Mimi ni mpenzi sana wa blog yako namoja kinachonivutia mashairi kwaiyo leo nimependa nikutumie hili shairi baada ya kukosa burudani kwa masiku kidogo.
naomba usitoe email yangu
Mdau
--------------------------------------------------------------------------

PWEZA
Pweza nimemkinai,kumla namkataa
Tena amenacha hoi, simtaki nawambia
Msije nita bedui ,unyongeni nitakuwa
Ukweli amenitesa , pweza simtaki tena.

Nilimpenda rohoni, kijijini kuhamia
Karibu na baharini, wavuvi kuwangojea
Kila wakitoka pwani, pweza niliwawania
Ukweli amenitesa , pweza simtaki tena.

Nikamfata sokoni, mnadani kununua
Bei sikujali kwani, pweza nilihitajia
Hujihisi burudani, kila ninapojilia.
Ukweli ametesa pweza simtaki tena.

Hukimbilia nyumbani, kupika nakazania
Namkosha pweza ndani, naviungo humtia
Humshemsha chunguni, nasupu nikajinywea
Ukweli amenitesa pweza simtaki tena.

Pindi ninapotamani kukaanga huamua
Mafuta sijali kwani kama yatanirukia
Hutaka awe laini, nasaladi hujilia
Ukweli amenitesa pweza simtaki tena.

Sasa tena sitamani, pweza nimemkataa
Kwenye yake madhumuni, mabaka amenitoa
Madawa hospitalini, wameshinda kunipea
Ukweli amenitesa pweza simtaki tena.

Waganga nadarubini, sababu wakanipea
Kuwa pweza sitamani, niko na aleji pia
Hataki tena mwilini, kakinai nawambia
Ukweli amenitesa pweza simtaki tena.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. pole sana mdau shairi lako ni muafaka...kwani yaliyokukuta si madogo..hata mie kipindi fulani pweza alinipa aleji lakini docta nikapata wa kunitibia sasa nakula kwa kujipimia.

    ReplyDelete
  2. Supu ya pweza ndio yenyewe, nanihii inakuwa hailali.

    ReplyDelete
  3. Jamani hili ni shairi na shairi linakuwa na maana iliyojificha ambayo mtungaji anataka wasomaji waumize akili zao kulichambua.
    Sasa hapa mtungaji anazungmzia PWEZA lakini ni pweza gani?

    ReplyDelete
  4. HONGERA MALENGA...UTENZI UMETULIA MNO. UJUMBE, VINA, VYOTE MUURUA...LAKINI NI ALEJI TU NDIYO HOJA AU?........KWANI MAMBO YA PWEZA S'MCHEZO BWANA! HAHAA
    MDAU
    JP

    ReplyDelete
  5. Big up malenga wetu,japo naona wasomaji wameshindwa kung'amua ujumbe uliopo, nionavyo mimi ujumbe unahusu onyo juu ya hili GONJWA HATARI-VVU,kama nimekosea nisahihishwe tafadhali.

    ReplyDelete
  6. mtoa maoni juu kweli,huyu jamaa anamaanisha Tahadhali ya ugonjwa wa UKIMWI,maana pale pia kasema alikuwa anajikaangia hata mafuta kumrukia hakujali,naona alikuwa ana maana hata CONDOM alikuwa havai anataka ale nyama yenyewe
    Umejitahidi Mahenga wetu Hongera

    ReplyDelete
  7. PWEZA
    Moyo kukinai,kuacha mbovu tabia
    taaban bin hoi, humtaki watwambia
    Hutaitwa bedui,pweza kumkimbia
    Pweza hatufai, wala kumkurubia

    Ulmipenda rohoni, na magesti kuhamia
    Pakavu na baharini, kote kuvinjairia
    Watokapo ndani,nawe uliwaipamia
    Pweza sote hatufai, wala kumkurubia

    Uliwafuta sokoni, kwa fedha kununua
    Bei poa jamani, mradi moyo kufurahia
    Hujihisi burudani, kila ukiparamia.
    Pweza sote hatufai, wala kumkurubia

    Kwa pupa nyumbani, kazi kufakamia
    kwa mziki na asumini, uturi kunukia
    Vifupi vigauni, na vidani kupambia
    Pweza sote hatufai, wala kumkurubia


    Kila ulipotamani, kuwa beep huamua
    Huwaita chumbani,Esta na Malia
    Hutaka wawe laini,urojo hujilia
    Huna kinga jamani, peku huingia

    kwa sasa hutamani, pweza wamkataa
    Miwasho mapajani, mabaka amekutoa
    Tiba hospitalini,bado haijatokea
    Pweza hatufai, wala kumkurubia

    Waganga na darubini,waijua sababu
    Mwili hauna amani,dhiki na tabu
    Kinga za mwilini, kufifia taratibu
    Pweza hatufai, wala kumkurubia

    Hongera kuamua, kwa msimamo thabiti
    Sote tungejua, majuto ni laiti
    Giza penye jua, ndio usmart
    Pweza hatufai, wala kumkurubia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...