Kaka Michuzi, nakuomba nipe japo nafasi, nipate kujibu shairi la yule alo kula pweza bila wasiwasi.
Usihofu niweke wazi kwani sina ninacho kificha. Pia shairi hili napenda litafsirike katika hali ya usanii na si vinginevyo.
Nitashukuru sana ikiwa utaliweka shairi hili barazani ili iwe ni njia ya kukuza kiswahili na pia kubadilishana mawazo.
Asante sana.

MTUZI: FANANI FULANI

Hishima natanguliza kwako bila ubaguzi,
Kisha nipewe baraza niliweke jambo wazi,
Yule alo kula pweza apate ufafanuzi
Wamsingizia pweza, ulicho kula ni penzi

Hii siri natangaza hadharani iwe wazi,
Wewe hukumla pweza, twajua tulo wajuzi,
Hujui? Hebu uliza, pweza havai mavazi
Wamsingizia pweza ulicho kula ni penzi

Sasa limekupumbaza walisimanga kwa tenzi,
Kama huku bembeleza, wapo wapishi wajuzi
Tayari wamelipoza, weye tuliza simanzi.
Wamsingizia pweza, ulicho kula ni penzi

Si samaki wa kwanza kuliwa na mwenye ujuzi,
Tia ndimu za Muweza, kisha paka tangawizi,
Kama unajiweza! Basi tia pia na nazi
Halafu karangizaa, kama wewe mfinyanzi,
Wamsingizia pweza, ulicho kula ni penzi

Hakika si mbaya pweza, usijifanye kinyozi,
Ukataka kumgeuza, bila kuwa na ujuzi,
Ataja kukuumiza, umdhanie mpenzi,
Wamsingizia pweza, ulicho kula ni penzi

Wahenga mi namaliza hili langu fafanuzi

Yule alo kula pweza ajue pweza si penzi
Akitaka kuuliza baraza hili li wazi!
Wamsingizia pweza uligho kula ni penzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. WALAHI YAELEKEA PWEZA HUYU ANA ASILI TA KITANGA NA LAZIMA AWE MTAMU ATI

    ReplyDelete
  2. Mpempe bwana weee....Mapenzi yamemshinda, amsingizia pweza

    ReplyDelete
  3. Pweza mwenyewe mikono miwili tu hana utamu wowote wino wake umekauka bwana next. Mbishani.

    ReplyDelete
  4. Hii blogu ya michuzi inatoa radha ya kitanzania hasa kuhusu haya mashairi yananikumbusha childhood kwani Radio Tanzania kuliku wa na kipindi kabisa cha mashaili malenga wetu kama sikosehi,Nategemea kuona mashairi mengi ktk blogu hii najua kuna vipaji kibao,hoyaa mdau michuzi kama vipi naomba niwe mtangazaji wa malenga wetu ktk hii blogu,teh teh teh teh.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...