NA KUWASAIDIA ZAIDI NA MUNGU AWABARIKI, SUSAN MZEE - SISI TUKO PAMOJA NA WEWE NA ASANTE KWA TAARIFA, USIVUNJIKE MOYO, UKWELI WAKO TUNAUJUA NA TUTAIELEZA JAMII NZIMA, HAWA MAFISADI WA KINAFIKI TUTAPAMBANA NAO. KILA LA KHERI, NI MIMI "USHUZI"

    ReplyDelete
  17. wewe unaongea hapo juu unaejua mpaka cheo cha huyo Susan Mzee huko HP, mimi nilikuwepo vilevile kwenye huo uchaguzi wa TA sikumbuki lolote isipokuwa tuu kaajiriwa kwenye IT company sasa wewe kukumbuka details zote hizi za miaka miwili iliyopita ni nani kama si mlengwa mwenyewe ? Susana acha uswahili unajijibia comment mwenyewe huu ni uswahili, kumbe unayataka wacha yakukute !! Mdau UK

    ReplyDelete
  18. Hivi hapa mada ni Susan Mzee ama huyu Mtoto ambaye ni mgonjwa Mubaraka Jumanne? acheni chuki binafsi, hatujengi bali tunabomoa, tujenge jamii yenye fikra na mwelekeo mzuri na kuwa mfano bora kwa kizazi chetu cha sasa na kijacho, tuanze kwa kumsaidia huyu kijana Mubaraka na wengine wote popote pale walipo.Tunashukuru sana kwa Ujumbe

    ReplyDelete
  19. Michuzi vuta Comment za huyu anayejiita ushuzi.asilete uhuni kwenye blog yetu. Susan ziko sehemu za kutafuta umaarufu sio kupitia ugonjwa wa huyo mtoto ambaye ameletwa na wazungu na nao hawahitaji msaada wa mtu.

    humtendei haki kijana mubaraka au wazazi wake. ndio kama umekwenda kumuona fine kitu kizuri ila kujiwekea comments za kujijenga sio jambo jema.wakati waliofanya kazi ni FACE WORLD. michuzi naomba huyu mtoto asitumiwe kama mtaji wa kisiasa. au kutafuta umaarufu.
    mdau-Reading

    ReplyDelete
  20. SUZAN HAFANYI HP ANAFANYA CARE READING, KILA CHAMA ANAPENDA AWE KIONGOZI HATAKI KUWA CHINI YA WATU, HAKUKUWA NA HAJA YA KUANZISHA CHAMA CHA WANAWAKE WAKATI TAYARI KUNA TAWA.
    KAMA ANAPESA ALIPIE JENGO LA CCM READING NI POUND 50 TU KWA WIKI.KWANINI CCM READING IMEOMBA PESA TOKA DODOMA KAMA SUSAN UNA PESA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...