Khalid Mohammed ‘maarufu kama TID’ aliyekuwa akitumikia kifungo cha mwaka mmoja katika gereza la Segerea, sasa ni mtu huru baada ya kupitia msamaha kwa wafungwa uliotolewa na JK katika maadhimisho ya miaka 47 ya Uhuru.
TID ambaye Julai 23, 2008 alihukumiwa katika mahakama ya Kinondoni kutokana na kujeruhi, alikuwa ni mmoja ya wafungwa 4,306, walionufaika na msamaha huo ambao ni kwa mujibu wa Ibara ya 45 (1) (d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya msamaha huo, TID alikuwa amekata rufaa mahakama kuu kupinga kifungo alichopata, na kila mdau anasubiri nini kitaendelea; je, atafuta hiyo kesi ama ataendelea nayo ili kujisafisha jina?


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. jamani mbona huo msamaha haujamfikia babu Sea na wanae yaani wale watu wanatia huruma sana.

    ReplyDelete
  2. Kaka Michu Balozi la mtandao mkali wa Zain naomba kuuliza, Hii picha ni ya lini? kwani huko Ukonga na Keko siku hizi hawapitishi wembe kichwani ukitinga kwenye anga zao? au kwa vile alikuwa supa staa?

    ReplyDelete
  3. TID ACHANA NA HIYO KESI ISIJE IKAKURUDISHA JELA BURE, ATATOKEA HAKIMU MWINGINE AKASEMA ULITAKIWA KUFDUNGWA MIAKA MITANO NA SI MOJA AKAKURUDISHA LUPANGO UKALIZIE MVUA ZILIZOBAKI, NAKUHISI ACHANA NAYO.

    ReplyDelete
  4. wanapishana tu, mwenzake Nature ndio anakaribia kwenda huko. Leta tena utoto wa kulewa na bhangi halafu unapandia watu kichwani. Watu wana pesa za kweli wametulia nyie mnarukaruka tu. Acheni hizo, mkue sasa.

    ReplyDelete
  5. Raisi Wetu tunampenda vizuri kutolewa TID. RAisi je wezi wa kuku pia wameachiwaaaaaa isije kuwa wanawachiwa wanaojulikana tu Mafisadi wakubwa ndio huru. TID nafikiri utakuwa umejifunza kaka uimbe mistari ya mafunzo kwa vijana wadogo wacha sasa nyimbo zam ijigambo usiwe kama hawa kina Mwana FA watakupoteza. TID wewe muimbaji mzuri imba nyimbo sasa za msingi za maendeleo na nafikiri kuanzia sasa Kila sherehe za UHuru utaenda ila Tanznaia kweli aibu kusema uhuru mwaka 47. Rwanda toka vita miaka sita tu wapo mbali. Ndosi.

    ReplyDelete
  6. mdau hapo hamna kesi tena, jalada limeshafungwa mtu ameachiwa huru hakuna tena maana ya kuendelea kukata rufaa ya nini,ingawa hata hivyo ambacho alikuwa amekifanya ni kuwasilisha notice of appeal ambayo inaonyesha nia yake ya kukata rufaa hivyo hata rufaa yenyewe alikuwa hajakata, kwa maana nyingine haijulikani kama alikuwa anataka kukata rufaa kupinga nini, hukumu yote au ukubwa wa adhabu.Kwa jinsi facts za kesi zenyewe zilivyo mimi naona kabisa rufaa ya TID ingeegemea zaidi kwenye ukubwa wa adhabu sasa hakuna tena maana ya kuendelea na rufaa hiyo ingawa kama nilivyosema hapo awali alikuwa hajakata rufaa bado.

    ReplyDelete
  7. Mdau G2 wa December 11, 2008 7:55 PM pamoja na Anonymous wa December 12, 2008 4:08 AM

    Msamaha huo wa raisi ulikuwa na masharti kadhaa, ikiwemo wanaotumikia adhabu ya chini ya miaka mitano, na wawe wametumikia walau robo ya adhabu yao. Pia wale wenye umri wa zaidi ya miaka 70, wenye ukimwi au TB ambao wako mahututi ie terminal cases, na ambao kesi zao hazihusiani na mapenzi na mwanafunzi/kubaka

    Kwa mantiki hiyo basi, babu Sea, aliehukumiwa kifungo kirefu asingeingia humo kwenye msamaha. Kuhusu hao wezi wa kuku, kama walihukumiwa kifungo kidogo na ni kosa la kwanza, nao pia kuna uwezekano wa kusamehewa, mradi watimize masharti mengine yote.

    Msamaha huu hauchagui unafahamika au vipi, upo na hutoka kila mwaka kwa kuzingatia vigezo vile vile, tusijichanganye na kufikiria umaarufu wa TID ndio umemtoa gerezani, manake kuna magazeti ya udaku yaliwahi kuandika eti mtoto wa raisi anamuombea msamaha TID!!

    ReplyDelete
  8. hongera sana TID, life is experience kwenda jela kuna kitu umejifunza ndani yake kaza buti uku juu. Jipange anandaa shoo za kutembelea Tz zima na ikibidi ughaibuni na uhakika wanaokupenda na usiokupenda utaudhulia kwa wingi kuona nini utakifanya baada ya life in jail ... ndio time ya kuingiza mahela masela

    ReplyDelete
  9. Huyo TID na wenzie sasa waache mambo ya bangi na ukorofi mitaani na wazingatie tu mambo ya muziki na usanii. Wanapojiona wao ni watemi na kuanza kuhatarisha amani matokeo yake ndio hayo ya kutupwa gerezani. Babu Seya mbakaji na mlawiti hawezi kupata msamaha wa Rais Mtu kama huyo ni hatari kwa watoto wetu wa kike na kiume hivyo mwache tu aozee gerezani.

    ReplyDelete
  10. huu unafki tu,mtoto mdogo wa babu seya alifungwa akiwa chini ya miaka 18,kulikua hakuna ushahidi wowote kuwa babu seya alifanya hivyo vitendo,lakini kwa kuwa ni mkongo,na haki haipo hapa bongo,mzee ataishia jera.

    ReplyDelete
  11. Mnauwakika gani babu seya kabaka? ile ni kubahatisha mtu kweli anabaka na wanawe baba watoto wa 3 sijui wote mnambaka msichana mmoja? ingekuwa mtu na mdogo wake sawa ila baba na watoto na mwengine kafunga chini ya umri wa miaka 18 kaenda jela miaka 15 unusu kweli haki? siwamemuonea tu jela moja na mzee wake ile kesi ichunguzwe mie naona hasa hizi kesi za Ufisadi ziwekwe kwenye tv live tuone sababu walioibiwa si serikali peke yake na sie binadamu tuna haki tumepiga kura lazima tujue nini kinaendelea mahakamani kuhusu ile kesi ya EPA au mnaonaje wadau?

    ReplyDelete
  12. Anon 6:47PM wazo lake linamantiki; kesi za hawa mafisadi wote zingewekwa kwenye live Tv au ziwe zinawekewa kipindi maalum cha tv kama vile CNN-Investigation au kipindi kama AC360 wakialika analysts kwenye vipindi hivyo ili wengine wapunguze huo ufisadi, maana najua hautaisha.
    Hivi jamani TZ kuna kitengo cha kuchunguza wanaohujumu uchumi wa walipa kodi? Sijasikia hata siku moja hawa jamaa kuchunguza mapesa yaliojazwa kwenye account bila kujulikana yametoka wapi au biashara gani(legitimate business) na kama wamelipia kodi?maana nchi nyingine kudeposit dola elfu kumi tu wanaaanza kukufuatilia kuona kama income yako ni halali.

    ReplyDelete
  13. TID achana na kesi...ulifungwa kwa Haki. Jifunze na Ujirekebishe...

    ReplyDelete
  14. Ze pink t-shirt may bring different perception about you. Get your dressing togther bro....!

    ReplyDelete
  15. Jamani wewe anonnymous wa December 12, 2008 6:47 PM ndiyo kusema huziamini mahakama zetu za nchini, mahakimu, majaji na wataalam wote wa sheria walioendesha kesi ya Babu Seya na watoto wake mpaka ikaonekana wana hatia na baadaye kuwahukumu kifungo hicho? Hata kama mmoja wa watoto wake alikuwa na miaka 17, je kitendo cha kulawiti ni sawa? Hivi kweli ukikuta mtoto wako amelawitiwa au amebakwa na kijana wa miaka 17 utasema sawa tu endelea maana wewe unastahili kufanya hivyo!! Mimi nadhani waache tu waendelee na kifungo chao. Hii iwe fundisho kwa watu wengine walio na mpango na vitendo vichafu kama vya akina Babu Seya na watoto wake. Sioni haja ya kuhoji hukumu halali iliyotolewa na mahakama halali zenye wataalamu wenye nondozz zao za sheria.

    ReplyDelete
  16. Kweli! Hii kesi ya babu Seya hata me hainiingii akilini. Naona uonevu tu! Inabidi ichunguzwe tena, me sio mwanasheria lakini kila nikipiga mahesabu naona haikuji kabisa.

    ReplyDelete
  17. etiiiii naskiaaaa kwamba kesi ya babu seya na wanawe ni hasira ya mtu ivi baada ya kunyang'anywa donge mdomoni,,,kapigwa baoooo
    hahahaaaaa

    weee michu ole wako

    ReplyDelete
  18. aimbe tu! kesi itamrudisha lupango

    ReplyDelete
  19. NYINYI WATU MNAOSEMA BABU SEYA KAFUNGWA KWA UHALALI MMETUMIA UHAKIKA GANI KUSEMA HIVYO? NCHI ZILIZOENDELEA WANGEWAPIMA NDA KUHAKIKI SASA HUKO WAMEWAHOJI WATOTO HALAFU WANASEMA USHAHIDI. BONGO TUENDELEE ACHENI CHUKI BINAFSI KWA KUKOMOA WATU. HAITATUSAIDIA. IYO KESI ITIZAMWE TENE SIO HAKI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...