Na Mwandishi Wetu
Mkutano Mkuu wa Sekta ya Utamaduni mwaka huu umepangwa kufanyika Mjini Morogoro kuanzia Jumatatu ya Disemba 15 Ijumaa ijayo ambapo wajumbe zaidi ya 300 wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermans Mwansoko imesema kuwa Mkutano huo utafanyika katika Hoteli ya Oasis mjini humo na kushirikisha wajumbe kutoka Idara, taasisi na Wizara na asasi mbalimbali kutokana Tanzania Bara na Visiwani.
“Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni Maadili ni nguzo ya Utamaduni wetu, na tunatarajia kuwa na wajumbe zaidi ya 300 wakiwemo maafisa Utamaduni wa mikoa yote, maafisa Utamaduni wa halmashauri zote, viongozi wa Mashirika ya Umma na na Binafsi, Vyama vya sanaa, asasi, Vyuo na Vyuo Vikuu pamoja na wadau mbalimbali,” alisema Mwansoko.
Katika taarifa hiyo pia Profesa Mwansoko amesema kuwa kwa kuzingatia umuhimu wa mkutano huo katika maendeleo ya sekta ya Utamaduni viongozi wakuu wa Wizara ya habari Utamaduni na Michezo watakuwepo wakiwemo Waziri, na Katibu Mkuu hivyo ni muhimu pia kwa watendaji wa sekta ya Utamaduni kushiriki.
Mkutano huo wa siku tano unafanyika kwa mara tano mfululizo ambapo pamoja na mambo mengine hupokea taarifa ya utendaji na utekelezaji wa maadhimio ya Mkutano uliopita kutoka kwa maafisa Utamaduni pia wadau na wataalam huwasilisha mada mbalimbali ambazo hujadiliwa na wajumbe katika jitihada za kutaka kuleta mabadiliko na maendeleo kwenye sekta ya Utamaduni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...