dukani mikocheni kwa mwalimu njia ya kuelekea rose garden ghorofa baada ya BP
vikwapazzzzzzz


deodorants

PAMBANA NA KIKWAPA
Kila mtu ana harufu ya aina yake na inasikika zaidi mtu akiwa karibu yako kama vile kwenye basi. Jihadhari isije kuwa nawe pia unatoa harufu kali ya kikwapa.
(I think everybody smelt something each time they are in close contact with another person in a crowded space. A good example would be when you are traveling in the bus. The smell that I get today inside the bus was so unpleasant that I start to wonder what it is actually? Maybe they smell me too but I don’t smell myself?)

LAINISHA NA NG’ARISHA LIPS ZAKO
Pendeza, lainisha ngozi ya midomoing’are na isichanike
(This diamond gloss enhances and colors lips with a high-shine glossy look).

JUA LINAZEESHA NGOZI – TUMIA MARY KAY PRODUCTS
Mionzi ya jua inazeesha ngozi sana hasa ngozi ya uso, tumia bidhaa za Mary Kay, zinasaidia sana.

(The Miracle Set is the age-fighting skin care collection proven to deliver dramatic results for soft, beautiful, younger-looking skin).
Jipatie Deodorants, lipgloss, Miracle set na vingine vingi toka

ARISE BEAUTY SUPPLY,
Tawi la Sinza –0754 270702
(mapambano karibu na Africa sana)

Mikocheni – 0754 270702 au 0784 456 046
Karibu na kwa mwalimu, pembeni mwa ATM ya CRDB

Au tuandikie
------------------------------------------------
kumbuka arise ndio wadhamini wakuu wa zawadi ya dola 500 ya mdau atayebahatika kuwa wa milioni 5 wakati wowote kuanzia sasa
ULE MUDA WA KUMPATA MDAU WA MILIONI 5 AMBAYE ATAPATA ZAWADI YA DOLA ZA KIMAREKANI 500 NDIO UNAKARIBIA KWA KASI NA WADAU MKAE MKAO WA KULA MAANA NAMBA INAKWENDA KASI SANA.

KAMA KAWAIDA JOPO LA WATAALAMU LIKO TAYARI KUFANYA VITU VYAKE VYA KUHAKIKI NA KUMTHIBITISHA MDAU YEYOTE TOKA POPOTE DUNIANI ATAYETHIBITISHWA NAO KUWA NDIYE WA 5,000,000.

KUMBUKA ARISE BEAUTY SUPPLY (PICHANI JUU) NDIO WADHAMINI WAKUU WA TUKIO HILI LENYE USHINDANI WA AJABU, NA TAYARI WAMESHAANDAA DOLA 500 KESHI KWA AJILI YA MDAU WA MILIONI 5.
KUNA UWEZEKANO MSHINDI AKAPATA BONASI YA PAFYUMU AMA KIPODOZI CHAGUO LAKE HAPO ARISE...

MASHARTI NI YALE YALE YA SIKU ZOTE:
1. TUMA UTHIBITISHO WAKO KUWA WEWE NI MDAU WA MILIONI 5 KWA KUBANANISHA KWENYE BARUA PEPE NA KUUTUMA KWA
issamichuzi@gmail.com UKIAMBATANISHA NA ANUANI YAKO KAMILI
2. UAMUZI WA JOPO LA MAJAJI NI WA MWISHO (HAKUNA KUKATA RUFAA)
3. MSHIRIKI ANAWEZA KUTOKA SEHEMU YOYOTE DUNIANI INAPOSOMWA GLOBU HII YA JAMII.
ANGALIZO:
KANYABOYA HAIRUHUSIWI NA WALA USIJISUMBUE. WATAALAMU WAMEJIANDAA VYA KUTOSHA KUHAKIKI MSHINDI HALALI KAMA ILIVYO KAWAIDA YAO. TARAKIMU ZILIZO CHINI KULIA MWA GLOBU YA JAMII NDIZO REFARII WA MCHEZO. KWA MAELEZO ZAIDI JUU YA ARISE BEAUTY SUPPLY

BAHATI NJEMA
-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Ni afadhali kukaa kimya kuliko kutuandikia kiingereza kibovu kama hicho.

    ReplyDelete
  2. Bongo watu wengi wananuka sana VIKWAPA, bora muende hapo Arise store mkanunue hizo deodorants na sio kututesa na VIKWAPA vyenu tunapotua Bongo. VIKWAPA vinakera, VIKWAPA vinanuka na VIKWAPA vinakufanya wala usitake kukaa na mtu karibu.

    Utakuta bonge la demu yaani mzuri kupindukia na aliyependeza kwa mavazi lakini ukimsogelea hatamaniki kwa kunuka KIKWAPA au unakuta bonge la jamaa na amepiga pamba kali lakini KIKWAPA chake kinanuka kama samaki aliyeoza. Tafadhalini jamani wala siwapigi madongo bali ni ushauri nasaha.

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli naomba nichangie kuhusu suala ya vikwapa. Ashukuriwe aliyetoa tangazo hilo....jamaniee Watanganyika tumieni hizo deodorant. Ni aibuuuu!, utakuta dada mrembo kila kitu lakini anatema kinoma noma harufu. Na matozi nao wanafuka balaa, serikali inapaswa kuingilia tatizo hili...ni kero kubwa kwenye mabasi. Haswa kwa sisi tunaorudi nyumbani kutembea, pamoja na wageni wanaotoka nje...kha hivi hawajisikii kunuka ama vipi?, Hata uoge vipi kwapa litatema tu...haswa kwa joto la daresalama. Solution ni hizo deodorant!!, siyo cologne, manaake cologne ina-mask tu juu juu...ikichanganyika na jasho ni mchanyato mwingine wa harufu ya kemikali za ajabu. Kikwete...toa stimulus rebate ya deodorants. By the way na wenye matatizo ya kunuka midomo, tafadhali nendeni kwa wataalamu wa vinywa, kuna solution.

    ReplyDelete
  4. JAMANI SASA KUNUKA KIKWAPA KUNATOKANA NA MAMBO MENGI. MOJA WAPO NI SPECES UNAZOKULA NA VINGINEVYO . NYINYI WENYEWE HAPA MAREKANI MNANUKA VIKWAPA SIO KWA AJILI YA JASHO SOMETIMES NI CHAKULA NA SPICES .
    NDIO MAANA KWA WAAFRIKA WANNAAONGOZA NI WA WEST AFRICA NIGERIANS .
    MUACHE HIO TABIA

    ReplyDelete
  5. Anon wa kwanza kabusa umekasirika kwa sababu umeambiwa kikwapa nini? unacho iko kikwapa ndo mana unakasirika eeeh. mbona iko kingreza kilichoandikwa kinaeleeka tu.

    anon mwengine apo juu kama spices ndio zinasababuisha au wateva kinachosababisha ndio kwa mana kuna dodoranti na pafyumu hi kwa ajii ya kumitigeti hio arufu regardless of the cause ya kikwapa

    ReplyDelete
  6. Yani hata mimi nimechoka na hiko kimombo....bora tutumie lugha yetu ya taifa ili tueleweke.

    ReplyDelete
  7. kunuka kikwapa is something natural and is beautiful, ndo maana mbuzi dume hufuata jike kwa harafu tu, it is very sexy, it is our natural thing,adds something in our naturality.

    ReplyDelete
  8. HIVI MICHUZI MSHINDI WA 5000000 MTAJUAJE KAMA NI ANONY, MTADHIBITISHAJE KUWA NI YEYE? NADHANI ANONY AKITUMA MAONI YAKE HAMNA KITU INABAKI KAMA SENT KWA UTAMBULISHO BAADAYE, IT NEEDS VERY DEEP UNDERSTANDING OF COMPUTER AND INTERNET PROGRAMS MAY MUAWATUMIE GOOGLE WAWASAIDIENI OTHERWISE I DOUBT THAT IT GONNA BE EXTREMELY HARD.

    ReplyDelete
  9. thanx for the info tafadhali tunaomba bei ya hizo bidhaa zako marry xmas issa michuzi

    ReplyDelete
  10. Jamani vikwapa vinaweza kuwa vya halufu nzuri au mbaya. Hivyo unapoongelea vikwapa lazima ueleze bayana ni kikwapa cha halufu ya perfume au halufu ya jasho. Lakini hata kama ni jasho huoni bongo joto kali?
    Unapowalaumu watanzania kwa vikwapa ni matusi makubwa sana, Mkulima kule vijijini anayeshinda shambani akihangaikia walau tu chakula. Unasema kikwapa kinanuka? Wewe uliye Marekani, UK, excellent job usidhalau wenzio. Yawezekana baba au bibi yako kikwapa chake kilikuwa kinanuka zaidi ya unavyofikiria. Msukuma mkokoteni je, Mvuvi pale ferry DSM, mpasua mbao je, mchimba madini kule merelani, Utingo/kuli je? Hawa wote wanapokuwa kazini unategemea halufu ya kikwapa chake iwe nzuri kulingasha na cha Grey Mgonja ambaye anaidhinisha matumizi ya pesa ofisini palipo na kiyoyozi na soft drinks all the time. Akitoaka ofini gari lenye kiyoyozi na akifika nyumbani vivyo hivyo. Jameni acheni kukashifu!!! Ni utofauti tu wa maisha. Deodorant inauzwa Tshs. 5000=, kipato cha mkokoteni kwa siku Tshs 500=. Je ataweza kuinunua??
    Mdau

    ReplyDelete
  11. We anonymous wa hapo juu mbona umeboa saana. Ndiyo maana Bongo hatuendelei, kuchekana kwingi mnoooo kuliko kusaidiana. Sasa mwenzio kaandika kiingeleza unamcheka baada ya kumpa courage. lugha inahitaji practice saana otherwise it dies naturally, the more you practice the more you become perfect. Tuache kuchekana huko ndio kunatuletea hofu ndio maana watoto wetu wanaogapa kupanua mdomo kujaribu kwasababu ya hofu ya kuchekwa na watu kama wewe. TUACHA IT IS NOT GOOD BEHAVIOR AT ALL!!!!

    ReplyDelete
  12. Nawapenda hawa jamaa wa Arise maana vitu vyao ni genuine nimenuna perfume na lips shine zao nzuri ingawa kuna bei kidogo lakini it worth every sent Sinza na Mikotcheni kote nimekwenda naamini watakuwa the best in town soon. Endelezeni kuleta hivyo vitu msije tu mkaleta vile vya China tutawashtukia ikijaribu.

    ReplyDelete
  13. jamani wabongo tumieni baby powder kama ni gharama deodarant hivyo vikwapa mnakuwa kama mabeberu bwana,nilikuwa likizo hapo yaani kuanzia airport wafanyakazi ni full kikwapa kwa kwenda mbele,na hamna kikwapa kizuri kandikeni ata powder ni cheap,next nikishuka nitamwaga sanduku la deoderant zima kwa staff wa airport.

    ReplyDelete
  14. Anon 6:07...acha kutetea tatizo bana, hata kama spices zinasababisha harufu tunachosema ni harufu ya mtu isikere watu wengine...sio ustaarabu. Whetever causes that smell....the point is it bothers other people around you... cover it up!. Naamini zipo njia za kiasili za kupunguza tatizo hilo, probably zipo deodorant za mitishamba.

    Tunaongelea zaidi wadau wa mjini (Dar) wengi wao wanauwezo wa kwenda baa kila jioni lakini hawataki kununua hizo deodorant!. Wasio na uwezo basi walau wajifukize UDI basi. Loh!. Na wewe Anon wa 8:01pm...negro, please!. That stench we're talking about here is DIRT, it is a rotten smell caused by bacteria. Ain't nothing sexy about it, it's GROSS. If you're talking about the natural clean scent your lover has right after shower...that's sexy. But five hours later, or after hard work...hell no. Nawashutumu pia wanaojimwagia marashi kupita kiasi, huo ni ushamba na ni kero kwa wengine pia. Do everything in moderation folks, extravagance ni haraam. Look, everybody has the right to live their lives the way they want...As Long As they Don't Interfere with my basic right to free, clean air. One's rights end where another's begin. Stink all you want, but don't come near me while you know we have to share a small enclosed space. This goes to smokers, too. I got news for you all...If you light it up in my presence...I will spit on your face. It's the same.

    ReplyDelete
  15. Ahhh,hayo maradhi yangu makwapa hapa najiuma mdomo,maana mimi kwa makwapa huna la kuniambia,na likitoka jasho au kama huyo jamaa anosema yananuka mimi ndio hunitoe kwapani,wakipita wanawake mimi huwatizama makwapa tu,kila mtu na maradhi yake,wengine makalio ,miguu na kadhalika mimi ndio mzee wa makwapa.

    ReplyDelete
  16. Jamani tuseme ukweli. Nyinyi wabeba maboksi na mayaya wa wazungu, wengi wenu mmejifunza kutumia hizo deodorant aidha Newala au Ukerewe. Tusisahau nyuma tuliokotoka. Mtushauri vizuri na sio kututukana. Ni kweli vikwapa vinanuka, stinks, nasty and disgustingly dirty.

    ReplyDelete
  17. dah annon wa kuzinguliwa/kupagawishwa na makwapa
    sii mchezo kijana yan ndo la-kustimulate harufu lile zito??
    hahahahaaaaaaaaaaaaaa u made my day
    i wont forget this ever!!

    ReplyDelete
  18. Vikwapa vinanuka sio siri. Kwa wale Day worker malipo kidogo hata wa vijijini washaurini kutumia limao ama ndimu. Ni kiasi cha kunyoa nyele za kwapani, kuoga na kukamulia hayo maji ya limao ama ndimu kwa wiki siku tano mwanzoni na baadaye unajipangia mwenyewe lini uweke na usiweke.Kwisha kazi, Maji hayo yana acid inayoaminika kuua bacteria wanaosababisha harufu mbaya hivyo watu wengi wanaweza kutokomeza kunuka kikwapa. sipingi hiyo biashara ya deodorant lakini kwa watu wa hali ya chini vilevile kwa wanaotumia deodorant lakini baada ya muda kidogo ni balaa hiyo ni njia madhubuti.

    ReplyDelete
  19. We michuzi umeshandaa ma-demu wako uwape hizi dola mia tano then mkutane bar mkazinywe. We Subiri uone. Piga ua, lazima au demu atayeibuka na hii hela. Halafu unatulletea za giza hapa kuwa atu JOPO la majaji liko tayari!

    ReplyDelete
  20. topik,, 'vikwapa'..hahahahhaha

    mie sina mbavu...muone huyo anony aliyesema..tangia alivyoshuka airport ni vikwapa..kwa kwenda mbele HAHAHHAHAHH..yaani nimecheka sana....

    asanteni jamani..kwa kutupa burudaniiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  21. Tanzania watu wengi wananuka vikwapa kwa sababu moja kuu ambayo wengi wakifuatilia itapunguza hili jambo

    Watu wengi wana high blood pressure lakini hawajijui. Hata uoge vipi, utumie ndimu, limao au deo kama bp yako ipo high na hutumii dawa au kufuata masaharti ukweli ni kuwa haitasaidia kitu. Na hizi deo zinaseal tu na sio kuondoa yote...hivyo ukiwa na kikwapa ukipaka asubuhi kabla ya saa sita mambo ni yale yale.

    Halafu vitu hivi viwili vinaenda hand to handy deo na body spray...Deodorant inazuia kutoa majasho kwenye kikwapa lakini harufu yake haikai mpajka jioni ...hivyo unatakiwa uwe na body spray ambayo harufu yake inalast longer kuliko ya deo.
    My 2 cents

    ReplyDelete
  22. Anon dec 18/11:29
    Bwana eeh...kila mtu anatokwa na jasho la kwapa. Wengine hutokwa zaidi ya wengine kwa sababu tofauti. Unaweza ukawa na High B.P lakini usitokwe na jasho kama baadhi ya wasio na High B.P. Issue hapa ni jinsi ya kupunguza kero kwa wengine ya harufu mbaya. Point yako si sahihi. Deodorant maana yake ni DEODORANT...as it De-odorizes (inapunguza harufu). FYI zipo deodorants zisizo na harufu yoyote. Zinazozuia majasho kutoka ni antiperspirants. Ukipata combination ni vizuri kwa mazingira kama ya Dar. Body spray kama ni deodorany it's going to help...lakini kama ni marashi tu...itakuwa overpowered na jasho kali kisha harufu mbili zitachanganyika na kuunda afuru ya ajabu. Mambo ya kemia hayo. If you like them body spray/colognes...please put it on after you apply deodorant. That will help.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...