KUNDI LA MAJAMBAZI MUDA MFUPI ULIOPITA YAMEVAMIA SHELI YA TOTAL ILIYOKO MAKUTANO YA BARABARA YA MOROGORO RODI NA KAWAWA RODI NA KUPORA KIASI KIKUBWA CHA PESA.
MMILIKI WA KITUO HICHO, GEORGE KRITSOS, AMBAYE PIA NI MWENYEKITI WA ZAMANI WA KLABU YA GYMKHANA, AMEJERUHIWA VIBAYA BAADA YA KUPIGWA RISASI UBAVUNI, NA AMEKIMBIZWA HOSPITALI KWA MATIBABU.
HABARI ZAIDI ZITALETWA PINDI ZIKIPATIKANA. POLISI WANAFANYA UPEPELEZI WA NGUVU KUYASAKA MAJAMBAZI HAYO AMBAYO KWA MUDA MREFU KIASI MATUKIO KAMA HAYA YALIPUNGUA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. SASA HAYA NDIO MATOKEO YA WAZIRI MASHA KUACHA KUFANYA KAZI ANAZOTAKIWA NA KUKALIA KUJIBISHANA NA BW. MENGI. HUYU MASHA HAJUI ANACHOTAKIWA KUFANYA KWENYE CHEO CHA UWAZIRI NI BORA JK AMPE UKUU WA WILAYA AJIFUNZE KWANZA.

    ReplyDelete
  2. Matukio hayakupungua. Ila jamaa walikuwa wanaoma ramani ya IGP mpya.

    ReplyDelete
  3. Walikuwa wanasubiri pikipiki zichoke.

    ReplyDelete
  4. ..kaka michuzi ahsante sana kwa kutuwezesha kupata ma breaking newz kwa sisi tulio mbali na nchi yetu...lakini hakuna kitu kama barabara ya morogoro rodi..naona hapo kidogo unarudisha nyuma kiswahili chetu...lakini ni kazi nzuri unayoifanya kutupa habari...

    ReplyDelete
  5. walijua kuna fungu pale mauzo ya j1,j2,,j3,j4 unadhani fungu dogo hilo. Ramani imechorwa hapo hapo na tabia ya vitajiri vya mjini kupiga dili zao kwenye mitandao watu wanawachora ati. Pole kwa aliyejeruhiwa na namtakia heri apone haraka

    ReplyDelete
  6. ukichunguza zaidi utagundua wakenya wako humo na ndo tunajifanya hatuwataki basi we ! mi hata kununua vitu vyao naona shida nilikuwa sijuii peptang tomato ya kwao yaani lilivyo ona tu eti proud kenya nikaiacha wenye tray nyambafu zao kudadadeki

    ReplyDelete
  7. ukichunguza zaidi utagundua wakenya wako humo na ndo tunajifanya hatuwataki basi we ! mi hata kununua vitu vyao naona shida nilikuwa sijuii peptang tomato ya kwao yaani lilivyo ona tu eti proud kenya nikaiacha wenye tray nyambafu zao kudadadeki

    ReplyDelete
  8. Bongo tambarare !!

    ReplyDelete
  9. matukio haya yanatokea kila siku huko Ngara, Biharamulo tena kinatekwa kijiji kizima, kwa nini nyie watu wa Dar ndiyo mnaona ni nyie tu mnastahili ulinzi? Can you imagine mtaa mzima wa Congo ukitekwa? sisi dhahama hiyo kila wiki inatukuta.Michuzi unajua na wewe ni elitist?

    ReplyDelete
  10. ujambazi umetokea wapi tena? mbona sielewi? bytheway bei zikoje huko usikute ni hasira za wananchi zimefikia pabaya kwa bei kuwa kubwa. kwanini wamuumize mwenye kituo na si wauzai?

    ReplyDelete
  11. Yuele MHILU amepona hapo? Au alishaachaga kazi?

    Mshkaji wangu namfamu huyo!

    ReplyDelete
  12. sheli ya total? au kituo cha mafuta cha total?, mahana sheli(shell) ni jina la kampuni ya mafuta kama bp,exon etc,sasa kaka michuzi kiswahili naona kina kuwa kigumu siku hizi,well lakini good job for breaking news,shukrani keep doing what you doing!!!!!

    ReplyDelete
  13. Balozi Michuzi msamehe tu huyo anon wa December 10, 2008 3:17 PM hapo juu. Inaonekana ni mgeni kwenye mtandao huu au huwa haji mara kwa mara.Hata mtaa wa Kongo wana kiswahili chao. Sisi tunashukuru kwa Hizo habari zilizovunjika sasa hivi, maana kuna watu wako hapo PPF tower lakini hawajui nini kimetokea, wananishangaa ninapowauliza kuhusu hili tukio.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  14. MTAJI WA MASIKINI...................

    ReplyDelete
  15. Nimependa maneno "Sheli ya total"

    ReplyDelete
  16. Inaelekea jamaa wa wa 3:17 hakupita JKT tulikokuwa tana vaa green vest ya kijani.

    ReplyDelete
  17. It’s about time businesses should employ surveillance cameras. It would be a matter of seconds for the culprits to be apprehended by the law when their faces appear in the media. If you can invest that much, why not put security a priority safety measure for the employees and your business.
    I pray that the victims get better and these fools arrested and face the law.

    ReplyDelete
  18. Tujenge upya wajibu na kazi ya Nyumba Kumi kwa usalama wa taifa!

    ReplyDelete
  19. silaha nyingi zilizopo bongo zimeingizwa kutoka nchi jirani zinazotutaka tuungane nazo.issues nyingi za kijambazi lazima zina mkono wa nchi jirani japo sio zote nimesema nyingi.kwahio tutegemee kusikia mambo kama haya mengi tu tukishaungana EA

    ReplyDelete
  20. MICHUZI KAKA YANGU NAJUA UMEMFAGILIA SANA OBAMA LAKINI HII SCANLE YA GOVERNOR WA CHICAGO UNAONAJE . NGOMA NZINTO HIYO MBONA HUONGELEI

    ReplyDelete
  21. Mimi ni MDAU wa everidei wa blog hii, sasa nikiona hawa wananchi wasioelewa lugha inayofanya tusikose kila asubuhi kupata break nyuzzzzz na habari kadhaa, huwa nasikitishwa maana unanafasi ya kuchangia na unataka kukosoa, MAIWAIFU WAKE, NA BASDEI YAKE YA KUZALIWA, WEWE ANON WA SAA 3;17 HAPO JUU UMENIBOA, KWANI BARABARA YA MORGORO ROAD, NDIO INAYOTULETA HAPA NA KUFANYA BLOG HII KUWA #1 KUNA BLOG KIBAO ZINA KISWAHILI KISAFI, HAPA MAISHA TAMBARARE NA LUGHA PIA!!!!KUHUSU HAO MAJAMBAZI, NDIO MAANA KUSISITIZE USALAMA WA MIPAKA YETU....OHHOOOO SINA MAANA MJADALA UNOENDELEA KUHUSU EAST AFRICA YA MASHARIKI, AU KUSEMA MAJAMBAZI WAMETOKA NCHI ZA JIRANI, ILA INABIDI TUDILI NA MATATIZO YETU YA KIUCHUMI NA USALAMA , KABLA HATUJAFUNGUA MIPAKA KUKARIBISHA MAJIRANI!!!!!!
    MZEE MISUP LIBENEKE LINAENDELEA NA LUGHA YETU NI ILE ILE KAMA KAWA!!

    ReplyDelete
  22. Wakenya hao.

    ReplyDelete
  23. CCTV HAIZIWII MWIZI KAMA VILE PILICE ASIVYOZUIA MWIZI WATANUNUA CAMERA NA BADO WEZI NWATAIBA TU, CHA MSINGI NI UMAKINI KATIKA UENDESHAJI WA KESI ZA MATUKIO YA AINA HII NA HUKUMU ZILINGANE NA MATUKIO YENYEWE, MTU AKILA MVUA 1OO HIVI NA ZIWE MIA KWELI AFIE HUKO HUKO JELA,PAMOJA NA SISI WANANCHI WENYEWE KUWA WA KWELI NWA NAFSI NZETU, TUNAWAJUWA AO NI NDUGU ZETU NI RAFIKI ZETU LAKINI BADO TUKO KIMYA TU. KUHUSU BARABARA YA MOROGORO ROAD, HUU NI MSAMIATI AMBAO UMEKUBALIKA KATIKA JAMII, UNAMUULIZA MTU UNENDA WAPI? NAENDA BARABARA YA MOROGORO ROAD ?9HILI LIMESHAKUWA JINA TENA, HATA HIVYO SI MAKOSA HIVYO NDIVYO INAVYOTAKIWA NA MAADA VIBAO VIMEANDIKWA MOROGORO ROAD MANANE HAYO MAWILI YAKICHUKUWA TASWIRA YA HIYO BARABARA, HATA SHELL SAWA HII NI KAMPUNI YA MAFUTA YA KIDACHI/HOLLAND NI YA KWANZA KUJA TANZANIA MIAKA MINGI ILIYOPITA SASA IMEZOELEKA KITUO CHA MAFUTA KUKIITA SHELL HATA KAMA NI CHA TOTAL, UNAMTUMA MTOTO MAFUTA YA TAA UNAMWAMBIA NENDO SHELL YA TANGI BOVU UKANUNUWE MAFUTA YA TAA, WAKATI TANGI BOVU KUNA BP/BRITISH PETROLEUM, NI KWAIDA NA NHAMNA MAKAKO YOYOTE KATIKA JAMII YA TANZANIA. HII NI MISEMO NA MAJINA YA KI- LOCAL, KWANI HUWEZI KWENDA JAPAN UKAMUOMBA MTU PAJERO AKAKUPA SHILINGI KUMI/WHATEVER, ATAKUPA GARI.

    ReplyDelete
  24. LAZIMA WATAKUWA NI WAKENYA TU. NI HAOHAO AMBAO WANATAKA KUHAKIKISHWA KWA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI. LAZIMA WATAKUWA WAO.

    ReplyDelete
  25. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

    ReplyDelete
  26. kweli hizi habari ni zakuvunjika.Mungu awaone hao majambazi wote.

    ReplyDelete
  27. wakenya haooooooooo wanja hodi ........ teh teh teh wapi mc nanihinoooooo

    ReplyDelete
  28. MICHUZI N'JOMBA USINIBANIE BANA WEEEE.
    MIE KILA CHIKU NIKISHOMA HABALI ZHAKO NAZIMIA KWA KICHEKO N'JOMBA OILE MBAYA.
    HIVI HAO MAJAMBAKAZI WALIVAMIA SHELL AU TOTAL? MBONA KAMA UNACHANGANYA UJI NA UGALI N'JOMBA. HAO NI WATU WAWILI TOFAUTI BANA.
    SHELL, TOTAL, BP HAZIKO PAMOJA N'JOMBA. NIMECHEMA TUUU UCHIKALIKE BACHIII.

    TENA UCHINIBANIE BANA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...