Kundi zima la miondoko ya kidole juu Jahazi Modern Taarab toka Magomeni Mapipa, Dar, linatarajia kukonga nyoyo za Watanzania wengine London katika sherehe ya sikukuu ya Uhuru zitakazofanyika leo katika ukumbi wa Silverspoon uliopo pembeni ya uwanja wa Wembley.
Kundi hilo la wasanii 12 likiongozwa na kiongozi wake, Mzee Yusuph, liliwasili nchini Uingereza jana na kupokelewa na baadhi ya mashabiki wake katika uwanja wa Heathrow (T5), hali iliyoleta burudani baada kutoa burudani kwa kughani nyimbo 'Two in One'.
Mkurugenzi wa Masoko ya kampuni ya Jambo Publications iliyoratibu onesho hilo, kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania Uingereza ,Bw.Juma Makabkila alisema maandalizi yote ya onesho hilo yamekamilika na iliyobaki ni wakati kuwadia..
Kwa sasa kundi hilo linafanya taratibu la onyesho hilo la leo, na maonesho mengine bado hayapo kwenye programu yao, yatatangazwa usiku wa leo.Mgeni rasmi atakuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mwanaid Sinare Maajar.
Wanamuziki wanaokuja na kundi hilo ni pamoja na Mzee Yusuph ni Nasibu, Leila Abdallah, Fatuma Masoud, Miraji Mohamed, Musa Mkenda Musa, Jumanne Ulaya,Fikirini Urembo, Rashid Nassoro na Isha Makongo.
Kundi la Jahazi hivi sasa linatamba na nyimbo zake kama kazi ya Mungu haiingiliwi, nakula kwa nakshi nakshi’, Sichoki kustahamili, Shukrani ya punda,Katu hatorudi kwako, nimemshika habanduki, mtasema sana lakini hapa ndio amefika na nyingine nyingi.
Bwana Mabakil alisema katika hali isiyokuwa ya kawaida, tiketi kwa ajili ya onesho hilo zinekwisha na iliyobaki sasa wanauza tikti 150 za ziada ambapo ukumbi huo unaingiza watu 600 tu.
Alisema ili kuondoa usumbufu kwa wale wanaotoka mbali , amewataka kupiga namba ya simu hii (Hotline ) 07861351135 ili kuweza ku-book tiketi hizo mapema ili wasije kufika katika sehemu ya onesho na kukuta milango imefungwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...