balozi mwanaidi maajar akiongea kabla ya onesho la jahazi usiku wa jumamosi

Kundi la Jahazi Modern Taarab jana liliweza kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa taarab Uingereza katika onesho lake lililofanyika katika ukumbi wa Silverspoon, uliopo pembeni ya uwanja wa mpira wa Wembley.

Katika onesho hilo mahsusi kwa ajili ya sherehe ya miaka 47 ya Uhuru wa Tanzania lilihudhuliwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaidi Sinare Maajar.

Kundi hilo liliweza kuzikonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa taarab kwa nyimbo kadhaa zikiwemo zilizopo kwenye albamu ya VIP, Two in one na nyinginezo zilizowafanya wapenzi kutotulia katika viti muda wote hadi mwisho wa onesho hili saa kumi alfajilr.

Kutokana na mamobi ya wapenzi wa muziki huo hapa Uingereza, Jahazi watafanya maonesho mengine Ijumaa ijayo tarehe 19/12/08 watakuwa katika ukumbi wa Lahore uliopo pembeni kidogo ya Job Centre,katikati ya mji wa Leicester.

Jumamosi taraehe 20 watakuwa Birmingham na Jumapili watawaaga wapenzi wao wa Uingereza katika onehso lao la mwisho litakalofanyika Milton Keynes.

mzee yusuf na vimwana wa jahazi wakirusha roho wadau wa london jahazi wakiwa kazini
umati wa wadau wakirusha roho na jahazi




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Ilikua show ya wanawake tu au wanuame hawataki kukosha roho zao?

    ReplyDelete
  2. Hii inaonesha kuwa jijini London kina baba bado tunatambua 'rusha roho' ni mahususi kwa kina mama, sie huwa tunawasindikiza ukumbini lakini mambo ya kutunza, kujishaua na n.k tunawaachia kina mama wasonge mbele kulikabili jukwaa kwa mbwembwe zote za kike.

    Sasa tunasubiri tuwaone mashabiki hao wakiwa ktk www.youtube.com video ya Jahazi Modern Taarab kutoa nakshi nakshi ktk muziki wa taarabu.

    ReplyDelete
  3. Hata mimi nilishangaa hadi nikachukua miwani yangu kutaka kujua kulikoni? Je hii ni halali - wanawake wajirushe pekee yao mbona hakuna wanaume>? Lol...ajabu lakini tuendelee kuishi.
    Wasalaam.

    ReplyDelete
  4. Mimi naomba kuuliza hizo LEBO za kwenye mikono ya suti za wanaume ni halali kuendelea kubaki hapo au unapaswa kuitoa baada ya kununua suti? Michuzi weka picha ya suti yenye LEBO tudiscuss kwangu ni kero

    ReplyDelete
  5. Aah hamjui kuwa London imejaa mamwinyi kutoka Unguja? ingekuwa Dar kwenye modern taarabu ungewaona wanaume wakirusha roho!

    ReplyDelete
  6. kwanza kabisa hii sio taarab, modern taarab ambayo kwa wengi tunajua kuwa ni vitu viwili tafauti, modern taarab ni uchumvi na matusi matupu. Sie wanaume tuliopo huku uk hatuoni sababu ya kujipeleka katika mafahali ambayo maudhui makubwa ni kuwafurahisha wanawake and let their hair down. kusema kweli modern taarab ni waste of time kwa mwanamme wa kweli, si mahali petu.

    ReplyDelete
  7. Jamani nyinyi munaoongelea wanaume kurusha roho ni watu wa wapi au hamujui maana yake? Tangu lini mwamumume aliyetimia akajiunga na kina mama kurusha roho. Kwa watu wa pwani wanaoilewa hiyo taarabu vizuri wakimwona mwanamume anarusha roho moja kwa moja wanajua kuwa mambo yamemharibikia.

    ReplyDelete
  8. wewe anonymous wa december 15 11:21 unguja inakuuma sana enh, watu kama nyie mmejaa tele, mnajidai kutoipenda zanzibar yetu lakini deep down mna wish ingekuwa mmetokea huko. ha ha ha

    ReplyDelete
  9. jamani wenyeji waambieni hao wakuja kuhusu uvaaji wa suti, na jaribuni kuwapa advice ya aina za suti. Mzee yusuf baada ya nyimbo yako kashfa zako zote kwa waliopo uk umekuja na kujipa kashfa mwenyewe kwa kushindwa kujua namna ya kuvaa suti ha ha ha ha ha ha ha ha ha haaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  10. LEBO ZA SUTI,,,hahaaaaaaa ni fashion yatakiwa iwe vile au?discus
    nani kawasafirisha kundi looote ili au walikua wangapi???
    mwanaume kidole juu haifai kabisa waweza kua "shoga" bure,mambo ya kike ayo

    ReplyDelete
  11. we unaye sema tukuache na unguja yenu unanitia kichefu chefu . aaaaah kunanini? acha ujinga hatuko kwenye malumbano ya ungunja na pemba hapa tuko kwenye jahaaaazi ndo maana umekwenda huko kwa mgongo wa kujilipua nyooooooo

    ReplyDelete
  12. Hongera sana wana Jahazi Modern Taarabu kwa kuburudisha watanzania walioko UK. Tunawapongeza na kuwatakia mafanikio mema katika hiyo ziara yenu ya UK. Tunawakaribisha pia huku Oslo kwa onyesho kama hilo.
    Wewe anonymous wa kwanza kabisa hapo juu ni mtu wa ajabu sana. Tunaanza kuwa na wasiwasi na wewe. Yaani mwanaume mzima unaongelea rusha roho? Unajua maana ya rusha roho lakini? Haya ni mambo ya akina mama. Wanapeana maadili ya kimama, mambo ya jinsi ya kukamata, kuwaburudisha, kuwalea na kuwastarehesha wanaume. Je wewe mwanaume mzima unayataka hayo ya nini? Unataka na wewe uwe unafanya kama wanavyofanya akina mama? Tuambie bwana!!
    Mdau wa Oslo

    ReplyDelete
  13. wewe uliyejibu issue ya uunguja, ume prove point ya mletaji issue yenyewe, kwani umesahau kuwa yeye alijibu hivyo kwa sababu mtu mmoja mwenye choyo kama wewe ndie alienzisha kwa kuitaja mamwinyi wa zanzibar katika topic hii. wacheni chuki. na alokwambia kama kila alo uk kajiripua ni nani? hiyo pia ni uchoyo wako wa pili. grow up you plonker

    ReplyDelete
  14. duh hiyo suti alinunuliwa haraka haraka? angalia inavyoburuta chini na ona viatu vilivyokaa kimaajabu ajabu?

    ReplyDelete
  15. HONGERA MAMA MWANAIDI MAAJAR UIFANYA UK KUWA YA WAMOJA UNAKUBALIKA HADI KWA WAPEMBA WATU AMBAO NI WAGUMU SANA.UMEONESHA MFANO BORA KUWA MAMA WA WATOTO WOTE.JK USIMWACHE MAMA HUYU NI HAZINA KUBWA KWA TAIFA LETU.

    ReplyDelete
  16. wewe anonymous wa December 15, 2008 4:26 PM mimi sikuanzisha mjadala huo wa unguja na pemba hapa ni mwenzio ambae ni small minded kama wewe aloanzisha nami nikamjibu. ikiwa una ufahamu mzuri ukirudia thread yote utaona wazi kama nimemjibu mtu na sikuanzisha mimi mjadala. pia usiwe na akili finyu za kuamini kuwa kila alokuwepo uk ni mkimbizi. amka unuse dongo la bongo.

    ReplyDelete
  17. Nimempata muungwana anae nijali miye..mapenzi yake dhamana twaheshimiana siiiye.........wallahi kma ukisikia hivyo na bado weye umeketi basi weye hamnazo.

    ReplyDelete
  18. Unguja, Unguja, kuna nini sasa huko Unguja? Unguja ilikuwa zamani sio sasa hivi. Hakuna lolote huko la maana ndio maana nyote mwakimbilia bara na wengine ndio mmekimbilia huko kwa bibi kwa mgongo wa CUF, kwani hatujui, mwatufanya wajinga, kama hiyo Unguja yenu nzuri kinachowakimbizia huko kwa bibi na kusubiri posho ya bibi kila wiki ni nini? Eeh au mwataka tuanze kumwaga mambo hadharani hapa! Sasa ngojeni na 'white paper' hiyoo iko njiani ikishakuwa sheria ndio mtakiona cha moto hakuna tena pesa ya bibi wala nini na ukitaka pesa ya bibi ukafanye kazi za kujitolea kwenye community. Si bora mgeenda kujitolea kwenye communities za kwenu! Subirini miaka yenu hata miwili haifiki,wote community work kama mnataka benefits!

    ReplyDelete
  19. mimi nimefurahiswa na hall,hall ndo ili sio party za U.S.A kubwa lakini mahall hovyooooooooooo.jamani kwanini waandaaji wa marekani wanatunyima raha?
    matangazo makubwa makerere mengiiiiiii.lakini mahall hovyooooooooooo.WHY?????????????.
    hall kama ili hata $mia kingilio watu tutakuja, michango inatolewa ya $ 100 mia tunanunuwa nguo za gharama tunaacha shughuli zetu,wengine mpaka wanasafiri,alafu hall bovuuuuuuuuuuu!!!!!!!!

    WHY WHY, WHYYYYY???????.

    ???????????????????????.

    ReplyDelete
  20. wewe unaewakebehi waunguja na kusema kuwa wako uk kwa mgongo wa cuf bila shaka hujui yaliopo uk, kuna idadi kubwa mno ya watanganyika vile vile waliojifanya wakimbizi. pia huna lako moja eti kumwaga mambo hadharani, haya basi ukumbi uko wazi mwaga ulichonacho tunakusubiri muongo mkubwa wewe, watu waseme na wewe useme!

    ReplyDelete
  21. Nishasema baada ya miaka 2 benefits hakunaaaa! woote kufanya kazi za kufagiaaa(kwa wale wanaoamka saa tano asubuhi wakisubiria benefits) na uzazi wa mpango juu sio kuwazalisha wake zenu watoto kibao, mtu ana watoto wanne au watano wote under 5, kisa benefits kama si unyanyasaji wa wanawake ni nini? Mmewageuza viwanda vya uvyotoaji watoto? Sasa angalau hao wanawake wenye watoto wadogo wakulea hawatafanya hizo community works. Lakini mliobaki woote baada ya two years ni kufanya kazi zitakazokuwepo job centres na kama hujapata kazi ni kufanya kazi za buree kwenye comminity mara 3 kwa wiki. Sasa kawaulizeni masolicitors wenu kuwa eti kuna mwongo mmoja kutoka Bongo kasema haya maneno kuhusu sheria mpya ya benefits! Halafu ndio utajua kama ni ukweli au uongo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...