Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Diplomasia mjini Maputo Dr.Patricio Jose akimpa zawadi ya kinyago JK baada ya kutoa mhadhara katika chuo hicho jana juu ya Mtazamo wa Tanzania Juu ya Jumuiya ya Maendelo ya Uchumi Kusini mwa Afrika SADC.Rais kikwete leo amehitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Msumbiji na tayari amerejea jijini Dar
JK akitoa mhadhara kwa wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Diplomasia mjini Maputo jana juu ya Mtazamo wa Tanzania Juu ya Jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC.

Mtaalamu wa utafiti katika kituo cha ukaguzi wa samaki katika bandari ya Maputo,chini Msumbiji akitoa maelezo kwa JK juu ya ukaguzi na uatafiti wa samaki unaofanywa na kito hicho.Msumbiji inauza samaki wake katika nchi za Ulaya


Mtaalamu wa Zao la Mpunga katika kituo cha Utafiti wa kilimo cha Umbeluzi,Boane nje kidogo ya jiji la Maputo Bwana Marcos Langa akitoa maelezo kwa JK juu ya uzalishaji wa mbegu bora ya zao hilo.Kituo hicho kina ushirikiano wa karibu na Vituo cha utafiti wa mazao vya Naliendele, Mtwara na Ifakara mkoani Morogoro




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. DPP amshangaa Makamba

    2008-12-17 13:54:35
    Na Muhibu Said


    Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Eliezer Feleshi, amepuuza kauli ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusufu Makamba, ya kutaka mjadala kuhusu watuhumiwa wa wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ufungwe, akisema kwamba kauli hiyo ni ya kisiasa.

    Feleshi alisema suala la watuhumiwa wa EPA, ni la kisheria, hivyo anashangaa kumsikia Katibu Mkuu huyo wa CCM akilihusisha suala hilo na siasa wakati vitu hivyo ni tofauti.

    ``Siasa na sheria wapi na wapi?`` alihoji Feleshi alipotakiwa na Nipashe juzi kueleza kuhusu kauli hiyo ya Makamba.

    Alipotakiwa kueleza kama kweli watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA wamemalizika, Feleshi ambaye yuko likizo alisema kwa ufupi: ``Kama umewamaliza wewe sawa.``

    Hata hivyo, wakati Makamba akisema kuwa suala la EPA limefungwa, juzi mtuhumiwa mpya katika kesi hiyo, Jonathan Munisi, alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu na kufunguliwa kesi ya kujipatia Sh. 2.6 bilioni kutoka BoT.

    Desemba 8, mwaka huu, Makamba aliomba mjadala kuhusu watuhumiwa wa wizi wa fedha kwenye EPA ufungwe kwa madai kwamba tayari watuhumiwa wote wamekwisha kufikishwa mahakamani.

    Alitoa kauli hiyo alipozungumza na wananchi katika Wilaya ya Karatu na Ngorongoro, mkoani Arusha katika ziara ya kukiimarisha chama chake mkoani humo.

    Makamba alisema anashangaa kuona bado kuna viongozi wa upinzani wanaoshabikia ajenda za EPA na ufisadi wakati wakijua suala hilo limekwisha.

    Makamba alisema kuna viongozi wa upinzani ambao wamekuwa wakipita mikoani na wakiendelea kulizungumza suala la EPA na ufisadi, hoja ambayo alidai kuwa imeisha.

    ``Ndugu zangu mjadala wa EPA na ufisadi umekwisha, Rais Kikwete tayari amechukua hatua, watuhumiwa wapo mahakamani, sasa hili jambo kila siku kuendelea kulizungumza ni ajabu sana,`` alisema Makamba.

    Alisema viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wanaendelea na `Operesheni ya Sangara` na kwamba kila kukicha wamekuwa wakizungumzia EPA na ufisadi ambao umekwisha kushughulikiwa na kusema kwamba: ``Umefika muda watafute hoja nyingine.``

    ``Mimi najua operesheni hiyo, ni nguvu ya soda na itakuwa `operesheni dagaa` siku si nyingi, kila siku EPA si imekwisha hiyo hoja,`` alisema Makamba.

    Makamba alitoa kauli hiyo siku chache baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuwaambia wahariri wa vyombo vya habari nchini kuwa serikali bado inashughulikia tuhuma hizo na kwamba mengi zaidi juu ya watuhumiwa wa EPA na Richmond yatakuwa hadharani hivi karibuni.

    Pia, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk. Edward Hoseah, aliahidi kuwa majina zaidi ya `sangara` wa ufisadi yatafahamika kabla ya mwisho wa mwaka huu.

    Hata hivyo, watuhumiwa waliofikishwa mahakamani, ni miongoni mwa walioshtakiwa kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi wa Sh bilioni 90.3 za EPA zilizohakikiwa.

    Pamoja na hayo, bado kuna watuhumiwa wa wizi wa sh. bilioni 42.6 za EPA, ambazo zinaendelea kuhakikiwa.
    Hivi sasa watuhumiwa 20 wa wizi wa Sh bilioni 133 za EPA walioshtakiwa, wako nje kwa dhamana.

    ReplyDelete
  2. Hao watu wa Msumbiji tunafanana nao sana

    ReplyDelete
  3. its kind strange to me, how come those details of mpungas, and how to process samaki, anapewa rais? i think he have alot of things to handle instead wahusika wa sectors hizo ndo wangekua beside wanakamata maelezo and soon they go back straight the go to work for that, badala ya rais arudi aitishe mkutano to explain them, thus why they always don't get it clear at all!

    ReplyDelete
  4. Jk labcoat limekutoa poooa bora ungekua daktari we unaonaje

    ReplyDelete
  5. Annon Dece 18: 11:39 nakuunga mkono.

    ReplyDelete
  6. nathani rais hapa anajaribu kuchek hwa watu ni wa aina gani,inawezakana haamini watendaji wake wa kazi mpaka kuamua kwenda huko.lengo na dhumuni ni kujaribu kuuangali mstakabali mnzima wa sadcc na kuangalia kama watanzania wanaweza vipi kufaidika as well as msumbiji.

    ReplyDelete
  7. Kusema ukweli Mkwere huyu anapiga pamba fresh sana.. Sijui tumwongezee kipindi cha tatu? Maana anakufanya uwe proud kuwa Mbongo.. Ila tu inabidi amwambie Mugabe aache kuwamaliza watu wake... He he he!!!


    Mdau, Boston, US

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...