wah. daniel yonah na basil pesambili mramba wakiwasili mahakama ya kisutu leo
wah. yonah na mramba wakiondoka mahakama ya kisutu kuelekea segerea
msafara wa kupeleka wah. segerea waondoka mkuku mahakamani.
stei tyund fo moo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. michuzi samahani na wadau nimeruka kwenye topic hii kwako issa michuzi na wewe weka kuhusu yako hapo dar-es-salaam piga picha za migahawa ya liverpool watumia kwenye website yao watakuwekea http://www.liverpoolfc.tv/news/drilldown/NG162237081125-1255.htm.

    ReplyDelete
  2. nyerere alsema hayo magereza yanawangojea wenyewe na akashauri wajitahidi kuyaboresha. haya sasa yametimia. Wizi mbaya jamani! wezi wa posta wanaona lakini?

    ReplyDelete
  3. Mh Mramba ndani ya lapa !! looo

    ReplyDelete
  4. Hawa jamaa wamekuwa kyika madaraka for too long, mpaka wakajisahau kuwa kuna watu wenye akili kama wao au kuzidi.Haya ndiyo matokeo yake.Liwe fundisho kwa wengine walio katika madaraka,sasa hivi hakuna kikao cha chama wala serikali kitakachowaokoa na fedheha hii, waangukieni wananchi na mrudishe mlichowaibia mpate kusamehewa!!!

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi naomba unisaidie kuelewa sawasawa...

    Hivi mshtakiwa anapaswa kuitwa MHESHIMIWA kweli? Anaheshimiwa na nani? Ina maana Hakimu atasema "Mheshimiwa mshtakiwa Mramba" kwa mfano?
    I don't think so!
    Tuliwaheshimu, wakatuona wajinga. Matunda yenyewe ndiyo hayo! Na wengine wanaoona ufahari kwa mali ya wizi, waangalie maana tunawaona.

    ReplyDelete
  6. Samahani Brother Michu pamoja na wadau wengine wote. Tusipotoshe kiswahili. Tunaomba isomeke "watuhumiwa" na si "waheshimiwa". Tunapotumia neno "waheshimiwa" badala ya "watuhumiwa" tunawapaka matope wanajamii "waheshimiwa"

    ReplyDelete
  7. Mzee pesa mbili hadi na malapa! hii kweli kali!

    ReplyDelete
  8. Anon 06:04pm
    Watuhumiwa ni kwamba hawana hatia mpaka watakapopatikana na hatia kwa hiyo hiyo mh. bado wanastahili. Isitoshe waheshimiwa karibia wote ni wezi tuu basi na wao wasitumie hii mh..
    Upuuzi mtupu mnaongea vitu ambavyo havina maana yoyote kwenye hii kesi.

    ReplyDelete
  9. Kutuhumiwa sio kupatikana na hatia, hizo ni tuhuma tu! Tafazalini acheni kuwahukumu kabla sheria haijachukua mkondo wake. Na hao bado ni wabunge hadi hapo watakapojiuzulu ubunge wao ndio hawataitwa waheshimiwa tena.

    Ahsanteni

    ReplyDelete
  10. HIYO NI AJALI YA KISIASA!!!

    ReplyDelete
  11. Kuna haja ya kuonyeshwa picha ya vyumba vya V.I. P vya Segerea na Keko!

    ReplyDelete
  12. MUOSHA naye HUOSHWA. Nafurahi kuona leo mtu aliyewadhika watu waliokufa kwa njaa na waliokoa maisha yao kwa kula mizizi na majani ambayo mengine yana sumu. Mungu amesikia kilio cha wote waliokufa kwa njaa wakati pesa za nchi zinanunua ndege pamoja na magari ya anasa. JK mungu akulinde,akupe moyo na nina imani ule msemo wa wako wa kila siku << unashangaa Kwanini watanzania ni masikini>>. Pia PCCB angazieni kwenye taasisi za umma kwani huko ndiko mabilioni ya walalaho yanapotokea. M1 baada ya M1 mpaka wote tuheshimiane. Nadhani sasa tutakuwa kama kambale, mdogo ndevu-mkubwa ndevu. Ni heshimu tu kwa kila mtanzania

    ReplyDelete
  13. Wanasheria nisaidieni. Hivi sheria ya Tanzania inaruhusu wabunge kupelekwa mahakamani; nina maana hawana kinga ya l=kisheria ("immunity")?? Maana ninavyofahamu kwenye nchi nyingi, zikiwemo hizi za Ulaya nilipo; ni mpaka mbunge aondolewe kwanza kinga aidha na spika wa bunge, bunge au raisi mwenyewe. Ni swali tu, sina nia ya kuchafua hali ya hewa maana kama ni rahisi namna hii, sijui kwa nini waliwachelewesha!

    ReplyDelete
  14. Acheni upuuzi nyinyi segerea gani wanakwenda na VX,Mzee wa kiona mbali naona kama hili ni changa la macho!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  15. HAPA KUNA KITU MBONA "WANATABASABU" Kwa mbali???!!! hawaonyeshi wasiwasi wala kushtuka au mimi??tu tumia dakika kadhaa kusoma "BODY LANGUAGE" katika picha zao zote......MHMmhhh

    ReplyDelete
  16. YES WE CAN!

    ReplyDelete
  17. nina comments mbili:
    1. Hawa ni watuhumiwa sawa na anan wa 6.04 alivyosema.
    Mtuhumiwa ni sio mualifu. Tofautieni hayo mawili

    2. Nataka kuona picha walipoingia segera. Kila siku picha zinaishia hapo kisutu tu? Kwa nini? Hamuruhusiwi segerea?

    3. Watuhumiwa hupelekwa segerea na VX/GX jamani? Sio ndinga za polisi ziwalepekazo? Mbona kunakuwa na double standard hapa?

    mtoto

    ReplyDelete
  18. hongera jk kaza buti kam vipi kam mbingu wa msarika tu hakuna kurudu nyuma

    ReplyDelete
  19. Ukiona Wabunge na mabarozi hata marais wakiburuzwa courtini, basi ujue "immunity" yao imeshaondolewa kwa manufaa ya umma n.k
    Tuombe jambo hili lisiwe kama mchezo wa kuigiza!! Kutufurahisha wanatarime na pia huko kwa wanatarime watarajiwa "Mbeya Vjj". Wanambeya jiandaeni, kuweni makini hasa ktk kipindi hiki kuelekea uchaguzi mdogo.Watanzania wengi wana matumaini makubwa kwenu ya kuleta mabadiliko ya kweli ndani ya nchi hii kwa vitendo, toeni fundisho kwa mafisadi. Wana sisiem waweza kufisadi haki zenu, kwa kujifanya wamechukizwa na jambo la ufisadi kumbe janja ya kutaka kujisafisha. Komaeni mpaka hukumu hizi zitolewe na kuchagua viongozi bora, maana viongozi bora tunawafahamu. Kazi kwenu...
    Ni hayo 2.

    ReplyDelete
  20. sikuamini,,,,nilipoona GX sijui inawabeba,,,nilicheka saaaaaana yan kwa hasira na gadhabu
    WHY?????????wamepewa dhamana adi wafatwe na shangingi la kifahari??mboni watuhumiwa wengine waingizwa ndani ya lile basi la watuhumiwa???
    annon alosema ivi picha zaishia tu mahakamani what abt keko/segerea??
    nyamafu kabisa,,
    lazima Muumba aingilie kati,,,ataeleta za kuleta lazima AFE,na ukoo wake wanye,,,labda wale tu wenye hofu ya Mungu
    kenge wekundu

    ReplyDelete
  21. MICHUZI,
    MWALIMU MMOJA WA SHULE MOSHI AMEFUNGWA MIAKA 58 JELA KWA TUHUMA ZA KUGUSHI MISHAHARA YA WENZIE NA KUJIPATIA SHS. MILIONI 4.2, SASA HAO MAFISADI WA EPA NA WA ALEX STUWART ITAKUWAJE???

    ReplyDelete
  22. Pale "Pesambilizzz" inapokuwa ndani ya "Kandambilizzzzz...

    ReplyDelete
  23. wakifungwa ndio itakuwa mikoba, CCM itapanda chati, watu watarudisha imani na chama na matumaini yatafufuka upya, JK fanya kweli safari hii. BUSH QUEEN

    ReplyDelete
  24. Hawa jamaa ndo wanasababisha tukimbie nchi yetu kwenda kuminyana na watu wengine kwenye nchi zao na wekeni nchi safi turudi tutakuwa wakimbizi wa uchumu mpaka lini

    ReplyDelete
  25. wizi mtupuuu

    sweet
    Arusha

    ReplyDelete
  26. jamani mi sijaelewa hawa watu waliwakuta wapi hadi wanawaleta mahakamani?Yaani mchakato wao mi haunipi picha halisi....naona kama kuna viini macho ktk huu mchezo.mtu wamuibue tu from nowhere halafu mahakamani!tena kwa shangingi GX!hivi hawa wanakaa pamoja au nani alianza kukamatwa kisha wakampitia nani-naomba ufafanuzi

    ReplyDelete
  27. JAMASI MSIWE WAJINGA. HII NI AJALI YA KISIASA. TUNAJUA FIKA KUWA YONA NA MRAMBA HAWAKUWA WANA-MTANDAO WA JK.
    KAMA NI UFISADI TUNATAKA KUWAONA KINA LOWASSA, KARAMAGI, ROSTAM.
    JK ACHA USANII

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...