Shoo kabambe ya sarakasi ya kwanza ya aina yake barani Afrika inakayojulikana kama Zain Mama Afrika Circus itaanza kuonyeshwa siku ya jumatano katika hema kubwa la kimataifa katika viwanja vya jeshi Masaki jijini Dar es Salaam. Shoo hiyo ya sarakasi ya kusisimua itakuwa ya saa mbili na nusu na itakuwa inaonyeshwa mara moja kwa wiki na mwishoni mwa wiki Jumamosi na Jumapili.

Mkurugenzi na muandaaji wa shoo hiyo, Winston Ruddle kutoka Zimbabwe, amesema sarakasi hiyo ya aina yake imedhaminiwa na kampuni ya simu ya mkononi ya Zain Tanzania na itakuwa na wasanii wenye vipaji wapatao 65 kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika ikiwemo Tanzania na itazinduliwa rasmi Novemba 26, mwezi huu.

“Ni shoo ya sarakasi ya aina yake. Kuna burudani mbali mbali 18 katika kila shoo. Tumejiandaa kwa kipindi cha miaka sita na tutawasisimua watazamaji wa rika zote kuanzia watoto hadi watu wazima. Tutakuwa na maonyesho yenye utajiri wa utamaduni wa Afrika,” alisema Ruddle.

Wasanii wote ni Waafrika. “Watazamaji watajionea wasanii wakifanya maonyesho ya aina yake na watapata thamani ya pesa zao,” alisema.
Hema kubwa la hadhi ya kimataifa lenye uwezo wa kubeba zaidi ya watu 1,000 limewekwa Masaki. “Itakuwa shoo ya kusisimua kuliko zote kufanyika nchini Tanzania. Wasanii, wanasarakasi na vionjo mbalimbali vitakonga nyoyo za watazamaji. Itakuwa ni shoo ya kukumbukwa. Wasanii wote wana vipaji vya kuzaliwa na wamepata mafunzo ya kina nchini Tanzania na nchi za nje. Wasanii watakaotumbuiza wanatoka Tanzania, Afrika Kusini, Zimbabwe, Kenya na Ethiopia na wana hadhi ya kimataifa,” alisema.

“Zaidi ya mavazi 500 ya kitamaduni yameandaliwa, vikaragosi na vionjo mbalimbali,” alisema Ruddle.

Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Costantine Magavilla amesema Zain inaona fahari kusaidia kuleta shoo hiyo nchini Tanzania. “Tunayo furaha kushirikiana na waandaaji wa shoo hii ya sarakasi ya aina yake ambayo itaanza kuonyeshwa hapa Tanzania Jumatano . Tunaamini Watanzania watasisimka na kufurahia shoo hii,” alisema.

Kutakuwa na maonyesho mawili kila mwisho wa wiki Jumamosi na Jumapili na onyesho lingine siku ya wiki ili kuwapa watazamaji muda wa kutosha wa kujionea sarakasi hiyo. Tiketi zitauzwa papo hapo Masaki kwa bei ya Tsh. 20,000, Tsh. 16,000 na Tsh. 8,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. jamani hawa wa dada wanaocheza hizi sarakasi wanaruhusiwa kuzaa? maana hii bingilibingili si inageuza na kuregeza viungo vyote vya uzazi kah!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...