habari za kazi bwana Michuzi

mimi ni mdau mkubwa sana wa Blog yako Kutoka Melbourne Australia
na napenda sana kusoma hii blog sababu ni ya jamii nzima ya Tanzania na wazalendo wote kwa ujumla. Kwanza napenda sana kuwapa hongera wazalendo wenzangu
kwa kusherehekea siku ya Uhuru na tuendelee kumuomba Mola azidishe
kutupa amani.

Swali langi kwamba hivi sisi watanzania tangu tumepata Uhuru tumekuwa watu wa amani na upendo na ushirikiano tunaishi kindugu. lakini sasa naona mambo yanazidi kuwa magumu au mabaya kwa upande wa serikali yetu nikimaanisha Mafisadi na wizi mbalimbali.

Hivi sisi watanzania hatuna wazo au fikra kwamba siku tuungane watanzania wote tuweze kudeal na hawa mafisadi????? tunaanza kuwakomesha mmoja baada ya mwingine labda wataogopa hao wanaotaka kuuanza wakijua watapata kibano.

wakati mwingine huwa nadhani kama tumerogwa maana maneno mengiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii lakini Vitendo hakuna inabidi siku tushikane mashati ili tuweze kukomboa pesa na taifa kwa ujumla.

MJADALA HUO UKO WAZI

Ni hayo tuu kwa leo

Mdau Melbourne.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. WEWE acha kuwa mnafiki, wewe hauko hapa nchini halafu unatuletea huu UPUUZI MTUUPU, sisi kama wananchi tunajua serikali yetu ipo na inatakiwa ifanye kazi, na kazi yao sio mpaka wananchi waungane TUNATAKA UTAWALA BORA na wa UWAJIBIKAJI.
    Nakuomba ukiwa kama mtu mwenye busara kwanza rudi nchini uonyeshe uchungu wako ukiwa hapa sio maneno matupu na kujifanya unauchungu sana na Tanzania, kwa taarifa yako wewe ni mchochezi unataka watu wapate hasira wachukue sheria mkononi humpati mtu kaka.
    NAOMBA serikali ifanye kazi mambo ya blahblah iwe mwisho,na sisi wananchi tusiwe wanafiki maana tunawachaguwa wenyewe kwa kupewa wali na kanga baada ya hapo unataka wafanyaje wakati umeshalipwa ulichohitaji na wao wanajilipa. TANZANIANS tuache kuwapa kura wasanii .NCHI imeeoza wote ni wasanii kama JK angekuwa anabusara zaidi si angechanganya sera basi na kusema kuna watu wengine wako upinzani wanauwezo nataka wanisaidie kny serikali yangu lakini hawezi na hato weza kufanya hivyo huo ni USANII MTUPU.
    mengine ntasema baadae.

    ReplyDelete
  2. Anan wa kwanza hapo juu safi sana. Huyu hawezi kubeba boxes huko na kujifanya anataka kupambana na UFISADI. Rudi hapa tuone meno yako yana makali kiasi gani!

    NI UFISADI uliotukuka kupambana na ufisadi ukiwa mbali hivyo!

    ReplyDelete
  3. Hivi nyinyi (ma-anony hapo juu) mna maana mtu akiwa nje ya nchi hawezi kuwa na mapenzi na taifa lake mpaka aje hapo bongo? Acheni roho zenu za korosho, na vinyongo visivyokuwa na msingi nyinyi! Mafisadi wengine ndio mnaanzaga hivyo hivyo. Ushauri: Anzeni kuwa na mapenzi na Watanzania (wananchi) wenzenu bila kujali wako wapi au vipato vyao.

    Kuhusu, maada naunga mkono wazo la wananchi kukasirikia mafisadi, wala rushwa na wanyonyaji!

    Mdau, Boston

    ReplyDelete
  4. Watu wengine wanapenda sana kujipendekeza waonekane wanajali kuliko wengine. Wewe umejificha huko Australia ukifanya vibarua halafu unajidai uko na uchungu na Tanzania juu ya UFISADI. Kabla hujasema serikali imekufanyia nini je wewe umeifanyia nini? Kwenda Australia! Unashauri wananchi waungane ukiwa na maana gani?????????Ndiyo kusema unatutukana watanzania kwamba hatujaungana? Mbona muungano uko imara na ndiyo maana chini ya rais wetu shupavu JK mambo yanaenda. Usituletee mambo ya longolongo za Australia. Kabebe mabox uweze kupata walau pesa ya kununulia digital kamera ili upige picha magorofa ya Astralia upate cha kuja kuonyesha ukirudi bongo!! Bongo tambarale rafiki yangu. Usifikiri ni kama unavyodhani!!
    Mdau

    ReplyDelete
  5. Mdau namba moja, mbili na nne naona mna tatizo kubwa la upungufu wa EXPOSURE kwenye ubongo wenu, ndio maana hamjui mlisemalo! Mtu akiwa nje ya nchi ndio asiseme kitu kinachomkera kuhusu nchi yake! Si ajabu mmeomba sana visa na mmenyimwa, sasa hasira za kula vumbi mnaleta kwa Michuzi blog! Grow up guys! No offence!
    Mdau,
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  6. We annon December 15 11:38 suala siyo kunyimwa visa wala kuwa na kinyongo na mtu hapa. Hapa ni ukumbi wa facts. Sisi hatuhitaji visa wala nini. Muda wowote tukiamua kutambaa tunatambaa kiulani tu. Lakini si tambaa ya box.

    Point yetu hapa ni kuwa huyu FISADI wa Australia anajifanya ati ana uchungu na nchi kwa kuandika message hii namna ile. Anatakiwa aseme yeye kama Mtanzania atalifanyia nini hili taifa. Kitendo cha kukimbilia box huku ukiacha mambo hayaeleweki ni aina ya ufisadi pia

    ReplyDelete
  7. Watu walio nje ya nchi pia ni watanzania na wana haki ya kutoa mawazo na kuonea uchungu tanzania kama watanzania wengine waliopo ndani na nje ya nchi
    mdau UK

    ReplyDelete
  8. Huu ndio ule wivu mbaya wa watanzania ukimuona mwenzio anajitahidi wewe unajaribu kumvuta chini. Akijenga nyumba, akinunua gari, akianzisha biashara ikibidi hata kumloga ili tu aaunguke. Ukilinganisha na wenzetu wivu wa kimaendeleo ni kujitahidi kufanya vizuri zaidi ya mwenzio. Mwenzetu ana kila haki kama mtanzania yoyote kuwa na uchungu na nchi yake.

    ReplyDelete
  9. MIMI SIJAONA JIPYA ULILOLIONGEA WEWE ULIETUMA HII ARTICLE, HAYO MAMBO NDO TUNAPIGIA KELELE KILA SIKU KWENYE MIJADALA MBALIMBALI LABDA KAMA UTATUSAIDIA MBINU ZAIDI YA KUPAMBANA NA HAO MAFISADI LKN KWA KUFUNGUA HUO MJADALA HAKUNA JIPYA LITAONGELEWA AMBALO HALIJAWAHI KUONGELEWA.

    ReplyDelete
  10. We annon Dec 16: 5:55 mchawi nini? Nani anakuvuta chini kwa kivipi? Ukienda chini shauri yako mwenyewe. Hakuna mtu anahangaika ,kukurogo labda wewe uwe mchawi mwenyewe.

    Mawazo yako tu. We piga kazi bila kuangalia nani anakuangalia. Kulialia namna hiyo ni dalili za woga na kutojiamini!

    ReplyDelete
  11. Unajua wabongo ni watu wa ajabu sana hasa waliopo hapa nyumbani. Sijui ni kitu gani kimewapata wa-TZ!! Yaani mtu analalamikia mafisadi, mafisadi wanaoleta umaskini wa kupindukia, wanaosababisha kusiwe na hospitali, maji, umeme, barabara, lakini bado wabongo wanawatetea!!!. Nadhani wabongo walioko nje wamefunguka macho, wameona kwamba nchi yenye huduma nzuri kwa jamii inawezekana: yenye maji safi, umeme, hospitals, elimu bora, nk inawezekana, ndio maana wanaona uchungu. Lakini wabongo walioko nyumbani wanaona kila kitu ni sawa tu, wamekata tamaa, wamebwaga manyanga, mpaka wanawatetea hao wanaowaangamiza!

    Na wala hawajui kuwa dunia imekuwa kijiji, eti aliyeko australia hana haki ya kuongelea nchi yake!! na hao wazungu walioko bongo je, hawana uchungu na nchi zao? na walioko Iraq, walioko Bulyankulu? Nani aliyesema aliyeko australia hatarudi tena nyumbani?. Nchi hii ina watu wa ajabu sana.

    ReplyDelete
  12. Narudi tenakama ifuatavyo, tena kwa wale mnajifanya mnauchungu wakati mpo NJE ya nchi, EMBU jiulize wewe hapo MTANZANIA ambae uko nje hivi kweli umeshawahi kuifikiria nchi yako kweli au unamapenzi ya kinafiki sababu huna jinsi,Nasema hivi kwa sababu, kama kweli umeenda kusoma na umejiona umefuzu na umemaliza huo ujuzi njoo nao hapa Tanzania tulisukume hili gurudumu pamoja sio kubaki kusema unauchunguuu na nchi hata kama UKO nje ya TANZANIA. Jamani tuwe wa kweli na tumuuogope mungu kama kweli unaipienda nchi yako RUDI uongezee ujuzi uliopata huko uje utusaidie hapa.Kimsingi mabwana wa UGAIBUNI kuwa na uchungu sio kwa kuusema bila vitendo embu changishaneni huko angalau msaidie hata gharama za watoto wasio na uwezi waende shule au basi zisadie hudumu za afya, mimi naona mnauchungu mwingi tena sana mkisikia MTANZANIA amefariki huko mtachanga hela za kumleta huku tena hela za maana but its a DEAD BODY kwanini msigeuze huo utaratibu ukawa wa maendeleo zaidi, eg kuna HISA huku zinauzwa mmeshachangishana mnanunua kwa manufaa yenu na taifa kwa ujumla, au kujaribu kuweka hela kny bank zetu za huku kwa kuziwezesha kuwa na mtaji wa kutosha na kuwapunguzia hata riba hao watanzania wengine waliopo hapa, fikirieni kwa undani sio kuleta mada ambayo haielezeki wala kuingia akilini,
    mwendelezo unakuja .....

    ReplyDelete
  13. Tena wewe anony wa hapo juu tena afadhali tuu unyamaze wee una undugu na mafisadi nini?? mbona unawatetea sana au huwa unaiba nao au wakiiba wanakukatia kitu kidogo maana unaongea pumba tuu. watu kuishi nchi za nje sio kwamba hatujui au hatukumbuki tulikotoka hapana na tunajua iko siku lazima turudi home. Home sweet home siku zote. Wewe unapigapiga kelele na hatutaacha kupiga kelele sababu kila mtu anatambua Tanzania tuna kila kitu kuanzia Migodi, Mbuga za Wanyama, Mito Milima na mabonde na maziwa makubwa kabisa na vyanzo vingine vingi na ambavyo tukitegemea tuu hivyo vyanzo vyetu na sisi tuna uwezo kuwa Taifa kubwa kama vila Marekani na mataifa mengine mengi. kwanini tukae kimya wakati watu wanakula kwa faida yao watu wanakuwa viongozi ili waweze kufaidi na matumbo yao na kujilimbikizia mali bila mpango na kusomesha watoto Ulaya. hakuna kitu kama hiyo hapa hawa wazungu wenzetu hakuna walichotuzidi sanasana tofauti yetu ni kwamba thinking capacity yao ni kubwa zaidi yetu sisi tuna nguvu ila hatufikirii kiundani zaidi. Mzungu akichunguza kitu lazima apate suluhu yake nini lakini sisi waafrica tutatoa sababu tuu ya kitu ili mradi kuona kimeshindikana. KWAHIYO SASA inabidi tujifunze kujenga mentality tofauti na tutaendelea tuu mimi na Imani na nchi yangu. Ila mabadiliko hayo yanaanzia kwetu sisi wenyewe kwa ndugu ,jamaa na marafiki pia na sio kwamba utalala na kuamka asubuhi ukakuta mambo yamebadilika hakuna muujiza kama huo, hapa muujiza ni sisi wenyewe kuchapa kazi kwa nguvu.

    Mdau
    Ughaibuni

    ReplyDelete
  14. sasa jamani niko nje nasoma, nikimaliza nitarudi nyumbani, nyie mnasema nimekimbia Bongo, sijui sina uchungu na nchi, sasa nisichangie mawazo yangu eti kwa sababu niko nje ya nchi nasoma??? nani kawaambia kwamba sitarudi nyumbani??? Au nikitaka kuchangia, inabidi kwanza nipande ndege nije Bongo, then ndio nichangie?? Think outside the box guys! No offence! Grow up guys!
    Mdau,
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  15. NILITEGEMEA UTASEMA MAMBO MAZURI KUMBE WATU UGHAIBUNI MKO HIVYO,
    kizungu cha kilevi kumbuka walisoma wengi nje na wakawa na uchungu kama huo ulionao wako wpai sasa. Acha ushabiki sababu huna kazi ya maana unauwezo wa kuingia kny NET na kuona maumbea ya bongo basi unachangia wajinga kabisa nyie.
    NTAWAONA mnaakili wote mkiwa hapo mlipo kuifanyia nchi yako mambo sio eti kutio michango, sisi tunalipa kodi huku unaona nchi inasogea ,HUU NDIO UCHUNGU naozungumzia mimi ,sio nyie mnasema online kisa mko UGHAIBUNI UPUUZI MTUUPU HUO.

    Naomba kizazi hiki kije hapa na usomi wenu ambao nategemea ni wa ukweli sio wa kununua vyeti bandia hapa na kuja kuingia siasa za njaa njaa.
    Hivi umeshajiuliza mwanao utamwambia nini wewe?umeenda nje kusoma kwa hela za nani??si ndio huo UFISADI, utawezaje mtu mtanzania safi usomeshwe nje ya nchi kama sio WIZI MTUPU. acha bwana hata kama ulienda vikwako na unajua utarudi unaweza rudi mfu nayo ni kurudi ila hutakuwa hujaifanyia nchi yako chochote zaidi ya kuuibia tuu.mkija na vishati vyenu vya sunday market mnajiona ndio mmentoka ng'ambo sio???

    NAOMBA kuwaambie nyie wa UGHAIBUNI fanyeni mnachoweza kufanya mkiwa huko huko tujue kweli walio UGHAIBUNI wako serious na TAnzania yao sio kulia humu, mnakaa kwa shida sana huko mkija huku vizungu vingi pumba imejaa kichwani nchi inazidi kudidimia hakuna la maana. Someni mambo ya agriculture,Engineering, UCHUMI mkirudi hapa mnawachallange hawa wazee waliopo ambao hawataki kubadili with proof.sio kukaa kusema unauchungu na tz.

    ntaendelea ukijibu =KIRIMORO

    ReplyDelete
  16. Ni kweli sisi tunaosoma nje ni vyema tuwakumbuke wa nyumbani ikiwezekana kuwaunganisha na ndugu jamaa na marafiki wapate nafasi ya elimu ya ughaibuni ili wote turudi kuinua taifa letu lenye utajiri wa ajabu. Ndivyo walivyofanya wenzetu kama Japan NK. Hakuna haja ya kulumbana tukiambiwa ukweli sanasana tutapoteza muda. Ndipo watanzania wenzetu wataona kuwa hatujioni sana kwa vile tumekwenda kusoma nje. Lakini walioko nyumbani msituone tunacheza.
    Mdau Ujerumani

    ReplyDelete
  17. This is so crazy,nimesoma hizi coments zote nimeona kitu kimoja ambacho kimeshakuwa cha kawaida kwenye hizi blog.Kuna mvutano mkubwa kati ya wa Tanzania waliopo nyumbani na wle waliopo nje ya nchi. Waliopo nyumbani wengi wao hutoa coment ambazo ndani yake unagundua ni wivu,hasira and all kind of negativity.Wanaongelea vitu ambavyo wala havina uzito oooh umerudi na shati la sunday market,ooh kiingereza just so stupid!!Wakati ni tofauti na wale wachangiaji wa nje ya Tanzania ambao wengi huongelea kitu halisi au kitu husika.Wewe uliye na hasira na wenzako walio ughaibuni kumbuka anaweza akawa ni mdogo wako,kaka au dada yako,rafiki yako au hata classmate wako,huoni aibu wala kujisikia vibaya unavyo hate. Talk about the real things which realy matter,open your eyes and be positive and the big thing stop hating!!
    Mtanzania Masomoni.

    ReplyDelete
  18. Mimi ndio Kirimoro:
    Unajua wewe anony:December 16, 20088:54 PM, naomba nikuhakikishie kuwa hatatuna hata hasira na wewe kuwa nje ya nchi ,1st tunajua unataabika huko nje ila ufanyaje ndio maana unakuwa unaulizia mambo ya nyumbani yamekaaje sio tu kwa kupenda kwako ila huna jinsi.kama kweli kilichokuuma ni kusema unakuja na vishati vyenu vya soko la j2 ni kweli jiiulize wewe uko huko ughaibubi unaichangia nini taifa lako?? KODI ulipi huo uchungu unautoa wapi wewe? hilo ndio swala langu sikatai usijue yanayoendelea huku TZ ila msijifanye mnauchungu wa kihivyo sana, la msingi ni mjitahidi kwa dhati kumaliza mnachofanya huko na kuja hapa nchi kupambana na haya matatizo lakini kumbuka walioliharibu taifa hili ni hao hao YES NO waliotoka ughaibuni ingawa sio wote.
    Kama wewe ni kijana na umesoma turudi nyumbani tukiungana hatushindwi kulikomboa taifa hili ila wote tuwe SERIOUS na PRODUCTIVITY then taifa litakombolewa. Tukianza kudai nchi yetu tajiri sijui nini haitusaidiii kabisa hilo linajulikana toka enzi hizo na waliotujulisha ni hayo ni hao hao wazungu na walitunyima ELIMU na ufahamu sasa kama wewe ni mfatiliaji sana wa mambo ya TZ utakumbuka BAba wa taifa alisema huu utajiri upo ila tusome kwanza akiwa na maana kuwa tupeleke watoto wetu shule kwa wingi wapate ufahamu na waje kulikomboa taifa matokeo yake waolipelekwa shule ndio hao hao MAFISADI sasa basi kama tukisoma na kukemeana jamani taifa hili sio la watu wachache basi tutalikomboa.
    NAWAOMBENI WATU WA UGHAIBUNI MSIJIONE MNASHAMBULIWA SIJUI LABDA NI CHUKI HAPANA NI KWASABABU TUNAIMANI MNAEXPOSURE NA VIJIELIMU NJOO BASI HUKU KWA WINGI MJE MUICHALLANGE HAO WALIOTUWEZESHA MPAKA TUMEFIKA HAPA. KULIKO KUKAAA HUMU KNY BLOG NA KUANZA KUONGEA HUWA YANAISHIA HUMU HUMU NA NDIO TATIZO LA WATANZANIA.
    NAOMBA NIKUPE MFANO MDOGO TUU,
    HAPA TZ TUNANYANYASWA HATA NA WAKENYA ,WAPO HAPA NCHINI NA WANAFANYA KAZI AMBAZO MTANZANIA ANAZIWEZA SASA KWANINI ANAAJIRIWA MKENYA,??? ILA SISI HATUWEZI KUPATA KAZI KWAO /SWALI NI KWAMBA WATZ NI WAOGA NA NI WAONGEAJI TUU KICHINICHINI HAKUNA VITENDO, TUNATAKIWA TUJE TUWAKIMBIZE HAWA NA WWENGINEO NAJUA TUNAUWEZO TUKIWEKA TOFAUTI ZETU KANDO.
    MUENDELEZO UPO, =KIRIMORO

    ReplyDelete
  19. Kwa wale wadau wanaosema kuwa, turudi, mimi nilirudi baada ya masomo ya juu ya biashara (MBA) Marekani. Hamna serikali wala tajiri aliyetaka kunipa mshahara wa mtu aliyesoma na degree ya MBA. Nikaanzisha biashara yangu lakini nikashindwa baada ya miaka minne ya kujitahidi kwa kuwa kila siku TRA yuko mlangoni, nikipeleka maratasi ya kodi, naambiwa haiwezi kupita bila ya kutoa hongo. Mpaka askari anakuja dukani "kuomba" msaada kwa ajili ya harusi ya mwanae.

    Mambo kama haya yanaendelea tangu uhuru. Serikali haijabadilisha sheria zozote zinazoweza kumlinda mwananchi wa chini wala mfanyabiashara. Bado sijaongelea matatizo ya umeme, maji, barabara mbovu, wizi, na elimu dumi ya watoto wetu. Nilishangaa niliposoma kuwa walimu wengi hawana cheti cha ualimu na wanafundisha katika mashule yetu hasa za binafsi.

    Kwa wale wanaosema kwa nini kazi wanapewa Kakenya, jibu ni rahisi. Wakenya wanajua kuchapa kazi, na ni wasomi. Kiingereza wanafahamu. Nchi yao ina vyuo vya Kimarekani na vyuo vyao vilianza kufundisha biashara na masomo ya juu ya biashara kama MBA na Ph.D tangu miaka ya sabini wakati sisi tunasheherekea Azimio la Arusha la kuwafilisi wafanyabiashara waliojenga nchi kwa jasho lao.

    Kwa kifupi, naipenda nchi yangu lakini sioni sababu ya kuishi katika hali ya maonevu. Tanzania kuna wasomi wengi, kuna Don wa kila aina hcuo kikuu lakini bado hatuwezi kujiendeleza na kutunga sheria za miaka ya 2008. Watu bado wanaonewa kila siku, iwe mahakamani au ofisi za TRA. Barabara bado ziko vile vile, polisi bado wanawaonea watu, ufisadi ndio usiseme, umeme matatizo, maji bado machafu, na elimu bado duni. Je, wadau hapa wanaosema rudi nyumbani uiendeleze nchi, niambie kwa nini wadau huko, wasomi wa hali ya juu kama hamwezi kubadilisha kitu chochote, mimi nitaweza vipi???

    Sasa niko nje zaidi ya miaka kumi na sina nia wala hamu ya kutembelea nchi yangu, na kama wadau watadai sina uchungu na nchi yangu, basi kama Balozi Michuzi anavyosena, " Kama Noma, ine Noma".

    Aluta Kontinua

    ReplyDelete
  20. WATU KAMA KINA KIRIMORO HAWATUWAKILISHI SISI WABONGO TULIOKO BONGO KWASABABU UKISHAKUWA NA LUGHA CHAFU BASI HUWEZI KUONGEA LA MAANA. WANAGOMBA MNO HAPA, WANATUMIA LUGHA ZA AJABU KAMA "VIJIELIMU, VIJISHATI VYA SUNDAY MARKET" N.K, SASA UNAJIULIZA MBONA WANA HASIRA SANA? ALAFU WANAFIKIRI NCHI INAJENGA KWA KULIPA KODI TUU, KWA KUWA NYUMBANI TUU, KWA HIYO KAMA UNASOMA AU KUFANYA KAZI UGHAIBUNI HUJENGI NCHI YAKO...WANAFIKIRI WACHINA NA WAZUNGU WENYE BUSINESS AU WANAOFANYA KAZI HAPA NCHINI HAWAJENGI NCHI ZAO!

    WATANZANIA TUAMKE, TUPANUE MAWAZO, UKIKAA HAPO ULIPO TU, BASI WAGENI WATAKUJA NA KU-COMPETE NA WEWE HAPOHAPO...WATACHUKUA KAZI NA BUSINESS HUKO WALIKOTOKA NA HAPO ULIPO, HIVYO BW. KIRIMORO INABIDI UWAENCOURAGE WATANZANIA WALIOKO NJE BADALA YA KULALAMA.

    ReplyDelete
  21. wewe kirimoro sijui nani huna point kabisa. Bado una akili za zamani kuwa watu wakiwa ulaya wanaosha vyoo, kubeba maboksi etc. Haya yalikuwa mambo ya 1960s-1980s. Siku hizi wapo waTz wanakazi za nguvu (mambo yamebadilika sana)ni elimu yako tu. Sasa hata wakirudi nyumbani..utawapa kazi wewe? Watarudi kama kuna kazi. Hiyo kodi unayolipa unaiona inatumikaje? Afadhali walioko nje wanalipa kodi ambazo zinakuja kama misaada huko!! Fungua macho na acha wivu na majungu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...